Tundu Lissu, nenda mahakamani badala ya kulalamika huko Kenya

Mbona unateseka kuorodhesha miradi inayojengwa kwa fedha za umma! Sasa ulitaka fedha zisitumike? Samia hajatumia fedha zake!
 
Aende mahakama zipi
 
Kama una ushahidi kwamba ni wanafunzi waliosajiliwa kupiga kura kwanini huendi mahakamani?
Mahakama ya wapi unayo mshauri apeleke kesi. Hivi unayo akili timamu ya kutambua mambo wewe?
 
Tanzania tutaonekana wapuuzi wa hali ya juu kama tutamfanya mtu kama huyu kuwa Rais wetu.
Tanzania ipi hiyo unayo izungumzia. Siyo hii hii tuliyo nayo sasa hivi chini ya CCM?

Hivi wewe umeibukia wapi, mbona sijawahi kukuona humu JF na akili za kipumbavu kama unazo onyesha hapa?

Maadam nimekutambua, sijihangaishi tena kusoma takataka zako kama hao wengine waliojazana humu JF.
 
I like Tundu Lissu as a person.
But I dont like the way he does his politiks currently.
He needs to readjust, vijana wa mwaka 1995 alipokuwa anapambana na uhuni wa wakina Ben kwenye migodi ni tofauti na hawa vijana waimba singeli wa mwaka 2005 who might probably be first time voters.
 

Dah chama dola kongwe kimeshindwa kabisa kuwashawishi watu wazima walio na umri wa miaka 18 na zaidi, kiasi CCM kutumia kura wa watoto ambao si walipa kodi wala hawajatimiza yale masharti 9 ya kusajiliwa ktk daftari la mkaazi lakini CCM inavunja sheria za TAMISEMI kujaribu kupata ushindi haramu.





HABARI ZA ZIADA :

a mujibu wa Kifungu cha 16 (5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya siku ya uteuzi. Wanaohusika katika zoezi hili ni wananchi ambao: -

  1. Wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakuandikishwa hapo awali;
  2. Watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025;
  3. Waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo moja kwenda jingine;
  4. Waliopoteza sifa mfano wale waliofariki kuondolewa katika Daftari;
  5. Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji; na
  6. Waliopoteza au kadi zao kuharibika.
Watendaji wa Uandikishaji/ Uboreshaji

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi hutumia watendaji mbalimbali wakati wa Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Watendaji hawa ni pamoja na:-

  1. Waratibu wa Uchaguzi wa Mkoa;
  2. Maafisa Waandikishaji;
  3. Maafisa Waandikishaji Wasaidizi;
  4. Waandishi Wasaidizi; na
  5. Mwenyesha Kifaa cha Bayometriki
Mawakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura

Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Chama cha Siasa chenye usajili wa kudumu kinaweza kumteua mtu mmoja katika kila kituo cha uandikishaji kuwa Wakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura.

Wajibu/Majukumu ya Mawakala wa Uandikishaji

  1. Kufuatilia zoezi la uboreshaji na kutazama kama linazingatia Sheria, Kanuni na Maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
  2. Kushirikiana na Waandishi Wasaidizi kutambua wakazi wa eneo hilo na kutoa taarifa juu ya watu wasio na sifa.
Pamoja na majukumu tajwa, Mawakala wa Uboreshaji hawaruhusiwi kufanya yafuatayo:-

  1. Kuingilia shughuli za uendeshaji wa zoezi la Uboreshaji. Msimamizi wa kituo ndiye mwenye mamlaka ya mwisho juu ya nani anastahili kuandikishwa au kuboresha taarifa zake kwa mujibu wa Sheria.
  2. Kufanya kampeni za kisiasa katika kituo cha uandikishaji
  3. Kuorodhesha majina ya watu wanaojiandikisha.
Kiapo cha Kutunza Siri cha Mawakala wa Uandikishaji

Kila Wakala wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, ni lazima kula kiapo cha kutunza siri za taarifa za mwombaji au Mpiga Kura aliyeandikishwa. Wakala atakula kiapo mbele ya Afisa Mwandikishaji au Afisa Mwandikishaji Msaidizi. Hata hivyo, kutokuwepo kwa Wakala wa uandikishaji katika kituo cha kuandikisha Wapiga Kura hakuzuii utekelezaji wa majukumu ya Uandikishaji Wapiga Kura.

Watazamaji wa Uandikishaji

Kwa mujibu wa Kanuni za 46, 47, 48, 49, 50 na 51 (1) za Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2024 zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 Watazamaji wa ndani na kimataifa, wanaruhusiwa kutazama mchakato wa Uboreshaji utakavyofanyika katika vituo vya Uandikishaji.

Watazamaji wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutembelea vituo vya Uandikishaji, ni lazima waombe na kupatiwa idhini ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Watazamaji. Aidha, Watazamaji 24 watakaoruhusiwa na Tume watapewa barua za kuwatambulisha kwa Maafisa Waandikishaji na Mwongozo wa watazamaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioandaliwa na Tume. Maafisa Waandikishaji watatakiwa kuwapa barua za kuwatambulisha kwa Watendaji wa vituo ambavyo watavitembelea. Aidha, Watazamaji wa Uandikishaji wa Wapiga Kura hawapaswi kutoa maelekezo kwa Mwandishi Msaidizi katika kituo husika.

Kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura

Kwa mujibu wa Kifungu vya 11 (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, Tume inatakiwa kuweka wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura ili kutoa fursa kwa wananchi:

  1. Kulikagua Daftari;
  2. Kufanya marekebisho ya majina au mahali wanapoishi;
  3. Kuingiza au kufuta majina ya Wapiga Kura;
  4. Kuweka pingamizi kwa Mpiga Kura aliyeandikishwa na hana sifa za kuwemo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Kumuwekea Pingamizi aliyeandikishwa kwenye Daftari la Awali

Kifungu cha 27 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024,kinaruhusu Mkurugenzi wa Uchaguzi au Afisa Mwandikishaji au mtu yeyote aliyeandikishwa kuwa Mpiga Kura, kuweka pingamizi dhidi ya jina lililopo katika Daftari la Awali la Wapiga Kura. Kifungu cha 28 Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, kinaweka utaratibu wa kuweka pingamizi. Mtu aliyewekewa pingamizi hutakiwa kupelekewa taarifa ili aweze kutoa ufafanuzi ndani ya siku saba (7).

Kifungu cha 29 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 Mahakama itapaswa kutoa uamuzi wa rufaa hiyo ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kupokea rufaa hiyo, uamuzi wa Mahakama ya Wilaya na iwapo aliyewekewa pingamizi hakubaliani na 25 maamuzi ya Afisa Mwandikishaji ya kuendelea kukataliwa kuwemo katika Daftari, ana haki ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi Wilaya ndiyo utakuwa uamuzi wa mwisho na mtu hatoweza kukata rufaa katika Mahakama nyingine yoyote
Source: INEC Tanzania
 
Mahakama kuu utaambiwa hawawezi kuingilia watendaji wa uchaguzi.
 
Wapiga kura ndio wenye haki ya kuamua nani awaongoze, period. Sio hizi porojo za kikada wala nguvu ya polisi.

2016 Trump alichaguliwa kwa kura. Akaondolewa kwa kura 2020. 2024 amerudishwa tena madarakani kwa kura. Keep watching.

Wapiga kura ndio wanajua sifa zake zinazowafaa katika matarajio waliyo nayo hivi sasa. Na walipomuondoa walijua ubovu wake.

Bla bla na talalila nyingi hazina maana kabisa. Nchi iweke uchaguzi huru na wa haki, kura za wananchi zitaongea.
 
Kama hawatamsaidia ww inakuuma nn si umuache aongee kwakuwa ni uhuru wake, huko mahakamani nenda wewe ukamshitaki kama unaona anakosea
 
Una demokrasia gani wewe hata wakenya waitamani? Ya kuingia na kura kwenye sandarusi tena zimeshapigwa. Hembu kawadanganye kijijini kwenu huko
 
Wewe ni mgeni hapa Tanzania? Kwa mahakama zipi,hizi ambazo majaji na mahakimu wanapokea maelekezo toka kwa mhimili uliojichimbia zaidi? Au wewe unataka kum challenge tu Lissu ? Kesi ngapi zimefunguliwa kupinga Tamisemi kusimamia chaguzi za serikali za mitaa na nini kimejiri au unajitoa ufahamu tu?
 
Hawo hawafuati hay
Hawo hawafuati hayo kwasababu wanajua endapo watafanya na kufuata sheria hawawezi kushinda.
 
Kwani
Ni activists zaidi kuliko politician. Hana uwezo wa kuconvice mtu aelekee upande wake. Ni rahisi sana kujitengenezea maadui kuliko marafiki. Anaituhumu tigopesa hadharani bila kuwa na ushahidi usioacha mashaka. Hana tofauti na lay person.
 
Wacha utoto nyashu, kwani nchi nyingine Marais wao hawakusanyi Kodi?
 
Kwani

Ni activists zaidi kuliko politician. Hana uwezo wa kuconvice mtu aelekee upande wake. Ni rahisi sana kujitengenezea maadui kuliko marafiki. Anaituhumu tigopesa hadharani bila kuwa na ushahidi usioacha mashaka. Hana tofauti na lay person.
Nadhani Activism ndiyo inayomtofautisha na Freeman Mbowe na kumuweka zaidi kama mtu mwenye mihemko japo si kwamba anahemka kwa ubaya. Inawezekana 90% ana malengo mazuri ila hana approach sahihi.
 
Alishaenda mahakama ubelgiji tayari kenya alikuwa airport tu waandishi wakamvaa kiufupi lazima ndege ikamatwe kama hatalipwa?!!
 
Kwani

Ni activists zaidi kuliko politician. Hana uwezo wa kuconvice mtu aelekee upande wake. Ni rahisi sana kujitengenezea maadui kuliko marafiki. Anaituhumu tigopesa hadharani bila kuwa na ushahidi usioacha mashaka. Hana tofauti na lay person.
Kwamba ukiwa activist ndio huwezi kushawishi, unajua unachoongea au ni hilo tatizo la kuwa bendera fuata upepo linakusumbua?

Ushahidi wa Tigo Pesa kufanya uhalifu ulianza kutolewa na boss mzungu aliyekuwa akifanya kazi humo. Sasa hata sielewi unaongea utoto gani. Nilijua tu una akili ya kitoto ndio maana hata huu uzi wako umejaa hoja nyingi za kitoto.
 
Nadhani Activism ndiyo inayomtofautisha na Freeman Mbowe na kumuweka zaidi kama mtu mwenye mihemko japo si kwamba anahemka kwa ubaya. Inawezekana 90% ana malengo mazuri ila hana approach sahihi.
Eti tundu lisu ameshindwa kutaja japo zuri hata Moja alilofanya mama Samia kwenye nchi hii. Anapuuzwa na Kila mtu ndani na nje ya nchi. Royal tour imechechemua utalii lakini Lisu haoni kitu, ni kichaa. Sijui chadema wanawezaje kuishi nae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…