Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi sikuwa nataka wapatane
Mimi sikuwa nataka wapatane
Mazungumzo kati yao waliogombana au kati ya wapatanishi?
Very honest advice mkuu tena kutoka kwa mkongwe unayeheshimika kama wewe! Binafsi nimekaa na kuzungumza na hawa wasanii inahuzunisha sana! Tena wasanii wakubwa ajabu! Nakubali huu ni ulimwengu wa mabepari lakini walau uwe ubepari wenye utu na kuheshimu kazi ya mwenzio na si kumtumia kwa maslahi binafsi then una mdamp kidhalilishaji!! Nafikiri tumeona akina mzee kipara kule upande wa filamu wakifa ktk dhiki ya ajabu pamoja na kuwajenga hawa vijana wa sasa! Lazima ujengwe mfumo utaompa sauti msanii kupitia hakimiliki na sheria zingine muhimu pia kutengeneza soko huru kwa wenye vipaji.kwa kuwakumbusha pia Ruge na Sugu si mara ya kwanza kupatana na tatizo mara nyingi anakuwa Ruge kutaka kuonesha hakukosea ili Sugu ampigie magoti kama alivyozoea! Brother Ruge badilika mahangaiko haya ya Dunia tusiyoijua kesho tujifunze kuwa roho safi! Yetu macho!My Take.
Kupatana ni jambo jema, hivyo sasa tutaziona nyimbo za Sugu na Vinega zikirindima Clouds japo msitegemee kuusikia Anti virus!.
Kupatana ni jambo moja, kutekekeza mapatano ni jingine, na kuyatibu makovu ya bifu lao pia ni jambo jingine kabisa.
Kwa maoni yangu, nawaona Jo na Ruge ni magentlemen na sio watu wa visasi hivyo lazima wakubali to strech their reconciliation hands a bit more ili kuwa accomodate the wounded ones ambao wana makovu ya udhalimu wao!.
Nawapongeza wote kwa uamuzi huu!.
Pia +watawalipa vizuri? Isiwe kuna dili wanataka kufanya tu.
King Kong,
Habari ni nzuri sana lakini heading yake hujhaitendea haki.
Hii habari ni nzuri sana kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya lakini pia na washabiki na wapenzi wa muziki kwa ujumla.
Napenda nitumie fursa hii kuwapongeza Mh. Sugu na Bw. Ruge bila kuwasahau Mh. Nchimbi na Mh. Lissu kwa kufanikisha suluhu na muafaka huu, sasa kazi iwe ni moja tu kuendeleza udugu na ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.
Nimekumbuka ile methali isemayo, ndugu wapatanapo, chukua jembe ukalime, sasa hapa mjini itabidi tukalime lami!!:lol::lol: