Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
“Naenda Mahakamani kufungua kesi kwanza ya kuvunjiwa mkutano wetu bila sababu, pili Viongozi na Wanachama wetu kupigwa bila sababu, tatu kukamatwa bila sababu, nne kufungwa bila sababu, tano uharibifu wa mali na mengine ambayo Wanasheria watapendekeza”
“Na tumesema tunamshtaki Shosti Nyahoza kama Shosti Nyahoza na tunamshtaki kamishna wa Polisi Awadhi Haji kama Awadhi Haji, hatutaki Mawakili wa Serikali waje waingilie tunataka tushungulike na hawa watuambia matendo yao yalikuwa halali namna gani na kama hayakuwa halali watuambie nani aliyewatuma” —— Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara Tundu Lissu akiongea mbele ya Waandishi wa Habari DSM leo August 14,2024.
PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - CHADEMA: Tutafungua kesi dhidi ya Sisty Nyahoza na Awadh Haji juu ya kukamatwa na kupigwa kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA