pachachiza
JF-Expert Member
- Oct 18, 2012
- 1,863
- 2,757
Umepata na usemaji wa Zitto pia!Zitto hawezi kukubali atatumia 2020 kujitangaza kwa 2025
Hongera mkuu mwaka unaumaliza vzr.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umepata na usemaji wa Zitto pia!Zitto hawezi kukubali atatumia 2020 kujitangaza kwa 2025
Hongera kwa maendeleo mazuri ya matibabu, naunga mkono wazo la wewe kuwa mgombea urais endapo utapitishwa na Ukawa, lakini sikubaliani na wazo la wewe kurudi Tanzania kwa sasa kutokana na unavyowatia hofu watawala wanaweza kutungua ndege uliyopanda hata kama ina abiria 300 bora wafe wote ili mradi wakuue wewe!Wakati vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 likianza chini kwa chini, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema yupo tayari kugombea urais ikiwa vyama vya upinzani vitampa ridhaa hiyo.
Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30, Septemba 7 mwaka jana akiwa Dodoma na watu wasiojulikana, amesema hayo jana wakati akizungumza na Mwananchi kuhusu maendeleo ya afya yake.
Mwanasiasa huyo alisema yeye ni mwanachama wa Chadema na hawezi kufanya jambo pasi na kuridhiwa na chama chake au vyama washirika wa Chadema kwani kufanya hivyo ni kinyume cha taratibu na maadili.
Kauli ya Lissu kuhusu kugombea urais mwaka 2020 imetokana na swali aliloulizwa kutokana na kuwa miongoni mwa wanasiasa wa upinzani wanaotajwatajwa, “Wakikaa katika vikao na kunipa bendera, nitakubali kubeba msalaba huo mzito kwa mikono miwili.”
Pia aliulizwa, ikiwa hataombwa na chama atajitosa mwenyewe kuwania nafasi hiyo? Rais huyo wa zamani wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) alisema, “Maadili yangu, unaambiwa ukiwa katika chama lazima upewe fursa kwa hiyo nitasubiri fursa hiyo.”
Katika Uchaguzi Mkuu uliopita wa 2015, vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF vilimsimamisha Edward Lowassa kuwania nafasi ya urais na licha ya kushindwa Dk John Magufuli wa CCM, alipata kura nyingi ambazo hazijawahi kufikiwa na mgombea yeyote wa upinzani.
Katika uchaguzi huo, ilishuhudiwa kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa vyama vingi ulipoanza mwaka 1995, upinzani ukipata kura zaidi ya milioni sita ikiwa ni tofauti ya kura milioni mbili dhidi ya mshindi wa nafasi hiyo.
Lowassa alipata kura milioni 6.01 sawa na asilimia 39.97 huku Dk Magufuli akiibuka mshindi kwa kupata kura milioni 8.9 sawa na asilimia 58.46.
Kuhitimisha matibabu Desemba 31
Kuhusu afya yake, Lissu ambaye ni mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni alisema anatarajia kuanza mwaka akiwa hana vyuma alivyowekewa Julai 9 katika mguu wake wa kulia ili kuunganisha mifupa.
“Desemba 31 nitafanyiwa upasuaji wa mwisho wa kuondoa hii antena ambayo nimekaa nayo kwa miezi sita tangu Julai 9 na nimeelezwa na madaktari kuwa mfupa uliokuwa uunge umeunga na mfupa uliotakiwa kuota unaendelea vizuri,” alisema
Lissu na kuongeza:
“Yaani Jumatatu (Desemba 31) nitahitimisha kazi ya kitabibu na nitaanza mwaka mpya (2019) na mguu mpya ambao hauna chuma.”
Lissu alisema baada ya kuondolewa kwa vyuma, kitakachofuata ni mazoezi ya kutembea na taratibu ataachana na magongo.
Baada ya hapo, Lissu alisema ataanza kuhudhuria vikao mbalimbali ambayo amealikwa katika mataifa ya Ulaya.
Alisema Januari 14 amealikwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na Umoja wa Ulaya (EU) Brussels, Ubelgiji na Februari mwakani amepata mwaliko wa wiki moja huko Washington Marekani.
“Huko kote nakwenda kuzungumzia kile kilichonitokea Septemba 7 (mwaka jana) lakini kile ambacho kinaendelea nyumbani (Tanzania) na mambo mengine,” alisema.
Kurudi Tanzania badobado kwanza
Alipoulizwa kwamba kuanza wake kusafiri nchi mbalimbali bila shaka ni wakati wake wa kurejea nyumbani, mwanasheria mkuu huyo wa Chadema alisema, “Katikati ya mwakani naweza kurejea. Kuanza mazoezi hakutanizuia kurejea kwani naweza kurudi nyumbani na nikawa nakuja huku (Ubelgiji) kwa madaktari.”
Hata hivyo, Lissu alisema hilo la kurejea nchini litafanikiwa baada ya kufanya mazungumzo na watu mbalimbali ikiwamo viongozi wenzake wa kisiasa pamoja na Serikali.
“Serikali itapaswa kunieleza usalama wangu utakuwaje baada ya kurejea, ingawa jukumu la Serikali ni kulinda raia wake na mimi ni miongoni mwao hasa ukizingatia kile kilichonitokea,” alisema.
Akigusia harakati zake za kupigania demokrasia, Lissu alisema , “Kama nilivyowahi kusema, sitarudi nyuma na mapambano ya kupigania demokrasia si ya wanasiasa pekee, bali makundi mbalimbali kama madaktari, waandishi wa habari, wakulima, wavuvi, bodaboda na wengine.”
Aliunga mkono hatua ya vyama vya Chaumma na ACT- Wazalendo kushirikiana na vyama vya Ukawa vya Chadema, CUF, NLD na NCCR-Mageuzi kutoa tamko la pamoja kuhusu mwaka 2019.
“Umoja ni nguvu utengano ni dhaifu, katika mapambano ya demokrasia kushirikiana ni muhimu zaidi na hicho walichokubaliana mwaka 2019 ni mwaka wa kupigania demokrasia nami nakiunga mkono asilimia 100,” alisema.
Chanzo: Mwananchi
Mbavu sina tena,...et mtachagua jiwe lenuHata yakiwekwa ma JIWE mawili. Tutachagua Jiwe letu. Lenu tunaliacha.
Ni kukomoa tu. Adabu irudi.
Mweeeh!!Hii habari kama jiwe kaipata basi mlango wa Choo uko wazi muda wote
PumbaNamshaaga sana lisu anamuogopa mbowe kuliko raisi wa jamhuri, bila shaka mbowe ni mtu hatari sana. Sasa kama anamuogopa na kumyenyekea mbowe kiasi hiko, ataweza uraisi kweli, jibu ni no, aanzie kwanza umwenyekiti chadema then akitoboa ndo tuone
Jimbo lake Singida huko kashindwa kuongoza,familia yake kashindwa mwache aropoke tu.
watoto wale wanaitaji kusoma wakili mkuu rais wa nini sijui,sio kuja kusalimu hospitali. Mke pia anahitaji huduma.
Bado ww unafkiria kuwa na mikiki ya siasa!
Waonee huruma waliokuzunguka
wewe ndiye mwewesekaji mkuu
Sio mbaya ndio uhuru wa maoni kwenye post yako namba moja. Ila kwa taarifa yako kuwa rais wa Tanzania kunahitaji tu kuwa na akili timamu. Hiyo ndio sifa pekee yenye kubeba asilimia 90. Hizo asilimia 10 ndio sifa nyinginezo. Kwenye nchi ambayo rais hashitakiwi kwa kosa lolote afanyalo akiwa madarakani ni sifa gani kubwa ya muhimu zaidi ya akili timamu?
Kama kweli, msilalamike Kura zimeibiwa, maana kwa vyovyote hazitatosha, safari hii acheni maigiza.Sio mbaya ndio uhuru wa maoni kwenye post yako namba moja. Ila kwa taarifa yako kuwa rais wa Tanzania kunahitaji tu kuwa na akili timamu. Hiyo ndio sifa pekee yenye kubeba asilimia 90. Hizo asilimia 10 ndio sifa nyinginezo. Kwenye nchi ambayo rais hashitakiwi kwa kosa lolote afanyalo akiwa madarakani ni sifa gani kubwa ya muhimu zaidi ya akili timamu?
Kuna mtu namuona anaweka mpira kwapani fastaa!TANGAZO:
Kesho tarehe 24/10/2020 kutakuwa na mdahalo wa kitaifa wa kufunga kampeni katika ukumbi wa Nkurumah;
Wagombea wanaotarajiwa kuhudhuria;
J.P. Magufuli - CCM
T.A. Lissu - CHADEMA
H.R. Sipunda - CHAUMA
Z.R. Kabwe - ACT Wazalendo
NYOTE MNAKARIBISHWA.
Inawezana ndio Princess huyu mfoji vyetiSasa kama hujui hata kuandika neno Rais, napata wasiwasi hata uwezo wako wa kuchangia hapa jukwaani
Hawa jamaa bhana,2020 Mara twende na Membe mwanadiplomasia aliebobea,Jasusi aliebobea,sasa hivi tayar yameshabadir gia
Hahahahahahah