Tundu Lissu, mwanasheria machachari ambaye amekuwa anaichachafya CCM kuhusu mikataba mibovu ya madini, ameshinda katika jimbo lake ila NEC inashindwa kumtangaza kwa sababu mpinzani wake anataka masanduku yafunguliwe kura zihesabiwe tena. Lissu anagoma kwani anasema sheria ya uchaguzi inamlinda -- huwezi kuhesabu kura wakati masanduku yalilala usiku kusikojulikana. Anasisitiza matokeo ya vituoni yaliyokuwa yamehakikiwa na wakala wa vyama na kusainiwa ndiyo yatangazwe.
Lissu amebana humo humo katika chumba cha kuhesabia kura na kitabu chake cha sheria ya uchaguzi ambacho tayari kakifungua ukurasa husika na kuweka juu ya meza.
Inasemekana CCM inamuoigopa sana Lissu, haimtaki akaingia Bungeni. CCM inaona ni bora hata akina 'Slaa" watano warudi Bungeni kuliko Lissu mmoja.