Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

Kuna kipindi JK alikuwa anapuyanga mpaka watu kama Kigwangallah na Aldefonce Birohe wakajua na wao wanaweza kuongoza Nchi. Marehemu JK Nyerere (RIP) aliwahi kutuasa kwamba uRais sio nafasi ya kumpa mtu kwa majaribio kwa kuwa tu aliyekuwepo madarakani alikuwa mbovu. I hope mwaka 2020 wapiga kura akili zao zitakuwa zimeshabarehe
Mwalimu alikua sawa kwa kauli hiyo ya kutokumpa mtu urais akajaribu na imethibitika kwa magumagu maana yeye alisema kabisa hakujiandaa kuwa rais na nafasi hiyo aliipata tu kwa bahati na tunashuhudia kinachoendelea kwa sasa ni dhairi kuwa tuliempa nchi hakujiandaa hata kidogo bado yupo kwenye majaribio na ndo maana aishi kulia kwamba kazi hii ni ngumu ila pamoja ugumu wake haachii awapishe waliojiandaa...nasikitika kuwa mawazo yake yanamtuma kuwa matajiri wakiishi kama mashetani basi maskini wataishi kama malaika alie karibu nae wamwambie maskini ndo wanaishi kama mashetani na ndo wanaolimia meno na hadi sasa hela za mbegu hawana na matajiri wanaishi maisha yaleyale waliozoea maana wao walikua na akiba zao labda hadi akiba zao ziishe
 
Ccm nimeichoka vibaya Sana inatunyanyasa Sana wafanya kazi kuhusu haki zetu za kupanda madaraja,nyongeza ya mshahara na ukisitaafu Tena tulipwe aslimila 25%,kweli kero Ni nyingi Sasa hvi hatuna amani na kazi hatuifurahii kazi kabisa,ila ndugu yangu kwa TUNDU LISSU ndo tutapotea jumla kabisa ,mkipata mwingine ndo tutawaunga mkono lakini Tundu Lissu akigombea hata nisipowapigia kura CCM watashinda tu ndo kinachonikera
Kawadanganye mabwega, kauli yako tuu hapa unaonyesha ni team lisasi, unajifanya unaumia na nyongeza harafu unampinga anayependa sheria ambae definitely atawaongeza kwa kufuata sheria!

Duuu
 
Narudia tena wapinzani hapa Tanzania urais wasahau. Wsngemsikia Mwalimu Nyerere kama wasingekua CCM B labda sasa wangeshachukua nchi. Mwaka 1995 mwalimu aliwaambia wajikite kwenye ubunge ili walichukue bunge maana hata kama rais atatoka ccm wao ndo watatengeneza serikali wakadanganywa na ujio wa mzee wa Kiraracha wakapoteza nafasi nzuri. Ieleweke mwaka ule ccm haikupendwa na sisi vijana vyuoni. Kumbuka Kimaro Muhimbili Mbatia Mlimani. Kiburi cha kina Marando kikatufikisha hapa tulipo. Sada hivi kuitoa ccm wazo hilo ondoeni labda muwe kweli mna akili ya NYUMBU mkiamini Lissu anaweza kushinda
Mkuu umegusa ukweli kwenye eneo fulani. Huwa naamini na siasa zinazoanzia chini.Ili chama kiwe madhubuti, lazima kiwe na nguvu kwenye serikali za mitaa; kuanzia na viongozi wa vijiji na mitaa, madiwani na kisha kisogee kwenye eneo la ubunge.Hapa chama kitakuwa na mabaraza ya madiwani ambayo wanayaunda wao na baadae bunge walilolihodhi. Kuanzia hapo, ndo tunaweza kuongelea Urais. Kwa sasa, upinzani bado haujawa imara kivile.TL kwa mfano, labda atarajie kura za huruma za Watanzania, lakini kiutendaji anadeserve kuwa PM au Mwanasheria Mkuu ili kusimamia dola.
 
Kwa maoni yangu Mh. Tundu Lissu anafaa zaidi akifanya kazi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, DPP au waziri wa sheria na katiba. Urais ni mzuri lakini tutakosa kuona taste yake hasa ktk taaluma yake where it needed most. Mi napenda akisonga front ktk law battles na siyo administrative

Me too
 
Kawadanganye mabwega, kauli yako tuu hapa unaonyesha ni team lisasi, unajifanya unaumia na nyongeza harafu unampinga anayependa sheria ambae definitely atawaongeza kwa kufuata sheria!

Duuu
Tundu Lissu????,kweli Mimi sipo,acha tuumie hivohivo
 
Kwa hiyo lowasa hagombei tena? Au lisu atagombea kupitia chama kipi? Kwa mipango na akili ya zito ukitazama kwa jicho la tatu anajitahidi sana kuwafool ukawa ili wampitishe yeye kugombea 2020, hii sasa inadhirisha vita ya madaraka ya wao kwa wao.

Hakuna vita

Strategy wanayotumia kwenda nayo opposition this time, si ya miaka na ya zama zile ya mazoea...

This time ni quite different, advanced one na ya kama tunagombana vile na ya kama tunawaunga mkono vile, kumbe ndiyo kilio chenu....

Ni mithiri ya gari moshi yenye injini mbili mbele na nyuma na zote zimewashwa na kuunguruma...

Hakuna tangazo linaloelekeza kuwa gari linaelekea wapi bali ajuaye ni dereva na control office pekee....

Hizi za kwako ni "traditional feelings" ama kwa kiswahili ni "hisia za utamaduni wa mazoea tu" na kwa kesi hii ni vyema sana CCM wakae mkao wa kufungasha virago....

Mtabaki na fikra hizihizi mwisho wa siku ni kama Makaburu wa Afrika ya Kusini na KANU ya Kenya ilivyofurumishwa mchana mchana kama wako ndotoni vile lakini kumbe ndiyo wanapotezwa hivyo!!
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Kwa maoni yangu Mh. Tundu Lissu anafaa zaidi akifanya kazi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, DPP au waziri wa sheria na katiba. Urais ni mzuri lakini tutakosa kuona taste yake hasa ktk taaluma yake where it needed most. Mi napenda akisonga front ktk law battles na siyo administrative
Hapana uko kote ulikopendekeza hafai kabisa labda apo alipo angalau siyo mbaya, ukimpeleka uko kuwa Waziri wa Sheria au Mwanasheria Mkuu atatupoteza vibaya mmno maana uwa anapenda kufanya jambo kwa maslai yake binafsi, namjua vizuri sana huyo
 
Binafsi napenda Lissu ashike nchi kwani atafuata katiba na sharia za nchi jambo ambalo ni muhimu sana. Ila wabunge Chadema isipate wabunge zaidi ya 2/3 ili kupitisha mambo isiwe kwa ridhaa ya Chadema peke yake bali ishirikiane na vyama vingine kwa maslahi ya nchi kwa ujumla. Inasaidia kuondoa jeuri.
 
Anapanga kumng'oa Fatma Karume kwenye kiti cha Urais TLS, ila poa si alikua yeye kabla hajapata majanga, go Lissu TLS yako ilikua na nguvu sana rudi home uongoze wanasheria mkuu
 
Niko tayari kufikiria kumpa kura yangu (akipewa nafasi na chama chake) hasa kama ata ahidi utawala wa sheria na haki vikiendana na kutupa mifumo (institutions )bora na madhubuti. Huyu mwingine ni wazi njia hiyo amethibitisha hataitembea kwani "ana amini" (kwa vitendo vyake) kuwa maendeleo na demokrasia haviendi pamoja.
Na huo ndio ukweli maendeleo na demokrasia haviendani ndio maana hata hao wanaojiita wanademocrasia wa Ulimwengu walipambana kwanza kupata maendeleo ndio wakaja na huu uchafu, kama unabisha nitajie nchi 5 zilizopiga hatua kimaendeleo wakiwa ktk mfumo shetani wa kidemokrasia
 
I also agree Tundu Lissu is the right candidate for presidency in 2020 for opposition in general.....

Siyo Edward Lowassa, si Fredrick Sumaye na wala si Zitto Kabwe and I know hawezi kuwa Freeman Mbowe wala Saed Kubenea ama Lazaro Nyalandu ama Fahmi Dovutwa...

For sure, kama wanataka kuleta hamasa na amsha amsha ya watu kuunga mkono opposition ktk uchaguzi ujao, Tundu Lissu is the right pick hadi kwenye ushindi...

SIFA ZA TUNDU ANTIPAS MUGHWAI LISSU KUONESHA KUWA NDIYE RAIS AJAYE 2020 - 2025:
• Ni mjuvi wa sheria za ndani na za kimataifa kwa kiwango cha kutisha sana

• Anayo national and international exposure ya kutosha na kuzidi sana

• Ni mwanadiplomasia mwenye uwezo wa kutosha sana

• Ndiye mtu pekee aliyepitia misukosuko inayofanana na ya Nelson Mandela (aliyewahi fungwa gerezani na kuja kuwa Rais wa Jamhuri ya watu wa Afrika ya Kusini).

Huyu naye (TAML) kafungwa mara nyingi sana na kifungo cha mwisho ni hiki cha zaidi ya mwaka sasa cha maumivu ya kuuguza majeraha ya risasi za SMG zilizojaribu kuzima nyota yake ya Uongozi na Utawala kwa kumuua kabisa

• Ni mwana Uchumi mbobevu kabisa.

Na kwa kifupi kabisa huyu bwana ndiye mtu sahihi na kipekee kwa sasa mwenye uwezo wa kukabiliana na Pombe Magufuli mpaka amlete kwenye mamlaka ya kutii na hata kumwangusha chini kwa kishindo kikuu kama Daudi alivyomwangusha Mfilisti Goliath!!

Kama Tundu Lissu atakubali kuwa mgombea Urais mwaka 2020, mimi peke yangu na kwa gharama zangu mwenyewe nitahakikisha natafutia kura za [√] zisizopungua 1,000,000 kwa ajili yake na chama atakacho gombea!!
Mapenzi yakizidi na ujuha unaongezeka lkn pia kiwango cha ujinga kinakua juu, Lissu na uchumi wapi na wapi, tatizo la ufipa moja tu, Muhemko na hii itawafanya muwe wajinga maisha yenu yote
 
Tumia matakwa ya kwako labda utaweza,ulishindwa 2015 karibu 2020 matakwa ya ndoto zako za mchana utafanikisha,unataka kumwondoa point za kumwondoa huna si ukapuku huo
No way, Tundu Lissu is the right candidate...

Tunataka mtu wa kumwondoa shetani ktk kiti cha enzi alichoiba siyo hizo personal ambitions zako....!!

Look at the BIG PICTURE brother, usiangalie tumbo lako tu, matakwa yako tu
 
Jimbo lake Singida huko kashindwa kuongoza,familia yake kashindwa mwache aropoke tu.
watoto wale wanaitaji kusoma wakili mkuu rais wa nini sijui,sio kuja kusalimu hospitali. Mke pia anahitaji huduma.
Bado ww unafkiria kuwa na mikiki ya siasa!
Waonee huruma waliokuzunguka
Wew utakuwa pungu
 
Huyu ana-backup kubwa ya mataifa ya nje na watanzania,watu hawatalala ule upande wa pili leo,huko kote anakofanya ziara siyo kwa bahati mbaya,
Sasa naelewa zile resolutions za mabunge ya EU na Marekani
 
MIHEMKO MIHEMKO MIHEMKO Tatizo la Ufipa ni moja tu, MIHEMKO, siku mkiweka mihemko pembeni mkatumia ubongo kufikiri ndio mtaupata japo Uwaziri, mihemko iliwaingia 2015 mkamsahau mfia chama mzee Slaa kwa sekunde moja tu, mkawaka na Mamvi na hatimae mkapotea, na hapa mtapotea zaidi nnaawaambia
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Magufuli na Lissu wanafanana EGO. Lissu akipata madaraka makubwa ya kuwa Rais naye atakuwa kama Joseph tu. Msidhani Lissu ni mvumilivu wa kukosolewa au kupingwa. Wanaofanya nae kazi karibu wanajua zaidi.

Halafu naye ni attention seeker mkubwa. Akiwa kwenye power atafanya PR stunts kama za Jiwe tu.

Kama mnabisha, tujaribuni kumpa tuone.
 
Back
Top Bottom