Na Mwal. Maziku, Singida
Makamanda salaam!
Waswahili wanasema ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni. Kitendo cha kiongozi wa CHADEMA Ndugu Lissu kutanguliza maombi binafsi kwa Rais ni usaliti mkubwa usio kubarika. Kwa hakika mtu huyu hakustahili kupewa majukumu ya umakamu Mwenyekiti kwani ameonyesha dhamira yake si njema, baadhi ya maombi ni pamoja na ;
1. KUOMBA KULIPWA MISHAHARA YA KIBUNGE, POSHO, NA MALUPULUPU YOTE- Kwa akili ya kawaida huwezi kupinga mtu kudai maslahi yake lakin hoja yangu ni kwanini aweke jambo hili kama kipaumbele akijua fika mahitaji ya chama? Unakumbuka msimamo wetu juu ya posho?
2. ATAFUTIWE PASSPORT YA KUSAFIRIA BAADA YA KUPOTEZA YA AWALI- Kiongozi wa chama cha Upinzani unakutana na Rais unaanza na hoja ya pasi ya kusafiria ? tena uliyoipoteza kwa uzembe ? Yani tabia za kina John Mrema kwenda kulewa pale Triple Seven ndio unaanza kuzionyesha wazi wazi? Ulipoteza vipi ile ya awali?
3. APATIWE ULINZI BINAFSI NA WASAIDIZI WA KUTEMBEA NAO- Hivi kaka Tundu Lissu umekuaje wewe? Umepata fursa ya kipekee kuzungumza na Rais unaweka hili kama kipaumbele? Hili lilipaswa kuwa nje ya majadiliano kaka, aisee aibu naona mimi. Tumbo Tumbo Tumbo!
4. WABUNGE 19 - VITI MAALUM WAONDOLEWE BILA KUFUATA KANUNI- Hili liko wazi wabunge waondelewe baada ya Baraza kuu kukutana na sio kufanya uhuni kutokana na wivu dhidi ya Halima na wenzie. Kaka Lissu wewe hujui kwanini mpaka sasa baraza halijakaa? Umetuangusha sana TL sheria haiko hivyo!
Kama Chama Cha Demokrasia na Maendeleo tusipopata viongozi wazuri huyu Lissu na wenzie wanaojijali wao tu na matumbo yao wataua chama hiki. Sasa nimeelewa kwanini Kamanda Mbowe hataki kumpa mtu mwingine kiti, wengi wabinafsi na Tundu Lissu ni mmoja wao.
LISSU AELEZA MAMBO SABA (7) ALIYOZUNGUMZA NA RAIS SAMIA
1. Ajenda ilikuwa "hali ya siasa ya nchi yetu." mazungumzo yamechukua takribasi saa moja, na mojawapo ya mambo niliyozungumza nae ni juu ya mwenendo wa kesi ya Mbowe
2. Ajenda ya pili ni suala na la vyama vya upinzani kufanya shughuli za kisiasa kwa mujibu wa sheria.
3. Jambo la tatu ni suala la #KatibaMpya na nimemwambia Mh. Rais ana nafasi ya kuhakikisha tunapata #KatibaMpya na anatengeneza mfumo wa kidemokrasia.
4. Ajenda ya nne, ni inayonihusi mimi na wenzangu tuliolazimika kuikimbia nchi yetu sababu ya vitisho. Nimemwambia Rais kwa mamlaka yake, nina haki ya kupatiwa matibabu kwa mujibu wa sheria, na mazingira yanayohusu kuondolewa kwangu @TunduALissu bungeni na kutokulipwa mafao yangu.
5. Nimemwambia Mh. Rais kuwa mimi @TunduALissu ninahitaji kurudi nyumbani, na ninahitaji atoe kauli ya kunikaribisha nyumbani na nitakuwa salama, nimehakikishiwa nitapata hati ya kusafiria, kwa kuwa yangu iliibiwa Ujerumi. Nimewaongelea pia wenzangu @WenjeEzekiah na @godbless_lema
6. Nimemweleza mh. Rais sisi @ChademaTz hatuna wabunge Bungeni kwa kuwa wale wabunge tumewafukuza uanachama. Nimemwomba Mh. Alishughulikie hilo.
7. Ajenda ya mwisho nimemwomba Mh. Rais atuongoze katika kuliponya Taifa kutokana na majeraha tuliyonayo, kwa kutekeleza ahadi yake ya kukutana na viongozi wa vyama vya upinzani.