Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

Kwa maoni yangu Mh. Tundu Lissu anafaa zaidi akifanya kazi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, DPP au waziri wa sheria na katiba. Urais ni mzuri lakini tutakosa kuona taste yake hasa ktk taaluma yake where it needed most. Mi napenda akisonga front ktk law battles na siyo administrative
Ila mkuu kuwa na rais anayeongoza kikatiba ni vizuri pia ...siyo rais anayetumia katiba iliyo kwenye kichwa chake.
 
Tundu Lissu????,kweli Mimi sipo,acha tuumie hivohivo
Kama Hata vichaa wanaweza kuongoza Tanzania kwanini Lissu awe kikwazo kwako? Hii nchi hata wewe mwenyewe unaweza kuiongoza tena inawezekana vizuri kuliko wengine maana haina katiba, katiba ni raisi!
 
Anataka kuja kugombea urais wakati huohuo anataka kuzunguka Ulaya kuichafua nchi anayotaka kuongoza. Huu ni uendawazimu wa hali ya juu kabisa.
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Jimbo lake Singida huko kashindwa kuongoza,familia yake kashindwa mwache aropoke tu.
watoto wale wanaitaji kusoma wakili mkuu rais wa nini sijui,sio kuja kusalimu hospitali. Mke pia anahitaji huduma.
Bado ww unafkiria kuwa na mikiki ya siasa!
Waonee huruma waliokuzunguka
Mbona aliyepo sasa hivi amebahatisha nafasi alionayo..na familia ni chali
 
Uchaguzi wa 2015 alishinda Lowassa tena Kwa kura nyingi lkn hilo halisemwi na waoga (ccm)
 
Hakuna vita

Strategy wanayotumia kwenda nayo opposition this time, si ya miaka na ya zama zile ya mazoea...

This time ni quite different, advanced one na ya kama tunagombana vile na ya kama tunawaunga mkono vile, kumbe ndiyo kilio chenu....

Ni mithiri ya gari moshi yenye injini mbili mbele na nyuma na zote zimewashwa na kuunguruma...

Hakuna tangazo linaloelekeza kuwa gari linaelekea wapi bali ajuaye ni dereva na control office pekee....

Hizi za kwako ni "traditional feelings" ama kwa kiswahili ni "hisia za utamaduni wa mazoea tu" na kwa kesi hii ni vyema sana CCM wakae mkao wa kufungasha virago....

Mtabaki na fikra hizihizi mwisho wa siku ni kama Makaburu wa Afrika ya Kusini na KANU ya Kenya ilivyofurumishwa mchana mchana kama wako ndotoni vile lakini kumbe ndiyo wanapotezwa hivyo!!
Wewe endelea kuota tu, sie tunawaza namna ya kumuongeza muda baada ya miaka kumi nyie eti mnawaza half time!! Nyie endeleeni na matunguli ya zzk tu sie tuna mungu
 
Nimesoma habari ya gazeti la Mwananchi kuhusu swala la Lissu kujiandaa na Urais 2020 hivyo kufanya idadi ya wagombea waliokwisha kutangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya Chadema kinyume kabisa na miongozo ya chama hicho kwa watia nia wake kuwa wawili mpaka sasa yaani Lissu na Lowassa.

Miongozo ya CHADEMA inawataka watia nia wa Urais kutangaza nia hiyo mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi mkuu ili kuepusha mpasuko ndani ya Chama. Aidha yuko Mbowe nae anataka kugombea Urais ila hatangazi ili apate nafasi ya kuwaengua wanaotangaza mapema wakati ukifika.

Kwa tunaomjua Lissu tunaamini kabisa kuwa hawezi kuwa kwenye nafasi kubwa kama Urais kwa sababu kubwa kuwa hayuko settled. Lissu anapaswa kuwa na chombo au mtu wa juu yake kumdhibiti. Lissu ni kama Lema, Wenje na sampuli hizo. Ni waongeaji, wakosoaji na wakitumwa kusemea jambo wana uwezo mkubwa wa kufanya.

Udhaifu wao mkubwa ni kwamba hawawezi kukaa kwenye kikao dakika 20 bila kutoka nje. Wako mbio mbio muda wote. Hawana ubunifu wao ni watekelezaji tu, ni watu wa visasi na makundi, wamekubuhu kwenye fitina hawa wote ndio walimpoteza Lytonga Mrema kwa kumgombanisha na wenzake akina Marando sasa wameshamgombanisha Mbowe na waliokuwa wapenzi wake akina Zitto, Dr. Slaa sasa wanataka Urais.

Dhambi kubwa ya Zitto na Dr Slaa CHADEMA ilikuwa ni kutangaza kugombea Urais. Waliosimamia mkakati wa kuvunja ndoto zao ni hawa vijana wa Lytonga Mrema waliotoka nae NCCR kwenda TLP halafu wakamtelekeza kule na kukimbilia CHADEMA. Kwasababu ni wabaguzi dhambi ile hawajawahi kuiacha ni sawa na kula nyama ya mtu.

Mimi binafsi namuunga mkono Lissu kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa sababu ndio pekee ninayemuona ana ujasiri wa kupambana na Mbowe japo hana mkakati. Simuungi mkono kwa sababu yeye atakuwa mwenyekiti mzuri kuliko Mbowe la hasha ila atavunja mwiko na kufungua mlango uliofungwa miaka mingi wa kupokezana vijiti ndani ya CHADEMA.

Aidha Lissu atatoa changamoto kwa siasa za upinzani nchini na kuzinogesha. Nampa tahadhari Lissu kuwa kama amesharubuniwa na Mbowe kuwa ataachiwa Urais na yeye aachie uenyekiti ameshashindwa kabla ya kuanza.

Kwa sasa Lissu focus kwenye Uenyekiti wa CHADEMA kwanza Urais unakuja tu wenyewe.

Nakutakia uponaji wa haraka Kamanda
 
Ashinde asishinde sisi tunataka Lissu asimame na Magufuli.
chadema hawawez kumsimamisha lissu kuwa mgombea.
lissu yupo more popular mitandaoni lakini mitaani hana hits yoyote.
na tukio ambalo limemuongezea crdt ni hili la kupigwa shaba.
pia ukiangalia ndani ya Jimbo.lake ni kama maendeleo yamechelewa so na uhakika .CCM watatumia tricks hiyo kumchafua...
 
Hapa ni kwa kuamua, lakini si kwa free & fair election [emoji850]
ahaa mkuu. uliona lini kiongozi wa Africa akatoka madarakan kwa sanduku la kura?!
madaraka matamu.na hivyo tumshukuru Mungu kwa hapa Tz hajatokea aliyenogewa lakini kwa upepo wa huyu "Bwana mkubwa" tuombe Mungu
 
Hakuna vita

Strategy wanayotumia kwenda nayo opposition this time, si ya miaka na ya zama zile ya mazoea...

This time ni quite different, advanced one na ya kama tunagombana vile na ya kama tunawaunga mkono vile, kumbe ndiyo kilio chenu....

Ni mithiri ya gari moshi yenye injini mbili mbele na nyuma na zote zimewashwa na kuunguruma...

Hakuna tangazo linaloelekeza kuwa gari linaelekea wapi bali ajuaye ni dereva na control office pekee....

Hizi za kwako ni "traditional feelings" ama kwa kiswahili ni "hisia za utamaduni wa mazoea tu" na kwa kesi hii ni vyema sana CCM wakae mkao wa kufungasha virago....

Mtabaki na fikra hizihizi mwisho wa siku ni kama Makaburu wa Afrika ya Kusini na KANU ya Kenya ilivyofurumishwa mchana mchana kama wako ndotoni vile lakini kumbe ndiyo wanapotezwa hivyo!!
Mkuu, kwa unavyowaza ingekuwa na viongozi wanawaza hivyo, ningediriki kusema, they have a dream to achieve.
But, najua kuna vitu hatupendi viwekwe wazi, lakini kiuhalisia the gents are too selfish.
 
Wewe endelea kuota tu, sie tunawaza namna ya kumuongeza muda baada ya miaka kumi nyie eti mnawaza half time!! Nyie endeleeni na matunguli ya zzk tu sie tuna mungu

Kuota🙄🙄🙄!!?

Mimi ninaota au wewe ndugu?
 
Back
Top Bottom