Pre GE2025 Tundu Lissu na hoja zake dhaifu dhidi ya Serikali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Unajua maana ya jimbo la uchaguzi? Kwani wilaya moja ikiwa na majimbo 20 ya uchaguzi kuna ubaya gani?
 
Hapa jambo la msingi ni kuelewa kazi za bunge na mbunge kwa ujumla,,,na zana nzima ya uwakilishi,,,kwa sababu wanaowakilishwa ni watu na sio ukubwa au udogo wa eneo
Hoja ya kuwa na wabunge wengi kwa kuwa eneo ni kubwa ila watu ni wachache ni kuongeza matumizi ya fedha za walipa kodi bila msingi wowote.
Hasa kwa bunge hili ambalo haliwezi kuisimamia serikali
 
Umeandika takataka
 
kama eneo la kiutawala ni kubwa kuna serikali za mitaa ndizo zinazohusika moja kwa moja na utoaji huduma na usimamizi wa rasilimali hivo kuongeza majimbo hakuwezi kuwa na tija yeyote kwa wananchi bali ni kuwapa watu ulaji tu,,,mfano wilaya ya Songea ina majimbo matatu na nahisi mnatamani mpate jimbo la nne,,,hivi hata yakiwa majimbo matano je ni tija ipi itapatikana ambayo kwa sasa tunaikosa kwa kuwa majimbo ni matatu na eneo ni kubwa kijiografia?
Hivi kwa bunge hili la sasa hata kama lisingekuwepo kuna madhara yeyote tungeyapata? kama chochote ambacho serikali (executive) inakipanga kinapita bila kupingwa hata kama kina mapungufu.
Kama eneo kubwa basi viongezwe vijiji peleka watendaji na watumishi wakahudumie wananchi mbunge hasa hawa wa sasa hakuna cha maana wanachoweza kusaidia zaidi kupiga makofi na kugawana posho.
 
Idadi hiyo ni impractical kwa mmbunge, kuweza kufahamu shida za kila eneo za wananchi kwenye mkoa.

Ni ngumu kuiweka serikali accountable na kuwasamea wananchi wote, shida za maeneo hazifanani kwenye mkoa.
 
Hivi hizi ni hoja dhaifu au wewe mleta hoja ndiye mdebwedo na dhaifu wa akili, uelewa na ufahamu wako...?
 
Hivi hiyo kura ya hapana wakala wake atakuwa nani ?Acheni ghiliba kwa kuweka sheria zinazolenga kukinufaisha chama cha mapinduzi huku vingine vikiwekewa mazingira magumu ya kushinda
 
Lissu angekuwa ana hoja kama angepinga kuongezwa majimbo mengine ya uchaguzi. Hoja ya kuongezeka kwa watu ni dhaifu mno. Hao watu hawawezi kuwakilishwa na mbunge mmoja kupeleka hoja zao bungeni? Kuongeza wabunge ni kujitwisha mzigo wa gharama zisizo na lazima.

Lissu ni sawa na wanasiasa wengine. Kwenye maslahi yao upinzani na CCM huungana na kuwa kitu kimoja. Hapo anacholilia ni tume kugawa majimbo kwa jinsi itakamvyonufaisha yeye na chama chake. Ameshasahau kuwa tunatakiwa tubane matumizi ili kuelekeza hela kwenye maendeleo. Kwa sababu ubunge una maslahi binafsi kwake hawezi pinga hilo.
 
Kwanza kwenye hoja unarudia kitu kiłę kiłę.

Pili nimeweka wazi ku-ignore upuuzi wa Zanzibar, mjini magharibi pekee inawabunge 19, hao ni zaidi ya wabunge wa mkoa mkubwa Tanzania bara (Tabora) yenye wabunge 12.

Hayo mengine takwimu żako sijui umezitoa wapi na hiyo kanuni yako ya idadi ya watu kwenye jimbo.

Kwa toleo la mwisho la uchaguzi jimbo lenye wapiga kura wachache ni Madaba, Ruvuma (65,000) na lenye wapiga kura wengi ni Geita (1035000). Kwengine ni vuruga machi from the lowest to the highest.

Hata mkiwekewa takwimu kwenye post mnaza quote hamsomi, tumezoea utaratibu wa kutoa vitu kichwani na kukejeli watu;Temeke inawapiga kura 1300,000 na majimbo mawili (Temeke na Mbagala).

Mengine unarudia point zile zile (on the same page), sasa sijui ulikuwa unabisha nini.
 
Hizo siyo hoja Dhaifu sema wewe binafsi unasaka uteuzi umeamua kujitoa fahamu kwa mambo muhimu ya msingi kuyaita hoja Dhaifu, wewe ndiyo mwenye hoja Dhaifu siyo Lisu kwani kero za Tume ya uchaguzi hazipaswi kufumbiwa macho kamwe
 
Kitu kibaya kama hakiondoki ama kuondolewa lazima warudie kusema hata mara 1000 hadi siku maovu yote yanamalizwa
 
Hakuna mwenye akili tumamu na mtanganyika atashiriki uchaguzi wa October. Ni ujinga na kupotezeana muda.

LIssu yupo sahihi 100%
Safari hii wabunge wa com watakosa wapiga kura watu hawatajitokeza kupiga kura mpaka Tume huru ya uchaguzi iundwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…