Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Katika siasa huwa kuna symbolism au utambulisho wa kisiasa na kimamlaka.
Ukisoma maandiko utakutana na nabii mkubwa kabisa wa wana wa Israel Musa akiwa na fimbo yake ambayo kama tunavyofahamu ilitumika kupitishia miujiza mikubwa kabisa ya Mwenyezi Mungu.
Hapa kwetu Tundu Lissu na yeye amejikuta akishikilia fimbo kila afanyapo mkutano. Naamini hiyo fimbo inamsaidia Lissu kumpa sapoti kutokana na kujeruhiwa sana kwa risasi kwenye miguu yake, lakini sisi wadadisi wa mambo tumegundua kuwa hiyo Fimbo pia inasaidia sana kumpa haiba Tundu Lissu.
Hii Fimbo inanikumbusha fimbo ya Musa kwa Farao, na inasymbolize ukombozi kwa Watanzania kutoka katika mikono ya udhalimu na utawala uliojaa jeuri na kiburi wa CCM.
Kwa jamii za Wafugaji, Fimbo hutumika kwa kujilinda dhidi ya wanyama wakali, kujilinda dhidi ya adui na kuihami familia. Fimbo ni alama ya heshima kwa mwanaume.
Nawapongeza sana waliomchagulia Lissu mavazi, Ile Lubega anayovaa kwenye mikutano yake na Fimbo anayoshika ni Ishara ya utamaduni wa mwafrika na inaonyesha kuwa yuko tayari kubeba majukumu ya Ukuu wa Kaya.
Lakini hii Fimbo ya Lissu , kama ilivyokuwa fimbo ya Musa inaashiria mwisho wa utawala mbaya kabisa wa JPM
Lissu hiyo fimbo usiiache popote utakapokuwa kwenye shughuli hizi za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu!