Tundu Lissu nenda taratibu, tumia hekima na busara kumaliza tofauti zako na Freeman Mbowe. Vinginevyo mnaiua CHADEMA

Mimi The Palm Beach si mwanachama wa CHADEMA ila ni mpenzi na mfuasi wake na nakiunga mkono kwelikweli chama hiki...

Ni wazi kuwa Kuna mgogoro mkubwa kati ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti wake Tundu Lissu ndani ya CHADEMA

Nitasikitika na kuumia sana kama chama hiki cha siasa kilicho tegemeo pekee la Watanganyika nacho kitafuata njia ya CUF, TLP na NCCR - MAGEUZI kujidhoofisha na kisha kwenda kujifia zake huko.

Na naona wazi kabisa, kazi hii ya kukisambaratisha chama hiki inafanywa na viongozi wenyewe kwa kujua au kutojua.

Mpaka hatua hii, haina shaka kuwa iko shida ndani ya CHADEMA hususani kwa viongozi wakuu wa chama. Ili kukiokoa chama hiki na kuhifadhi moto wake uliowashwa kwa miaka takribani 30 sasa usizimike ni lazima ifanyike intervention ya haraka kuzuia hali hii isifikie point of no return.

Press Conference ya Tundu Lissu huko Singida leo imethibitisha shaka yangu hii.

Kila alichoki - address kule Singida mbele ya waandishi wa habari kuhusu uchaguzi wa serikali za vijiji na mitaa hakina shida, ni kizuri na ni kweli hali ndivyo ilivyo

Lakini mwishoni alipoulizwa swali na waandishi wa habari kama hiyo ni kauli ya chama ama la na yeye kujibu kuwa, kila alichokisema hapo ni cha yeye Tundu Lissu na sio kauli ya chama na kwamba baadaye ndio atapeleka hoja hizo ndani ya chama na kushinikiza ziwe ni kauli rasmi ya chama, nikawa shocked kidogo na kuliona tatizo hili ninalolisema hapa kwa uwazi kabisa...

Hii ya Singida ni mwendelezo wa tukio na kauli nyingine aliyoitoa kule Same - Kilimanjaro. Hii ya Same ilimshambulia Mwenyekiti wake Freeman Mbowe moja kwa moja bila kificho....

Kauli ya Tundu Lissu kule Same - Kilimanjaro aliitoa baada ya kusambaa kwa tuhuma kuwa, ule mkutano uliokuwa uhututubiwe na yeye huko Same, eti ulizuiliwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kwa kushirikiana na CCM kwa kutumia Polisi...

Ieleweke kuwa hoja hapa si kuzuiliwa kwa mkutano huo iwe ni kwa sababu hiy kweli au nyingine....

Tatizo ni namna Tundu Lissu alivyoshughulikia tuhuma hizo zilizomuhusisha Mwenyekiti wake...

Kauli yake kule Same Kilimanjaro ilikuwa hii, nanukuu;

"........Kama ni kweli, basi nyie ndiyo wenye chama, ndio wanachama wa chama hiki. mnapaswa kujiuliza Je, kila anayevaa makombati haya ni mwenzetu kwa kiasi gani kama anaweza kushirikiana na wabaya wetu kutuhujumu. Ila kama tuhuma hizi sio za kweli, basi mtanisamehe.."

Hii statement ni tata sana. Ni kama vile Makamu Mwenyekiti alishajiridhisha kuwa ni kweli Mwenyekiti wake ametenda hivyo na akaisema indirectly ili kupeleka ujumbe mahususi kwake...

Kwa kawaida, mimi nilifikiri kuwa, kabla ya kusema lolote, basi Makamu Mwenyekiti alipaswa kutumia hekima kidogo ya kuwasiliana na Mwenyekiti wake na kupata kauli yake juu ya tuhuma hizo zilizoelekezwa kwake. Na majibu ya Mwenyekiti ndiyo yalipaswa kuwa mwongozo wake kujibu hoja hiyo hadharani mbele ya umma...

Lakini kwa kauli yake hii, moja kwa moja inaonesha kuwa hakuwa amewasiliana na Mwenyekiti wake.

Na kama ni hivyo, napata shaka kuelewa kama hata Mwenyekiti na ofisi kuu ya chama (katibu mkuu na mtendaji mkuu wa chama) kama walikuwa wanajua kuwa Makamu Mwenyekiti wao atakuwa ziarani Same - Kilimanjaro siku hizo.

USHAURI:

CHADEMA kaeni chini, malizeni tofauti zenu amicably. Na kama kuna mambo yanayokwanza wengine, basi yashughulikiwe haraka ndani ya chama kwa taratibu za wazi za kichama....

Kuonesha tofauti zenu waziwazi huku nje ni hatari sana na wapinzani wenu wakuu CCM watatumia mwanya na udhaifu huu kuwamaliza kabisa na kusambaratika Moja kwa moja...

Hiki (Anguko la CHADEMA) ndicho CCM wanachokisubiri kukiona kikitokea Ili waweze kupumua....

Na hili la kuisambaratisha CHADEMA likitokea mikononi mwenu wewe Freeman Mbowe, Tundu Lissu, John Mnyika na Kamati kuu kwa ujumla fahamuni leo kuwa, mtalipa gharama kubwa sana Ili Watanganyika wawasamehe...!!!

CC: Erythrocyte
Chadema ife mara ngapi? By the way Watanzania ni kama wamegoma kuisapoti imebakia wanaharakati tuu.

Kina Heche wako wapi? 😂😂 Tangu lini watu dizaini ya kina Lisu wakawa na hekima? Umewahi ona wapi?

Kila mtu apambane kivyake.
 
..Lissu akomae humo humo.

..huyu bwana akisafiri, au akipumzika kidogo tu, Ccm wanajisahau kabisa.

..hata Samia alikuwa haonekani maana Lissu alikuwa hayupo nchini.

..hata haya mazonge ya kuenguana bila Lissu kuyapigia kelele, Ccm wangetia pamba kwenye masikio, na kuendelea na hujuma zao.
Lissu huyu anayeunga mkono ushoga?
 
Acha kife ili tupate chama kipya na imara zaidi….
Mara nyingi kujenga nyumba mpya ni aghali ukilinganisha na kuziba kiraka.
Chama kipya muda haupo kabla ya uchaguzi huu wa serikali za mitaa hata uchaguzu mkuu mwakani.
Kwa saaa inatakiwa busara na mageuzi ya mawasiliano ndani ya chama.
Lissu hagombei pesa,wala Mbowe hagombei wafuasi.
 
Itakuwa ni simanzi na majonzi kuwa hekima inakosekana ndani ya Chama kikuu Cha upinzani hadi kipasuke vipande 2. Kuna kitu kimoja tu nacho ni Chadema kukaa na kumaliza tofauti hizi kwa Kila mwenye hofu kusema wazi wazi. Matumizi ya kuongea mitandaoni ni utovu wa nidhamu.
Fikirieni kwa miaka kadhaa Watanganyika walivyojitoa kwa ajili ya Chama na viongozi wake. Watu wamepotezwa, kuuliwa, kupewa vilema na wengine kufungwa. Kukuza mgogoro ni kutoitendea haki demokrasia na wanachama wa Chadema.
 
Tatizo la Chadema ni Mbowe,

Shida yenu tukianza kumsema humu kinazuka kile kikundi chake cha kikabila kumtetea...

Mbowe ni pro maslahi sana, hua namshauri Lissu atengeneze Chama kipya...

Najua kitachukua mda mrefu, lakini by 2030 kitakua tishio na tunaweza kuchukua nchi...

Kuendelea kuing'ang'ania Chadema, kuna siku watamshinda nguvu na kumzushia propaganda itakayochukua mda kuisafisha.
 
Uko sahihi sana. Nilishashauri huko nnyuma kuwa CHADEMA iwe na kikundi maalumu cha intelectuals kuwashauri masuala mbalimbali. Hicho kikundi kisitokane na viongozi wakuu wa chama wa wakati huo. Kuna kipindi kulikuwa na watu wanaitwa " WAZEE WA CHAMA" sina uhakika kama wapo na ni hai kwa kiasi gani. Hao Wazee walishawahi kufanya kazi nzuri sana kipindi cha urais wa Dr. Kikwete.
Chama lazima kifanye mambo yake ya kuhakikisha kinatamalaki all the way,all the time.
Sio kila anaejiunga na Chadema anakitakia mema Chadema.
Kuiga siyo shida weka wajumbe 7 wa kudumu ndio wenye chama wa kuhakikisha chama hakiyumbi, kura zao ndio muelekeo au maamuzi ya chama.
Chama hakiongozwi kwa mihemuko au hotuba nzuri za kuwaburudisha wanachama na wapenzi tu,kuna zaidi ya hayo.
 
Hakika.
 
Tatizo la Chadema ni Mbowe,

Shida yenu tukianza kumsema humu kinazuka kile kikundi chake cha kikabila kumtetea...

Mbowe ni pro maslahi sana, hua namshauri Lissu atengeneze Chama kipya...

Najua kitachukua mda mrefu, lakini by 2030 kitakua tishio na tunaweza kuchukua nchi...

Kuendelea kuing'ang'ania Chadema, kuna siku watamshinda nguvu na kumzushia propaganda itakayochukua mda kuisafisha.
Chadema ilishapoteza focus siku nyingi sana

Kimekua kikundi cha harakati na matukio
 
Chama lazima kifanye mambo yake ya kuhakikisha kinatamalaki all the way,all the time.
Sio kila anaejiunga na Chadema anakitakia mema Chadema.
Kuiga siyo shida weka wajumbe 7 wa kudumu ndio wenye chama wa kuhakikisha chama hakiyumbi, kura zao ndio muelekeo au maamuzi ya chama.
Chama hakiongozwi kwa mihemuko au hotuba nzuri za kuwaburudisha wanachama na wapenzi tu,kuna zaidi ya hayo.
Ndio demokrasia hii?
 
Tatizo la Chadema ni Mbowe,

Shida yenu tukianza kumsema humu kinazuka kile kikundi chake cha kikabila kumtetea...

Mbowe ni pro maslahi sana, hua namshauri Lissu atengeneze Chama kipya...

Najua kitachukua mda mrefu, lakini by 2030 kitakua tishio na tunaweza kuchukua nchi...

Kuendelea kuing'ang'ania Chadema, kuna siku watamshinda nguvu na kumzushia propaganda itakayochukua mda kuisafisha.
Ushauri wako ni wa baadae sana endapo mikakati mingine itashindwa. Shida ya Chadema ni viongozi kuwa na mitizamo tofauti bila kuwa na chombo cha kuiunganisha hiyo mitizamo na kutengeneza mtizamo mmoja wenye nguvu. Ndiyo maana Lissu, Mbowe, Mnyika wa sasa wanaonekana ni tofauti sana na wale tuliowajua enzi zile. Walikuwa na kitu kama sijakosea kinaitwa Baraza la Wazee wa Chama. Sina uhakika kama wapo na wana nguvu gani sasa kukishauri na kusimamia mwenendo wa chama.
 
Kuwa na mitazamo tofauti siyo kosa kwenye chama cha siasa. Siyo kikundi cha kwaya kile kwamba kila mtu lazima acheze sawa na mwenzie
 
Lisu akomae hapo hapo, jamaa wanamzunguka hao
1. Tuwe tu wakweli chadema ya sasa pumzi ameishikilia Lissu
2. Mwenyekiti wetu umaarufu wake hata mvuto umepungua
3. Ninaamini Mwenyekiti wetu anaifaidi chadema kuliko chadema inavyonufaika
4. Mbowe ingefaa aachiwe na wengine yeye abaki kuwa mshauri tu.
5. Je miaka yote Mbowe hajaweza kuandaa mrithi?
 
1. Tuwe tu wakweli chadema ya sasa pumzi ameishikilia Lissu
2. Mwenyekiti wetu umaarufu wake hata mvuto umepungua
3. Ninaamini Mwenyekiti wetu anaifaidi chadema kuliko chadema inavyonufaika
4. Mbowe ingefaa aachiwe na wengine yeye abaki kuwa mshauri tu.
5. Je miaka yote Mbowe hajaweza kuandaa mrithi?
Tatizo la Chadema ni Mbowe,

Shida yenu tukianza kumsema humu kinazuka kile kikundi chake cha kikabila kumtetea...

Mbowe ni pro maslahi sana, hua namshauri Lissu atengeneze Chama kipya...

Najua kitachukua mda mrefu, lakini by 2030 kitakua tishio na tunaweza kuchukua nchi...

Kuendelea kuing'ang'ania Chadema, kuna siku watamshinda nguvu na kumzushia propaganda itakayochukua mda kuisafisha.
Lissu iko siku atakujuta muda aliotumia kutumimikia chama ambacho kipo kwa ajili ya mbowe na kikundi chake toka Kaskazini.
 
Mimi The Palm Beach si mwanachama wa CHADEMA ila ni mpenzi na mfuasi wake na nakiunga mkono kwelikweli chama hiki...

Ni wazi kuwa Kuna mgogoro mkubwa kati ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti wake Tundu Lissu ndani ya CHADEMA

Nitasikitika na kuumia sana kama chama hiki cha siasa kilicho tegemeo pekee la Watanganyika nacho kitafuata njia ya CUF, TLP na NCCR - MAGEUZI kujidhoofisha na kisha kwenda kujifia zake huko.

Na naona wazi kabisa, kazi hii ya kukisambaratisha chama hiki inafanywa na viongozi wenyewe kwa kujua au kutojua.

Mpaka hatua hii, haina shaka kuwa iko shida ndani ya CHADEMA hususani kwa viongozi wakuu wa chama. Ili kukiokoa chama hiki na kuhifadhi moto wake uliowashwa kwa miaka takribani 30 sasa usizimike ni lazima ifanyike intervention ya haraka kuzuia hali hii isifikie point of no return.

Press Conference ya Tundu Lissu huko Singida leo imethibitisha shaka yangu hii.

Kila alichoki - address kule Singida mbele ya waandishi wa habari kuhusu uchaguzi wa serikali za vijiji na mitaa hakina shida, ni kizuri na ni kweli hali ndivyo ilivyo

Lakini mwishoni alipoulizwa swali na waandishi wa habari kama hiyo ni kauli ya chama ama la na yeye kujibu kuwa, kila alichokisema hapo ni cha yeye Tundu Lissu na sio kauli ya chama na kwamba baadaye ndio atapeleka hoja hizo ndani ya chama na kushinikiza ziwe ni kauli rasmi ya chama, nikawa shocked kidogo na kuliona tatizo hili ninalolisema hapa kwa uwazi kabisa...

Hii ya Singida ni mwendelezo wa tukio na kauli nyingine aliyoitoa kule Same - Kilimanjaro. Hii ya Same ilimshambulia Mwenyekiti wake Freeman Mbowe moja kwa moja bila kificho....

Kauli ya Tundu Lissu kule Same - Kilimanjaro aliitoa baada ya kusambaa kwa tuhuma kuwa, ule mkutano uliokuwa uhututubiwe na yeye huko Same, eti ulizuiliwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kwa kushirikiana na CCM kwa kutumia Polisi...

Ieleweke kuwa hoja hapa si kuzuiliwa kwa mkutano huo iwe ni kwa sababu hiy kweli au nyingine....

Tatizo ni namna Tundu Lissu alivyoshughulikia tuhuma hizo zilizomuhusisha Mwenyekiti wake...

Kauli yake kule Same Kilimanjaro ilikuwa hii, nanukuu;

"........Kama ni kweli, basi nyie ndiyo wenye chama, ndio wanachama wa chama hiki. mnapaswa kujiuliza Je, kila anayevaa makombati haya ni mwenzetu kwa kiasi gani kama anaweza kushirikiana na wabaya wetu kutuhujumu. Ila kama tuhuma hizi sio za kweli, basi mtanisamehe.."

Hii statement ni tata sana. Ni kama vile Makamu Mwenyekiti alishajiridhisha kuwa ni kweli Mwenyekiti wake ametenda hivyo na akaisema indirectly ili kupeleka ujumbe mahususi kwake...

Kwa kawaida, mimi nilifikiri kuwa, kabla ya kusema lolote, basi Makamu Mwenyekiti alipaswa kutumia hekima kidogo ya kuwasiliana na Mwenyekiti wake na kupata kauli yake juu ya tuhuma hizo zilizoelekezwa kwake. Na majibu ya Mwenyekiti ndiyo yalipaswa kuwa mwongozo wake kujibu hoja hiyo hadharani mbele ya umma...

Lakini kwa kauli yake hii, moja kwa moja inaonesha kuwa hakuwa amewasiliana na Mwenyekiti wake.

Na kama ni hivyo, napata shaka kuelewa kama hata Mwenyekiti na ofisi kuu ya chama (katibu mkuu na mtendaji mkuu wa chama) kama walikuwa wanajua kuwa Makamu Mwenyekiti wao atakuwa ziarani Same - Kilimanjaro siku hizo.

USHAURI:

CHADEMA kaeni chini, malizeni tofauti zenu amicably. Na kama kuna mambo yanayokwanza wengine, basi yashughulikiwe haraka ndani ya chama kwa taratibu za wazi za kichama....

Kuonesha tofauti zenu waziwazi huku nje ni hatari sana na wapinzani wenu wakuu CCM watatumia mwanya na udhaifu huu kuwamaliza kabisa na kusambaratika Moja kwa moja...

Hiki (Anguko la CHADEMA) ndicho CCM wanachokisubiri kukiona kikitokea Ili waweze kupumua....

Na hili la kuisambaratisha CHADEMA likitokea mikononi mwenu wewe Freeman Mbowe, Tundu Lissu, John Mnyika na Kamati kuu kwa ujumla fahamuni leo kuwa, mtalipa gharama kubwa sana Ili Watanganyika wawasamehe...!!!

CC: Erythrocyte

View: https://x.com/LuhagaMpina/status/1856317859023958089?t=PWWX9l0lXdsqQitve7GHsA&s=19
 
Kwani ni lini tundu lissu aliwahi kuwa na hekima!
 
Sijui.

Sijapata nafasi kumuuliza...

After all Mimi ni mwananchi, mpenzi na mfuasi tu wa CHADEMA niliye nje kabisa huku kijijini kwetu Shinyanga...

Simjui Mbowe wala Tundu Lissu zaidi wa kuwaona kwenye TV na picha tu. Wala wao hawanijui mimi.....

Labda Erythrocyte aseme Neno hapa
Tundu Lissu atimuliwe CHADEMA haraka
 
Umenena vema Mkuu
CDM wanayumba kutokana na mambo kadhaa:

CDM wameshindwa kuhimili kishindo cha chnagmoto za Ukubwa wa Taasisi.
Taasisi inapokuwa kubwa sana huwa ni desturi kwa migongano na changamoto kubwa kuibuka kwa kasi. Njia ya kuhimili hili ni kujenga na kufanya maamuzi kwa kuzingatia kanunu, sheria na vikao halali. dosari hii imesababisha washindwe kutofautisha kati ya adui wa kiongozi na adui wa chama. Wamewapoteza makamanda wao muhimu ambao waliwalea na kuwakuza kwa jasho na damu kwa sababu nyepesi nyepesi tu. Yaani una Messi, Iniesta na Xavi alafu mwenyekiti wa club unwapoteza kirahisi tu bila kujari hatma ya club yako. Ukiwa club kubwa lazima uwe na uwezo wa ku handle ma stars. Ukiona wanaanza kukufunika usiwaondoe kubaliana na hali kwa maslahi ya club, cha msingi club ishamiri. Ukiona kiongozi anapenda kuzungukwa na mambumbumbu na kuwageuza watu wenye upeo mkubwa kuwa maadui, ujue Taasisi husika lazima ipoteze mweleko.

Leadership crisis;
Waanzilishi waliwaamini vijana, wakawajenga na kuwalea vema kwa ajili ya kukiongoza chama hicho. Baadaye wakaamua kwa ridhaa yao kukabidhi uongozi wa CDM kwa vijana hao. Lakini vijana hao ambao sasa ni wazee wameshindwa kurithisha weledi, uzoefu kwa kizazi kingine. Viongozi wana vikundi ndani ya chama kwa ajili kutetea uwepo wao ndani ya chama badala ya kuwaandaa vijana kwa ajili ya kukipambania chama. Miaka ya nyuma ilikuwa kawaida kwa vijana kupelekwa Europe kwa ajili ya mafunzo na kuwajengea uwezo, Myika, Zitto n.k ni mifano ya vijana waliolelewa na chama. Udhaifu wa uongozi umesababisha kutamalaki kwa sera ya zidumu fikra za kiongozi na yeyote atakayepishana na kiongozi anaoneka msaliti na hafai kwenye chama. Udhaifu huo umesababisha CDM ikose mipango na mikakati ya muda mrefu na muda mfupi. Kundi la wasomi lililoongozwa na kina Baregu limeyeyuka kwa sababu uongozi unajiona miungu watu, hauitaji fact zinazotokana na utafiti bali fikra na matamanio binafsi ya viongozi. Udhaifu huo umesababisha uongozi ufanye makosa makubwa kimaamuzi ambayo yamenyong'onyesha matumaini ya wafuasi hasa ambao siyo wanachama CDM lakini walikuwa na imani na kuiunga mkono CDM. Laiti kama wangekuwa na washauri na watafiti wazuri baadhi ya mitego ya kisiasa wangeiruka. Kwa sasa kila kiongozi ni speaker anasema chochoto na popote bila kupima athari za kisiasa za sasa na muda mrefu za matendo yao.

Maslahi binafsi;
viongozi wameanza kuweka mbele maslahi binafsi kama Mrema alivyokuwa anafanya NCCR. Kutokana na msukumo wa maslahi binafsi kuna kiongozi nadhani wa club ya simbaa aliwahi wakabidhi umoja wa wanawake na vijana wa club yake kwa mpinzania wake mkuu mwenyeki wa Tanzania Young Afrcn. Kadhalika akaingia kwenye negotiation ambayo hata mjinga alijua kuwa ulikuwa mtego ambao ulilenga kumweka ndege tunduni, ambapo hatma yake imepelekea yeye binafsi kuwa wakala wa timu pinzani.

Delegation of power kwa ngazi ya Mkoa, wilaya, kata na vijiji imefeli na hakuna mtu anayejisumbua.
Hauwezi kushinda vita kama hauna last mile warriors. lazima uwe na watu wenye mamlaka ya kufanya maamuzi haraka katika mazingira waliyopo (kata, vijiji, wilaya) badala ya kusubiri kamati kuu na baraza kuu.

CDM imeshindwa kuukamata mfumo
Badala ya kuukamata mfumo wao wanapambana na mfumo. hata pale mfumo unapotaka kujenga ukaribu nao wao wanaupiga mishare huku wakijua fikra kuwa siku ya mwisho hatma yao kimkakati itahitaji ushirikiano na mfumo. wana fursa ya kuukamata mfumo lakini hawaitumii. Maalimu Seif RIP alipopata fursa hii, aliitumia ipasavyo kule katika kisiwa cha karafuu Ukerewee naaliweza kupindue meza, sema ndio hivyo mambo mengine hayaelezeki.

Jambo ambao CDM wanapaswa kulijua na kulifanyia kazi kwa sasa; watu wengi ambao siyo wanachama wao wakiwemo baadhi ya the green team wanatamani wawe imara ili wawakabidhi jahazi. wimbi hilo halitokani na jitihada za viongozi wa CDM bali ni matokeo ya kuumizwa na kuwachoka the green team. endapo CDM wakiendelea kulegalega, ataibuka mtu kutoka the green team ataunda chama kimpya na wao watakuwa kama NCCR na TLP.
Mko nyuma ya key board as if haya yanayotokea hayawahusu
 
Back
Top Bottom