Pre GE2025 Tundu Lissu na hoja zake dhaifu dhidi ya Serikali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lissu Yuko sawa, Tanganyika tusipo badilika Kuna uwezekano mkubwa watoto au wajukuu zetu kuja kuwa manamba ndani ya nchi yao.
 
Tuongee bila jazba, kwa sababu wewe uko sahihi, na Tundu Lissu yuko sahihi.
Kwa hoja yako hii, kama Dar es Salaam ina Wabunge 10, itakuwa vizuri Mtwara, ambako ndiyo MAKAZI yangu, tuwe na Wabunge WATATU au WANNE.
Hapa maana yangu ni kwamba hii ni HOJA INAYOFAA KUZUNGUMZWA, kidemokrasia.
Tufike mahali tuisemee Nchi yetu.
Mama Samia asikilizwe.
Tundu Lissu asikilizwe.
Wewe usikilizwe.
Mwisho wa siku yafanywe yale yenye manufaa kwa Nchi yetu Tanzania
 
Mimi ni muumini wa amani, Utulivu, ustawi na maendeleo, nitapambana na kiashiria chochote kinachotaka au kuashiria kuiondoa amani ya Taifa hili na Utulivu wake, ambao umepelekea ustawi mzuri katika kuvutia wawekezaji, hakuna mwekezaji atafurahia vurugu, fujo kwa upuuzi huo utapelekea shughuli kusimama, uchumi kudumaa, viwanda na makampuni kupata hasara na mengi tu, Govt should take it seriously, peace, peace peace!
 
Kampigeni tena risasi nyingine nyingi zaidi
 
Kulinda na Kuitetea amani yetu sio jambo la kuoneana huruma bali ni jambo la msingi kabisa, lenye uzito tofauti kabisa na mambo yenu ya katiba na uchaguzi
Katiba ina Athiri vipi amani ya nchi?
 
Katiba ina Athiri vipi amani ya nchi?
Kila mmoja wetu ana perception yake juu ya katiba yetu, binafsi naona ipo vizuri sana, mwingine anaona mbaya kabisa, swala hapa ni mitazamo na mapokeo yaliyopo ndani ya katiba kutegemeana na uelewa wa mtu mmoja mmoja! (wote tukiiona nzuri) Pana shida hapo!
 
Umenena vyema lakini tukitaka katiba mpya iliyoboreshwa zaidi ina Athiri vipi amani ? Kama ulivyodai hapo juu?
 
Umenena vyema lakini tukitaka katiba mpya iliyoboreshwa zaidi ina Athiri vipi amani ? Kama ulivyodai hapo juu?
Katiba ni kitu ambacho hakijawahi kuwa sahihi hata siku moja, hata ya America, hii ni kutokana na mitazamo tofauti ya kibinadamu, - - Angalia Kenya, - -
 
Katiba ni kitu ambacho hakijawahi kuwa sahihi hata siku moja, hata ya America, hii ni kutokana na mitazamo tofauti ya kibinadamu, - - Angalia Kenya, - -
Sijakataa , pia katiba zinaboreshwa kulingana na wakati , nchi nyingi tu duniani zimefanya hivyo na kupata matokea chanya .

Ninachotaka kujua ni hapo juu umedai , mnalinda amani ya nchi kuliko hayo mambo ya katiba na uchaguzi , nikakuuliza madai ya maboresho ya katiba yana Athiri vipi amani ya nchi?
 

Pitia hizo takwimu (ignore upuuzi wa majimbo ya Zanzibar), yapo kwa sababu ya kunyonya tu bara.

Hoja ya Lissu aina mashiko hasa kwa bara ya kuwa majimbo yagawanywe kutokana na idadi ya watu.

Hiyo ni impossible kwa rural Tanzania watu wachache wametapakaa katika eneo kubwa na wote hawafiki łąki mbili kwengine ni łąki na nusu. Ukisema hiyo ndio baseline.

Dar Es Salaam ambayo inamezwa na Tabora 55 times, Iła kwa population yake kubwa Dar inatakiwa kuwa na mara mbili ya wabunge wa Tabora (that doesn’t make sense).

Sehemu pekee itakayofaidika na idadi ya wabunge ni miji mikubwa kama Dar, Arusha mjini na mwanza mjini.

Bado kuna gharama za mishahara ya wabunge.

Ni hivi watu wanaangalia mambo kama population density, uchumi wa eneo, upatikani wa elimu, afya na crime rate. Maeneo yanagawanya kwa misingi hiyo kutokana na population density ya eneo husika.

Uwezi kukuta eneo la mjini na rural lina idadi ya wapiga kura sawa hata siku moja. Hata huko USA anaposema colleges hazina idadi sawa ya wapiga; same na UK hivyo hakuna jimbo lolote la rural linaweza kuwa na wapiga kura sawa na majimbo ya mjini.

Ni vitu ambavyo Lissu anatoa kichwani kwake.
 
Hivi hivi vitu umetoa kichwani mwako au umecopy mahali. Sidhani kwamba Lisu hana Akili pia sidhani kama watanzania hawana akili, Mimi nasema twendeni tutafika.Watanzania mbele yasafari watapembua pumba zipi na mchele upi. Lisu hata bila kufanya kampeni yoyote ile hakuna mtu atakwenda kupiga kura kwa mfumo huu hata hao CCM wenyewe ingawa masanduku yatajaa kura na washindi watapita kwa kishindo tena kwa asilimia 98 na wapiga kura itaonyeshwa wamejitokeza kwa asimia 150. Kwahiyo hao ndiyo viongozi tutakao wapata ACT watapewa viti vitatu vingine zanziba, Cuf watapewa viti viwili Mtwara, CDM safari hii watapewa viti 5 na chauma watapata mgombea mmoja. ADC mgombea wake wa uraisi atapewa ukuu wa mkoa. Uteuzi umeisha sio uchaguzi ni uteuzi.
 
Desk issue, kukaa na kujadili, ndiyo msingi wangu mkuu, wanaposema "uchaguzi hautafanyika hapo ndipo jinai inapoingia" nilitegemea Makatibu wakuu wa vyama waitane wakae, waone wanafanyaje?, - - hatua kwa hatua--, kufikia kwenye kwenye lengo sahihi na hatimaye kuyawasilisha katika ngazi husika.
 
Huwezi kuweka kigezo cha perception kwenye kitu kibaya.
Kwa hiyo wewe unaweza kwa perception zako ukaona tukio la mtu kubaka ni jambo Zuri.
Katiba yetu ni mbaya hilo ni suala ambalo lipo wazi
 
labda useme aje na kile unachokitaka wewe na kuridhisha upande wako na ccm
 
Wingi wa Wabunge katika Mkoa wowote hauna faida yoyote kwa Wananchi.
Kama Mkoa wa Tabora, ambao ni mkubwa mara tatu ya Nchi ya Rwanda, ina Mkuu wa Mkoa mmoja, kuna tatizo gani kuwa Wabunge 2 au 4?
Kwa nini tuwe na Wabunge 300, wakati Wabunge 35 au 70 watatusaidia kuokoa sehemu ya Kodi zetu zinazotumika kuwalipa Mishahara na Posho?
Hoja yangu ni kwamba, kuwa na Wabunge wengi ni hasara kwa Taifa.
Na kuthibitisha hili, idadi ya Wabunge ndani ya Ukumbi wa Bunge huwa haifiki Asilimia 50.
Kisha idadi kubwa ya Wabunge wanaishi nje ya Majimbo yao.
Tanzania haihitaji Wabunge 300.
Tanzania inahitaji Wabunge wasiozidi 75.
 
Mbona kama vile huna akili kabisa...!??

Swali la msingi unalopaswa kulijibu ni hili: Kwamba, msingi wa representation huwa ni watu au vitu...?

Kama eneo ni kubwa lakini Lina population ndogo, unaweka representation ya Wabunge wengi ili wawakilishe nini? Misitu na milima na nyika..?

Are you really thinking properly au ndiyo hivyo tena mlishavurugwa na mentality ya uchawa...?

Kwa kanuni ya NEC walioitoa juzi kuwa ktk kugawanya majimbo watazingatia idadi ya watu (600,000 kwa mijini na 400,000 kwa maeneo ya vijijini) unadhani Zanzibar yenye population isiyozidi 1,800,000 nchi nzima, watapata majimbo mangapi...?

Haya, vipi Tabora ambayo Ina eneo kubwa la ardhi lakini ikiwa population ndogo, unadhani instahili kuwa na majimbo mengi kama ilivyo sasa...?

Vipi Jimbo la Handeni vijijini lenye wapiga kura 24,000 tu? NEC walitumia kigezo kulifanya hili ni Jimbo sawa na Temeke lenye wapiga kura 470,000..??

Wakati mwingine mnapoamua kupinga hoja fulani, basi tumieni akili basi badala ya kutumia makalio...!!
 

Unadai Lussu ana hoja dhaifu halafu badala ya kuzijibu kwa hoja unaleta propaganda. Bure kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…