Tundu Lissu na kuruka vihunzi

Tundu Lissu na kuruka vihunzi

Superbug

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
13,864
Reaction score
35,079
Maisha ya Tundu Lissu yamejaa majaribu makubwa na vizingiti vingi anavyowekewa na wasiomtakia mema ikiwepo system.

Mfano,

Walidhani watamshinda kwa hoja bungeni ikashindikana.

Walidhani watamshinda mahakamani kwa makesi ikashindikana.

Wakaona wamuuwe Mungu akakataa ikashindikana.

Wakasema hatarudi nchini amerudi.

Wakasema atakamatwa akitua airport hajakamatwa.

Wakasema hatachaguliwa na chama chake akachaguliwa.

Wakasema hatapewa fomu kwavile Ana kesi mahakamani kapewa fomu.

Na Sasa wanasema hatashinda tumuachie mungu muda utaamua.

Kiufupi maisha ya tundu lisu yanatupa somo kubwa Sana kwenye maisha.
 
Jamaa utani utani mara kweli anachukua nchi.Huyu jamaa kunusurika kote huko nadhani kuna mpango ambao Mungu amemuandalia.watu wenye uwezo wa kutambua mambo ktk spiritual world.scenario kama hizi huwa zina jambo kubwa nyuma yake. Keep ur eyes open.
 
Ubaya haujawahi ushinda wema, na Wala giza halijawahi ushinda mwanga.

Walipigana kumzuia lakini hawakuelewa kuwa mipango ya Mungu hupangwa na Mungu mwenyewe na sio system.
 
Hapa ndio patamu, trend ya matukio inaonyesha hajawahi kushindwa! Muroto ajiandae kisaikolojia
Kesi zote alizosimamia mahakamani alishinda? Miga tumeshitakiwa ... Its not fair kujifanya unayajua maisha ya mtu mpaka ya ndani....
 
Jamaa utani utani mara kweli anachukua nchi.Huyu jamaa kunusurika kote huko nadhani kuna mpango ambao Mungu amemuandalia.
Mungu wala hana mpango na mgombea yeyote amewapa uhuru nyinyi wenyewe muamue ni yupi kati yao atawafaa ili kuepusha mambo ya kumlilialilia bdae, na asitokee mgombea yeyote aseme cjui katumwa na Mungu kuja kuwakomboa watz mara ooh chaguo la Mungu never been, Mungu hanaga hizo shobo.
 
Kesi zote alizosimamia mahakamani alishinda? Miga tumeshitakiwa ... Its not fair kujifanya unayajua maisha ya mtu mpaka ya ndani....

..Acacia walikwenda mahakamani/ "miga."

..na ili waondoe kesi ilibidi serikali isalimu amri na iachane na madai ya usd 191 billion na kukubali kishika uchumba cha usd 300 million.

..hukusikia kwamba Prof.Kabudi alitaka kubwaga manyanga? Ni kwasababu alishindwa kutetea kilichokuwepo kwenye ripoti za Mruma, na Ossoro.

..tatizo la ccm ni kutokusikiliza upande wa upinzani hata wanapotoa ushauri mzuri. tangu mwanzo wapinzani walisema mikataba ile ni mibaya. sasa njia nzuri ilikuwa kusaini mikataba michache huku tukiusoma mchezo, lakini ccm wakaenda wakasaini bulyankulu, nzega, geita, buzwagi, north mara, nadhani jumla iko zaidi ya saba. Nzega nadhani umeshafungwa. Bulyankulu na Buzwagi nayo nimesikia iko ktk hatua za mwisho.

..na kosa mnalofanya vijana wa ccm ni kuwateremshia lawama za wizi wa madini cdm, badala ya ku-deal na wazee wenu waliomo ndani ya chama chenu ambao walipitisha sheria zetu na kusaini mikataba mibovu.

..haiingii akilini umlaumu TL kuliko Mkapa, Kikwete, na wana-ccm wengine waliokuwa wapambe na watetezi wakubwa wa sheria na mikataba mibovu.
 
Wanao bisha kuwa Tundu Lissu ni mpango wa Mungu safari hii watathibitisha hilo.
Mungu ni mkuu,na hadhihakiwi!
 
Mungu wala hana mpango na mgombea yeyote amewapa uhuru nyinyi wenyewe muamue ni yupi kati yao atawafaa ili kuepusha mambo ya kumlilialilia bdae, na asitokee mgombea yeyote aseme cjui katumwa na Mungu kuja kuwakomboa watz mara ooh chaguo la Mungu never been, Mungu hanaga hizo shobo.
If God decided to bless you,he does not ask permission to anybody.
 
1596889784781.png
 
Maisha ya Tundu Lissu yamejaa majaribu makubwa na vizingiti vingi anavyowekewa na wasiomtakia mema ikiwepo system.

Mfano,

Walidhani watamshinda kwa hoja bungeni ikashindikana.

Walidhani watamshinda mahakamani kwa makesi ikashindikana.

Wakaona wamuuwe Mungu akakataa ikashindikana.

Wakasema hatarudi nchini amerudi.

Wakasema atakamatwa akitua airport hajakamatwa.

Wakasema hatachaguliwa na chama chake akachaguliwa.

Wakasema hatapewa fomu kwavile Ana kesi mahakamani kapewa fomu.

Na Sasa wanasema hatashinda tumuachie mungu muda utaamua.

Kiufupi maisha ya tundu lisu yanatupa somo kubwa Sana kwenye maisha.
Umesahau moja mkuu, wakasema kuwa wamnyime airtime kwenye vyombo vyao vya habari uchwara ( ITV, Azam Tv , TBC, Clouds Tv, Star Tv, Channel Ten na Eatv)na kumzimia sauti akiongea ila wapi nayo imeshindikana watu wanarekodi kwa simu na kamera zao na wanarusha tu speech zake na raia tunaziona
 
Mungu wala hana mpango na mgombea yeyote amewapa uhuru nyinyi wenyewe muamue ni yupi kati yao atawafaa ili kuepusha mambo ya kumlilialilia bdae, na asitokee mgombea yeyote aseme cjui katumwa na Mungu kuja kuwakomboa watz mara ooh chaguo la Mungu never been, Mungu hanaga hizo shobo.

Mkuu unaamini sawa na mimi. Nikisikiaga mtu anasema Mungu ndio atampa mtu mke au mume, roho inaniuma sana. Nimegundua kuna watu wengi hawatumii utashi walopewa na Mungu. Badala ya kuhalalisha au hukosoa matokeo kwa kumhusisha Mungu!!
 
Watahangaika sana kuzuia mipango ya Mungu,mwisho wa siku itakuwa Kama Mungu alivyoona a
 
Back
Top Bottom