Tundu Lissu nenda taratibu, tumia hekima na busara kumaliza tofauti zako na Freeman Mbowe. Vinginevyo mnaiua CHADEMA

Chadema ife mara ngapi? By the way Watanzania ni kama wamegoma kuisapoti imebakia wanaharakati tuu.

Kina Heche wako wapi? 😂😂 Tangu lini watu dizaini ya kina Lisu wakawa na hekima? Umewahi ona wapi?

Kila mtu apambane kivyake.
 
Lissu huyu anayeunga mkono ushoga?
 
Acha kife ili tupate chama kipya na imara zaidi….
Mara nyingi kujenga nyumba mpya ni aghali ukilinganisha na kuziba kiraka.
Chama kipya muda haupo kabla ya uchaguzi huu wa serikali za mitaa hata uchaguzu mkuu mwakani.
Kwa saaa inatakiwa busara na mageuzi ya mawasiliano ndani ya chama.
Lissu hagombei pesa,wala Mbowe hagombei wafuasi.
 
Itakuwa ni simanzi na majonzi kuwa hekima inakosekana ndani ya Chama kikuu Cha upinzani hadi kipasuke vipande 2. Kuna kitu kimoja tu nacho ni Chadema kukaa na kumaliza tofauti hizi kwa Kila mwenye hofu kusema wazi wazi. Matumizi ya kuongea mitandaoni ni utovu wa nidhamu.
Fikirieni kwa miaka kadhaa Watanganyika walivyojitoa kwa ajili ya Chama na viongozi wake. Watu wamepotezwa, kuuliwa, kupewa vilema na wengine kufungwa. Kukuza mgogoro ni kutoitendea haki demokrasia na wanachama wa Chadema.
 
Tatizo la Chadema ni Mbowe,

Shida yenu tukianza kumsema humu kinazuka kile kikundi chake cha kikabila kumtetea...

Mbowe ni pro maslahi sana, hua namshauri Lissu atengeneze Chama kipya...

Najua kitachukua mda mrefu, lakini by 2030 kitakua tishio na tunaweza kuchukua nchi...

Kuendelea kuing'ang'ania Chadema, kuna siku watamshinda nguvu na kumzushia propaganda itakayochukua mda kuisafisha.
 
Chama lazima kifanye mambo yake ya kuhakikisha kinatamalaki all the way,all the time.
Sio kila anaejiunga na Chadema anakitakia mema Chadema.
Kuiga siyo shida weka wajumbe 7 wa kudumu ndio wenye chama wa kuhakikisha chama hakiyumbi, kura zao ndio muelekeo au maamuzi ya chama.
Chama hakiongozwi kwa mihemuko au hotuba nzuri za kuwaburudisha wanachama na wapenzi tu,kuna zaidi ya hayo.
 
Hakika.
 
Chadema ilishapoteza focus siku nyingi sana

Kimekua kikundi cha harakati na matukio
 
Ndio demokrasia hii?
 
Ushauri wako ni wa baadae sana endapo mikakati mingine itashindwa. Shida ya Chadema ni viongozi kuwa na mitizamo tofauti bila kuwa na chombo cha kuiunganisha hiyo mitizamo na kutengeneza mtizamo mmoja wenye nguvu. Ndiyo maana Lissu, Mbowe, Mnyika wa sasa wanaonekana ni tofauti sana na wale tuliowajua enzi zile. Walikuwa na kitu kama sijakosea kinaitwa Baraza la Wazee wa Chama. Sina uhakika kama wapo na wana nguvu gani sasa kukishauri na kusimamia mwenendo wa chama.
 
Kuwa na mitazamo tofauti siyo kosa kwenye chama cha siasa. Siyo kikundi cha kwaya kile kwamba kila mtu lazima acheze sawa na mwenzie
 
Lisu akomae hapo hapo, jamaa wanamzunguka hao
1. Tuwe tu wakweli chadema ya sasa pumzi ameishikilia Lissu
2. Mwenyekiti wetu umaarufu wake hata mvuto umepungua
3. Ninaamini Mwenyekiti wetu anaifaidi chadema kuliko chadema inavyonufaika
4. Mbowe ingefaa aachiwe na wengine yeye abaki kuwa mshauri tu.
5. Je miaka yote Mbowe hajaweza kuandaa mrithi?
 
Lissu iko siku atakujuta muda aliotumia kutumimikia chama ambacho kipo kwa ajili ya mbowe na kikundi chake toka Kaskazini.
 

View: https://x.com/LuhagaMpina/status/1856317859023958089?t=PWWX9l0lXdsqQitve7GHsA&s=19
 
Kwani ni lini tundu lissu aliwahi kuwa na hekima!
 
Tundu Lissu atimuliwe CHADEMA haraka
 
Mko nyuma ya key board as if haya yanayotokea hayawahusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…