Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

Na mm nna hakika "chadema" hawawezi kuhudhuria maana katka chaguz zote hao "chadema" ndo huwa wanakataa.. Kuna kipndi 2015 katka chaguz za wabunge walikua wanaonyesha live "chadema" wakaaona wanagaragazwa wakastitisha Mara moja huo ujinga
Yaani hasa wa wagombea Urais nani anaweza kumgalagaza JPM kwa hoja? Hakuna lazima waingie mitini
 
Nimesoma habari ya gazeti la Mwananchi kuhusu swala la Lissu kujiandaa na Urais 2020 hivyo kufanya idadi ya wagombea waliokwisha kutangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya Chadema kinyume kabisa na miongozo ya chama hicho kwa watia nia wake kuwa wawili mpaka sasa yaani Lissu na Lowassa.

Miongozo ya CHADEMA inawataka watia nia wa Urais kutangaza nia hiyo mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi mkuu ili kuepusha mpasuko ndani ya Chama. Aidha yuko Mbowe nae anataka kugombea Urais ila hatangazi ili apate nafasi ya kuwaengua wanaotangaza mapema wakati ukifika.

Kwa tunaomjua Lissu tunaamini kabisa kuwa hawezi kuwa kwenye nafasi kubwa kama Urais kwa sababu kubwa kuwa hayuko settled. Lissu anapaswa kuwa na chombo au mtu wa juu yake kumdhibiti. Lissu ni kama Lema, Wenje na sampuli hizo. Ni waongeaji, wakosoaji na wakitumwa kusemea jambo wana uwezo mkubwa wa kufanya.

Udhaifu wao mkubwa ni kwamba hawawezi kukaa kwenye kikao dakika 20 bila kutoka nje. Wako mbio mbio muda wote. Hawana ubunifu wao ni watekelezaji tu, ni watu wa visasi na makundi, wamekubuhu kwenye fitina hawa wote ndio walimpoteza Lytonga Mrema kwa kumgombanisha na wenzake akina Marando sasa wameshamgombanisha Mbowe na waliokuwa wapenzi wake akina Zitto, Dr. Slaa sasa wanataka Urais.

Dhambi kubwa ya Zitto na Dr Slaa CHADEMA ilikuwa ni kutangaza kugombea Urais. Waliosimamia mkakati wa kuvunja ndoto zao ni hawa vijana wa Lytonga Mrema waliotoka nae NCCR kwenda TLP halafu wakamtelekeza kule na kukimbilia CHADEMA. Kwasababu ni wabaguzi dhambi ile hawajawahi kuiacha ni sawa na kula nyama ya mtu.

Mimi binafsi namuunga mkono Lissu kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa sababu ndio pekee ninayemuona ana ujasiri wa kupambana na Mbowe japo hana mkakati. Simuungi mkono kwa sababu yeye atakuwa mwenyekiti mzuri kuliko Mbowe la hasha ila atavunja mwiko na kufungua mlango uliofungwa miaka mingi wa kupokezana vijiti ndani ya CHADEMA.

Aidha Lissu atatoa changamoto kwa siasa za upinzani nchini na kuzinogesha. Nampa tahadhari Lissu kuwa kama amesharubuniwa na Mbowe kuwa ataachiwa Urais na yeye aachie uenyekiti ameshashindwa kabla ya kuanza.

Kwa sasa Lissu focus kwenye Uenyekiti wa CHADEMA kwanza Urais unakuja tu wenyewe.

Nakutakia uponaji wa haraka Kamanda
Ila wewe jamaa roho ngumu kweli. Unakuwa msemaji wa hiari wa Chadema bila kuombwa wakati uliikataa Chadema wewe mwenyewe? Unashauri ili iweje wakati muda wote unaombea wenzako mabaya muda wote.
 
Kama Baba Jesca anatawala kwa raha zake hakuna anayeshindwa kuongoza geto letu TZ
 
kuna watu mkifungua mdomo ndo ujinga unajidhihiridha wazi. nilitegemea utoe sababu kwa nini hafai uraisi ukilinganisha uwezo wake na majukumu ya uraisi.

kilicho jaa kwenye bandiko lako ni chuki juu ya chadema
 
Lowasa bado yupo tu
Lowasa ana nyota kali lakin hana maeno ya ushawishi anaomba kura kama bado yupo ccm
Bodaboda, machinga, mama ntilie hao watakuwa rafiki zangu, PIPOZI PIPOZI
 
Huyu ana-backup kubwa ya mataifa ya nje na watanzania,watu hawatalala ule upande wa pili leo,huko kote anakofanya ziara siyo kwa bahati mbaya,
Sasa naelewa zile resolutions za mabunge ya EU na Marekani

..walifikiri wanaweza kufanya tukio la kinyama kama lile halafu hao wakubwa wakaendelea kuwachekea.

..na kwa ujinga wao wakaongeza kufanya mambo mengine, hata yanayogusa hisia za walipa kodi na wanaowaweka madarakani wafadhili wetu.

..matokeo yake wafadhili kuchomoa makucha yao. Likifanyika kosa lingine kuna mtu ataparurwa na kupata michubuko na makovu mskubwa.
 
Baada ya Lissu The Great kutangaza nia , kichaka kilichojaa mijusi na panya kimelipuliwa na kiberiti , wadudu wote chali !
 
Kwa kuzingatia sifa kuu mbili tu muhimu Zitto ni zaidi ya Lissu kwa nafasi ya Urais Upinzani. Sifa zangu mbili ni

1. Ukomavu wa kisiasa
Zitto amekomaa kisiasa kuliko Lissu. Zitto amekabiliwa na misukosuko mingi ya kisiasa na amevuka yote.

2. Exposure (Kujua na kujulikana)
Zitto anajua mambo mengi sana. Anajulikana sana kitaifa na kimataifa. Ana network kubwa sana duniani na ndani ya Tanzania. Zitto ana deserve kuwa Rais na atamudu zaidi kuliko Lissu.

Lissu achukue Uenyekiti wa Chadema kwanza ndio awaze Urais
 
Back
Top Bottom