Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tundu Lissu, mwanasheria machachari ambaye amekuwa anaichachafya CCM kuhusu mikataba mibovu ya madini, ameshinda katika jimbo lake ila NEC inashindwa kumtangaza kwa sababu mpinzani wake anataka masanduku yafunguliwe kura zihesabiwe tena. Lissu anagoma kwani anasema sheria ya uchaguzi inamlinda -- huwezi kuhesabu kura wakati masanduku yalilala usiku kusikojulikana. Anasisitiza matokeo ya vituoni yaliyokuwa yamehakikiwa na wakala wa vyama na kusainiwa ndiyo yatangazwe.
Lissu amebana humo humo katika chumba cha kuhesabia kura na kitabu chake cha sheria ya uchaguzi ambacho tayari kakifungua ukurasa husika na kuweka juu ya meza.
Inasemekana CCM inamuoigopa sana Lissu, haimtaki akaingia Bungeni. CCM inaona ni bora hata akina 'Slaa" watano warudi Bungeni kuliko Lissu mmoja.
Mtanzania la leo linasema TUNDULISU ameshinda.
Duu, kama ndivyo ilivyo au itakavyokua Tundulisu kushinda - Najipanga kusherehekea ushindi !!!
Mtanzania la leo linasema TUNDULISU ameshinda.
Na mimi nina hamu ya kujua huyu mpiganaji kafikia wapiKabila na Njowepo, hamnnishindi mimi...!! Nina hamu ya kupata confirmation kuwa kashinda, nimeshapata tetesi za ushindi wa mpiganaji huyu...!!
Poa poa Mumbo sasa mambo safi na kazi zinaenda. Patachimbika bungeni this timeStreema Radio Tuner, najua sasa mambo yataenda ofisni mzee,