Nazgur
JF-Expert Member
- Apr 19, 2020
- 3,729
- 2,851
Habari wana jamvi,
Nimekuwa nikifuatilia mikutano yote ya CHADEMA, mara nyingi wanakuja na hadithi mpya na nyingi zinatungwa na washabiki wao hapa JF kisha mgombea anapanda nazo jukwaani.
Je, Chadema hawana Ilani yao? Nimejaribu kuingia Google lakini nimeona ya mwaka 2015. Je, mpya bado haijachapishwa au bado ipo kwenye vimakaratasi?
Kuna jambo lililetwa na mwana JF hapa kuwa kuna kifungu kwenye katiba yao kinasema kitatungiwa Sheria kwamba endapo mwanamke atalalamika police kuwa mwanaume amefanya mapenzi nae bila ridhaa yake basi atakuwa amebaka.
Tulitaka ufafanuzi wa jambo hilo kwa mgombea, atuambie je huyo mwanaume yeye atakuwa na haki gani ya kujitetea endapo atakuwa amesingiziwa au ananyanyaswa na huyo mwanamke?
Pia, kuna kifungu 84 cha madini ambacho kimeongelewa na ndugu pole pole kuhusu rasilimali madini kuwekwa rehani.
Je mgombea anasemaje juu ya hilo na tunataka kusikia akikisoma kutoka kwenye ilani yake na si majibu ya mtaani.
Pia, Chadema ilani yenu si mkataba kwa wananchi bali ni maneno ya kwenye mitandao ndio ilani yenu?
Tunataka majibu hayo, kwanini hamtembei na ilani yenu kama reference ya mnachoongea na mkitupa ufahamu kuwa hayo yanatokana na kifungu gani kutoka kwenye Ilani yenu ili tuwaamini?
Chadema na mgombea wenu acheni dharau kwa wananchi, toeni ilani ili tujue kilichomo.