Tundu Lissu nenda taratibu, tumia hekima na busara kumaliza tofauti zako na Freeman Mbowe. Vinginevyo mnaiua CHADEMA

ndiyo maana nikasema Lisu na Gachagua wanatofautiana nchi tu lakini wanafanya siasa za aina moja za kibinafsi, kuwadharau na kuwazodoa mabosi zao hadharini na kwamba ni wakoseaji wa kila kitu kilichofanywa na chama awali 🐒
 
Ukiona moshi jua moto ulishawaka muda mrefu 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Wazee wenyewe kama Ali kibao, ccm inawaua kiholela, halafu rekebisha hapo Kikwete sio Dokta.
 
Pole sana
 
Huyu Tundu Lissu hana shukrani , bila ya Mwamba Mbowe saa hizi angkuwa shimo la Tewa !!!!
 
Naunga mkono hoja kwa 100%.
 
Mkuu, mimi pia nilipata muda nikamsikikiza Tundu Lissu ameeleza masuala mengi na yote ameyafafanua uzuri sana.

Tatizo la Chadema ni mwenyekiti wao na wakilitambua hilo basi wanakuwa wamepiga hatua kubwa sana na watapata “more support”.

Mheshimiwa Mbowe sasa hivi azidi kudhihirisha kuwa hana nia ya kukiongoza Chadema kisawasawa na kujitayarisha kuwa chama mbadala wa CCM.

Tuchukulie Chadema imeshindwa uchaguzi wa serikali za mitaa, lakini bado Chadema kina uwezo wa kupata kura na wabunge kilowapoteza 2019/2020.

Yanayotakiwa kufanywa na uongozi wa juu wa Chadema ni kumweka mtu kati na kumwambia apishe wenye nia dhabiti wakiandae chama kiwe tayari kukikabili CCM kisawasawa kwani Chadema kimepoteza political landscape ya kisiasa na kilichobakia ni kuongelea pembeni ya uzio wa landscape hiyo.

Isitoshe Chadema sasa hivi yazidi kupoteza uwanja wa mapambano yaani ground game jambo ambalo wasijaribu kulikubali.

Mheshimiwa Mbowe awe mlezi na mshauri na awe mjumbe wa kudumu halmashauri kuu wa chama.

Pili, Chadema iajiri strategist zaidi ya wannę ambao watakiandaa chama kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwakani 2025. Sambamba na hilo pia aajiriwe meneja wa kampeni ambae ndie atashughulikia masuala yote ya rasilimali watu, usimamizi wa kampeni nchini kote.

Tatu, Chadema impitishe Tundu Lissu kuwa mwenyekiti mpya na wamuandae kuwa mgombea uraisi pamoja na kumpata mgombea mwenza.

Nina mengi ya kistratejia zaidi lakini ntakuja nayo pale tu Chadema itapojitambua kupitia uchambuzi wa kutumia formuła ya SWOT.

Pamoja na kutumia SWOT ni lazima Chadema itambue nani ni nani ndani ya chama.

Kwa kufanya hivyo kitaweza kurekebisha na kuboresha kitu chaitwa “ground game” ambayo ndo yaonekana kukididimiza chama.
 
Mafisi kukaa pamoja ni ngumu sana, sbb fisi ni walafi na hawawezi ridhika, na fisi hawezi badilika tabia yake
 
Lissu ni msaliti anayekiua CHADEMA kwa makusudi. Mmiliki wa CHADEMA Sultani Mbowe asimuache aendelee kumharibia chama. Mbowe fukuza hiyo LISSU.
 
Mkuu hizo ni njia za kivita zilizokaa kimafumbo hauwezi kuelewa mpaka upate watu wakusaidie kutegua fumbo hili. Nchi hii mkienda kwa kusikilizana hamuwezi kufika mbali kwangu mimi naona njia hii ni salama kuliko kudanganyana.
 
USHAURI:
CHADEMA kaeni chini, malizeni tofauti zenu amicably. Na kama kuna mambo yanayokwanza wengine, basi yashughulikiwe haraka ndani ya chama kwa taratibu za wazi za kichama....

Kuonesha tofauti zenu waziwazi huku nje ni hatari sana
Naunga mkono hoja, niliwahi kuuliza humu Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?
Msikilize hapa

Anaye ongoza timu ya Chadema kwenye vikao vya maridhiano ni Mwenyekiti wake, na KM, Lissu anauliza in public wana akili hawa?, maridhiano ya nusu mkate ameyaita ujinga, kumaanisha Mwenyekiti wake na KM wake ni ...

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…