Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

Mwalimu alikua sawa kwa kauli hiyo ya kutokumpa mtu urais akajaribu na imethibitika kwa magumagu maana yeye alisema kabisa hakujiandaa kuwa rais na nafasi hiyo aliipata tu kwa bahati na tunashuhudia kinachoendelea kwa sasa ni dhairi kuwa tuliempa nchi hakujiandaa hata kidogo bado yupo kwenye majaribio na ndo maana aishi kulia kwamba kazi hii ni ngumu ila pamoja ugumu wake haachii awapishe waliojiandaa...nasikitika kuwa mawazo yake yanamtuma kuwa matajiri wakiishi kama mashetani basi maskini wataishi kama malaika alie karibu nae wamwambie maskini ndo wanaishi kama mashetani na ndo wanaolimia meno na hadi sasa hela za mbegu hawana na matajiri wanaishi maisha yaleyale waliozoea maana wao walikua na akiba zao labda hadi akiba zao ziishe
 
Kawadanganye mabwega, kauli yako tuu hapa unaonyesha ni team lisasi, unajifanya unaumia na nyongeza harafu unampinga anayependa sheria ambae definitely atawaongeza kwa kufuata sheria!

Duuu
 
Mkuu umegusa ukweli kwenye eneo fulani. Huwa naamini na siasa zinazoanzia chini.Ili chama kiwe madhubuti, lazima kiwe na nguvu kwenye serikali za mitaa; kuanzia na viongozi wa vijiji na mitaa, madiwani na kisha kisogee kwenye eneo la ubunge.Hapa chama kitakuwa na mabaraza ya madiwani ambayo wanayaunda wao na baadae bunge walilolihodhi. Kuanzia hapo, ndo tunaweza kuongelea Urais. Kwa sasa, upinzani bado haujawa imara kivile.TL kwa mfano, labda atarajie kura za huruma za Watanzania, lakini kiutendaji anadeserve kuwa PM au Mwanasheria Mkuu ili kusimamia dola.
 

Me too
 
Kawadanganye mabwega, kauli yako tuu hapa unaonyesha ni team lisasi, unajifanya unaumia na nyongeza harafu unampinga anayependa sheria ambae definitely atawaongeza kwa kufuata sheria!

Duuu
Tundu Lissu????,kweli Mimi sipo,acha tuumie hivohivo
 
Kwa hiyo lowasa hagombei tena? Au lisu atagombea kupitia chama kipi? Kwa mipango na akili ya zito ukitazama kwa jicho la tatu anajitahidi sana kuwafool ukawa ili wampitishe yeye kugombea 2020, hii sasa inadhirisha vita ya madaraka ya wao kwa wao.

Hakuna vita

Strategy wanayotumia kwenda nayo opposition this time, si ya miaka na ya zama zile ya mazoea...

This time ni quite different, advanced one na ya kama tunagombana vile na ya kama tunawaunga mkono vile, kumbe ndiyo kilio chenu....

Ni mithiri ya gari moshi yenye injini mbili mbele na nyuma na zote zimewashwa na kuunguruma...

Hakuna tangazo linaloelekeza kuwa gari linaelekea wapi bali ajuaye ni dereva na control office pekee....

Hizi za kwako ni "traditional feelings" ama kwa kiswahili ni "hisia za utamaduni wa mazoea tu" na kwa kesi hii ni vyema sana CCM wakae mkao wa kufungasha virago....

Mtabaki na fikra hizihizi mwisho wa siku ni kama Makaburu wa Afrika ya Kusini na KANU ya Kenya ilivyofurumishwa mchana mchana kama wako ndotoni vile lakini kumbe ndiyo wanapotezwa hivyo!!
 
Reactions: mmh
Hapana uko kote ulikopendekeza hafai kabisa labda apo alipo angalau siyo mbaya, ukimpeleka uko kuwa Waziri wa Sheria au Mwanasheria Mkuu atatupoteza vibaya mmno maana uwa anapenda kufanya jambo kwa maslai yake binafsi, namjua vizuri sana huyo
 
Binafsi napenda Lissu ashike nchi kwani atafuata katiba na sharia za nchi jambo ambalo ni muhimu sana. Ila wabunge Chadema isipate wabunge zaidi ya 2/3 ili kupitisha mambo isiwe kwa ridhaa ya Chadema peke yake bali ishirikiane na vyama vingine kwa maslahi ya nchi kwa ujumla. Inasaidia kuondoa jeuri.
 
Anapanga kumng'oa Fatma Karume kwenye kiti cha Urais TLS, ila poa si alikua yeye kabla hajapata majanga, go Lissu TLS yako ilikua na nguvu sana rudi home uongoze wanasheria mkuu
 
Na huo ndio ukweli maendeleo na demokrasia haviendani ndio maana hata hao wanaojiita wanademocrasia wa Ulimwengu walipambana kwanza kupata maendeleo ndio wakaja na huu uchafu, kama unabisha nitajie nchi 5 zilizopiga hatua kimaendeleo wakiwa ktk mfumo shetani wa kidemokrasia
 
Mapenzi yakizidi na ujuha unaongezeka lkn pia kiwango cha ujinga kinakua juu, Lissu na uchumi wapi na wapi, tatizo la ufipa moja tu, Muhemko na hii itawafanya muwe wajinga maisha yenu yote
 
Tumia matakwa ya kwako labda utaweza,ulishindwa 2015 karibu 2020 matakwa ya ndoto zako za mchana utafanikisha,unataka kumwondoa point za kumwondoa huna si ukapuku huo
No way, Tundu Lissu is the right candidate...

Tunataka mtu wa kumwondoa shetani ktk kiti cha enzi alichoiba siyo hizo personal ambitions zako....!!

Look at the BIG PICTURE brother, usiangalie tumbo lako tu, matakwa yako tu
 
Wew utakuwa pungu
 
Huyu ana-backup kubwa ya mataifa ya nje na watanzania,watu hawatalala ule upande wa pili leo,huko kote anakofanya ziara siyo kwa bahati mbaya,
Sasa naelewa zile resolutions za mabunge ya EU na Marekani
 
MIHEMKO MIHEMKO MIHEMKO Tatizo la Ufipa ni moja tu, MIHEMKO, siku mkiweka mihemko pembeni mkatumia ubongo kufikiri ndio mtaupata japo Uwaziri, mihemko iliwaingia 2015 mkamsahau mfia chama mzee Slaa kwa sekunde moja tu, mkawaka na Mamvi na hatimae mkapotea, na hapa mtapotea zaidi nnaawaambia
 
Reactions: mmh
Magufuli na Lissu wanafanana EGO. Lissu akipata madaraka makubwa ya kuwa Rais naye atakuwa kama Joseph tu. Msidhani Lissu ni mvumilivu wa kukosolewa au kupingwa. Wanaofanya nae kazi karibu wanajua zaidi.

Halafu naye ni attention seeker mkubwa. Akiwa kwenye power atafanya PR stunts kama za Jiwe tu.

Kama mnabisha, tujaribuni kumpa tuone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…