Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Niko tayari kugombea Urais mwaka 2020 nikipewa ridhaa na Upinzani

ahaa mkuu. uliona lini kiongozi wa Africa akatoka madarakan kwa sanduku la kura?!
madaraka matamu.na hivyo tumshukuru Mungu kwa hapa Tz hajatokea aliyenogewa lakini kwa upepo wa huyu "Bwana mkubwa" tuombe Mungu
Ikiwa hivyo kuna haja gani ya kufurahia na kushabikia matokeo ya kupikwa na yanayojulikana ??!!. Mtu yeyote anayeshabikia hali hiyo ni TAHAHIRA kabisa .
 
Kwa maoni yangu Mh. Tundu Lissu anafaa zaidi akifanya kazi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali, DPP au waziri wa sheria na katiba. Urais ni mzuri lakini tutakosa kuona taste yake hasa ktk taaluma yake where it needed most. Mi napenda akisonga front ktk law battles na siyo administrative
Akubali rushwa hiyo toka CCM?
 
Kwani Jiwe alianzia uenyekiti CCM?
Alikuwa waziri kwa miaka 20, so kulikuwa na kitu cha kumpima, sio huyu toka atokako tu eti direct raisi! Chadema wampe uenyekiti then tuone ufanisi wake
 
Akili zako matope tupu, huna unalolijua. CDM sio lazima uwe mwenyekiti ndio ugombee Urais!! Peleke mbele ushamba wako.
 
Magufuli alikuwa kwanza mwenyekiti wa ccm ndio akawa rais?
Alikuwa waziri for 20 years ndio kilikuwa kipimo chake, huyo lisu awe mkiti kwanza wa chadema tuone ufanisi wake before.
 
Na huo ndio ukweli maendeleo na demokrasia haviendani ndio maana hata hao wanaojiita wanademocrasia wa Ulimwengu walipambana kwanza kupata maendeleo ndio wakaja na huu uchafu, kama unabisha nitajie nchi 5 zilizopiga hatua kimaendeleo wakiwa ktk mfumo shetani wa kidemokrasia
Kama mna amini hivyo badilisheni katiba tusiwe na vyama vingi, wala haki za binadamu tuwe nchi inayo ongozwa na dictator officially. Vinginevyo mnatulisha matango pori kujifanya wanademokrasia huku mkitaka na kujitahidi kufuta sauti za wengine zisisike na chaguzi zisio kuwa huru wala za haki. Maendeleo ya Hitler na Qaddafi kwa mfano yali ishia wapi?
 
Akili zako matope tupu, huna unalolijua. CDM sio lazima uwe mwenyekiti ndio ugombee Urais!! Peleke mbele ushamba wako.
Kwa nini hamtaki kumpa uenyekiti kama kweli anafaa? Machadema bana hayajielewagi kabisa. Na yatazidi kuteseka kufikiria vitu visivyowezekana
 
wa
unanikumbusha mwanamke akizaa watoto wawili, wakati anazaa anajiapiza hazai tena!..ghafla mimba

hivi kwa TZ hii, tume hii, upinzani huu na record za JPM za barabara kila kona, Lissu anamtisha nani??

kama EL alifikia pale, record yake haiji kuvunjwa miaka ya karibuni
tumishi tunalia mhe: katusahau ngoja tuhamie airtel
 
Bila shaka wewe ndiye kwenye post moja hapa JF umeelezewa kuhusika na wizi na uvujaji wa pesa ndani ya CDM?
 
huo ndio ulikua mpango mkakati wao Wajanja tulijua zamani
labda ashindane kuwa mwenyekiti wa chadema
 
Kuanzia leo Lissu amesababisha watu wasiyojulikana kupumulia mashine
 
Nimesoma habari ya gazeti la Mwananchi kuhusu swala la Lissu kujiandaa na Urais 2020 hivyo kufanya idadi ya wagombea waliokwisha kutangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya Chadema kinyume kabisa na miongozo ya chama hicho kwa watia nia wake kuwa wawili mpaka sasa yaani Lissu na Lowassa.

Miongozo ya CHADEMA inawataka watia nia wa Urais kutangaza nia hiyo mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi mkuu ili kuepusha mpasuko ndani ya Chama. Aidha yuko Mbowe nae anataka kugombea Urais ila hatangazi ili apate nafasi ya kuwaengua wanaotangaza mapema wakati ukifika.

Kwa tunaomjua Lissu tunaamini kabisa kuwa hawezi kuwa kwenye nafasi kubwa kama Urais kwa sababu kubwa kuwa hayuko settled. Lissu anapaswa kuwa na chombo au mtu wa juu yake kumdhibiti. Lissu ni kama Lema, Wenje na sampuli hizo. Ni waongeaji, wakosoaji na wakitumwa kusemea jambo wana uwezo mkubwa wa kufanya.

Udhaifu wao mkubwa ni kwamba hawawezi kukaa kwenye kikao dakika 20 bila kutoka nje. Wako mbio mbio muda wote. Hawana ubunifu wao ni watekelezaji tu, ni watu wa visasi na makundi, wamekubuhu kwenye fitina hawa wote ndio walimpoteza Lytonga Mrema kwa kumgombanisha na wenzake akina Marando sasa wameshamgombanisha Mbowe na waliokuwa wapenzi wake akina Zitto, Dr. Slaa sasa wanataka Urais.

Dhambi kubwa ya Zitto na Dr Slaa CHADEMA ilikuwa ni kutangaza kugombea Urais. Waliosimamia mkakati wa kuvunja ndoto zao ni hawa vijana wa Lytonga Mrema waliotoka nae NCCR kwenda TLP halafu wakamtelekeza kule na kukimbilia CHADEMA. Kwasababu ni wabaguzi dhambi ile hawajawahi kuiacha ni sawa na kula nyama ya mtu.

Mimi binafsi namuunga mkono Lissu kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa sababu ndio pekee ninayemuona ana ujasiri wa kupambana na Mbowe japo hana mkakati. Simuungi mkono kwa sababu yeye atakuwa mwenyekiti mzuri kuliko Mbowe la hasha ila atavunja mwiko na kufungua mlango uliofungwa miaka mingi wa kupokezana vijiti ndani ya CHADEMA.

Aidha Lissu atatoa changamoto kwa siasa za upinzani nchini na kuzinogesha. Nampa tahadhari Lissu kuwa kama amesharubuniwa na Mbowe kuwa ataachiwa Urais na yeye aachie uenyekiti ameshashindwa kabla ya kuanza.

Kwa sasa Lissu focus kwenye Uenyekiti wa CHADEMA kwanza Urais unakuja tu wenyewe.

Nakutakia uponaji wa haraka Kamanda

Hatuchaguliwa mwenyekiti wala mgombea urais na misukele ya lumumba, wewe endelea tu kutumika kiboya hapo lumumba lakini kuteuliwa huteuliwi ng'o, rekodi yako ya kukwapua hela Chadema inakuandama mpaka siku unaingia kaburini.
 
Nimesoma habari ya gazeti la Mwananchi kuhusu swala la Lissu kujiandaa na Urais 2020 hivyo kufanya idadi ya wagombea waliokwisha kutangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya Chadema kinyume kabisa na miongozo ya chama hicho kwa watia nia wake kuwa wawili mpaka sasa yaani Lissu na Lowassa.

Miongozo ya CHADEMA inawataka watia nia wa Urais kutangaza nia hiyo mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi mkuu ili kuepusha mpasuko ndani ya Chama. Aidha yuko Mbowe nae anataka kugombea Urais ila hatangazi ili apate nafasi ya kuwaengua wanaotangaza mapema wakati ukifika.

Kwa tunaomjua Lissu tunaamini kabisa kuwa hawezi kuwa kwenye nafasi kubwa kama Urais kwa sababu kubwa kuwa hayuko settled. Lissu anapaswa kuwa na chombo au mtu wa juu yake kumdhibiti. Lissu ni kama Lema, Wenje na sampuli hizo. Ni waongeaji, wakosoaji na wakitumwa kusemea jambo wana uwezo mkubwa wa kufanya.

Udhaifu wao mkubwa ni kwamba hawawezi kukaa kwenye kikao dakika 20 bila kutoka nje. Wako mbio mbio muda wote. Hawana ubunifu wao ni watekelezaji tu, ni watu wa visasi na makundi, wamekubuhu kwenye fitina hawa wote ndio walimpoteza Lytonga Mrema kwa kumgombanisha na wenzake akina Marando sasa wameshamgombanisha Mbowe na waliokuwa wapenzi wake akina Zitto, Dr. Slaa sasa wanataka Urais.

Dhambi kubwa ya Zitto na Dr Slaa CHADEMA ilikuwa ni kutangaza kugombea Urais. Waliosimamia mkakati wa kuvunja ndoto zao ni hawa vijana wa Lytonga Mrema waliotoka nae NCCR kwenda TLP halafu wakamtelekeza kule na kukimbilia CHADEMA. Kwasababu ni wabaguzi dhambi ile hawajawahi kuiacha ni sawa na kula nyama ya mtu.

Mimi binafsi namuunga mkono Lissu kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa sababu ndio pekee ninayemuona ana ujasiri wa kupambana na Mbowe japo hana mkakati. Simuungi mkono kwa sababu yeye atakuwa mwenyekiti mzuri kuliko Mbowe la hasha ila atavunja mwiko na kufungua mlango uliofungwa miaka mingi wa kupokezana vijiti ndani ya CHADEMA.

Aidha Lissu atatoa changamoto kwa siasa za upinzani nchini na kuzinogesha. Nampa tahadhari Lissu kuwa kama amesharubuniwa na Mbowe kuwa ataachiwa Urais na yeye aachie uenyekiti ameshashindwa kabla ya kuanza.

Kwa sasa Lissu focus kwenye Uenyekiti wa CHADEMA kwanza Urais unakuja tu wenyewe.

Nakutakia uponaji wa haraka Kamanda
Empty Set.
 
Wakati vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 likianza chini kwa chini, Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema yupo tayari kugombea urais ikiwa vyama vya upinzani vitampa ridhaa hiyo.

Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30, Septemba 7 mwaka jana akiwa Dodoma na watu wasiojulikana, amesema hayo jana wakati akizungumza na Mwananchi kuhusu maendeleo ya afya yake.

Mwanasiasa huyo alisema yeye ni mwanachama wa Chadema na hawezi kufanya jambo pasi na kuridhiwa na chama chake au vyama washirika wa Chadema kwani kufanya hivyo ni kinyume cha taratibu na maadili.

Kauli ya Lissu kuhusu kugombea urais mwaka 2020 imetokana na swali aliloulizwa kutokana na kuwa miongoni mwa wanasiasa wa upinzani wanaotajwatajwa, “Wakikaa katika vikao na kunipa bendera, nitakubali kubeba msalaba huo mzito kwa mikono miwili.”

Pia aliulizwa, ikiwa hataombwa na chama atajitosa mwenyewe kuwania nafasi hiyo? Rais huyo wa zamani wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) alisema, “Maadili yangu, unaambiwa ukiwa katika chama lazima upewe fursa kwa hiyo nitasubiri fursa hiyo.”

Katika Uchaguzi Mkuu uliopita wa 2015, vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF vilimsimamisha Edward Lowassa kuwania nafasi ya urais na licha ya kushindwa Dk John Magufuli wa CCM, alipata kura nyingi ambazo hazijawahi kufikiwa na mgombea yeyote wa upinzani.

Katika uchaguzi huo, ilishuhudiwa kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa vyama vingi ulipoanza mwaka 1995, upinzani ukipata kura zaidi ya milioni sita ikiwa ni tofauti ya kura milioni mbili dhidi ya mshindi wa nafasi hiyo.

Lowassa alipata kura milioni 6.01 sawa na asilimia 39.97 huku Dk Magufuli akiibuka mshindi kwa kupata kura milioni 8.9 sawa na asilimia 58.46.

Kuhitimisha matibabu Desemba 31
Kuhusu afya yake, Lissu ambaye ni mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni alisema anatarajia kuanza mwaka akiwa hana vyuma alivyowekewa Julai 9 katika mguu wake wa kulia ili kuunganisha mifupa.

“Desemba 31 nitafanyiwa upasuaji wa mwisho wa kuondoa hii antena ambayo nimekaa nayo kwa miezi sita tangu Julai 9 na nimeelezwa na madaktari kuwa mfupa uliokuwa uunge umeunga na mfupa uliotakiwa kuota unaendelea vizuri,” alisema

Lissu na kuongeza:
“Yaani Jumatatu (Desemba 31) nitahitimisha kazi ya kitabibu na nitaanza mwaka mpya (2019) na mguu mpya ambao hauna chuma.”

Lissu alisema baada ya kuondolewa kwa vyuma, kitakachofuata ni mazoezi ya kutembea na taratibu ataachana na magongo.

Baada ya hapo, Lissu alisema ataanza kuhudhuria vikao mbalimbali ambayo amealikwa katika mataifa ya Ulaya.

Alisema Januari 14 amealikwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) na Umoja wa Ulaya (EU) Brussels, Ubelgiji na Februari mwakani amepata mwaliko wa wiki moja huko Washington Marekani.

“Huko kote nakwenda kuzungumzia kile kilichonitokea Septemba 7 (mwaka jana) lakini kile ambacho kinaendelea nyumbani (Tanzania) na mambo mengine,” alisema.

Kurudi Tanzania badobado kwanza
Alipoulizwa kwamba kuanza wake kusafiri nchi mbalimbali bila shaka ni wakati wake wa kurejea nyumbani, mwanasheria mkuu huyo wa Chadema alisema, “Katikati ya mwakani naweza kurejea. Kuanza mazoezi hakutanizuia kurejea kwani naweza kurudi nyumbani na nikawa nakuja huku (Ubelgiji) kwa madaktari.”

Hata hivyo, Lissu alisema hilo la kurejea nchini litafanikiwa baada ya kufanya mazungumzo na watu mbalimbali ikiwamo viongozi wenzake wa kisiasa pamoja na Serikali.

“Serikali itapaswa kunieleza usalama wangu utakuwaje baada ya kurejea, ingawa jukumu la Serikali ni kulinda raia wake na mimi ni miongoni mwao hasa ukizingatia kile kilichonitokea,” alisema.

Akigusia harakati zake za kupigania demokrasia, Lissu alisema , “Kama nilivyowahi kusema, sitarudi nyuma na mapambano ya kupigania demokrasia si ya wanasiasa pekee, bali makundi mbalimbali kama madaktari, waandishi wa habari, wakulima, wavuvi, bodaboda na wengine.”

Aliunga mkono hatua ya vyama vya Chaumma na ACT- Wazalendo kushirikiana na vyama vya Ukawa vya Chadema, CUF, NLD na NCCR-Mageuzi kutoa tamko la pamoja kuhusu mwaka 2019.

“Umoja ni nguvu utengano ni dhaifu, katika mapambano ya demokrasia kushirikiana ni muhimu zaidi na hicho walichokubaliana mwaka 2019 ni mwaka wa kupigania demokrasia nami nakiunga mkono asilimia 100,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
Waona mbali tulifahamu kuanzia mwanzo kuwa TL alikuwa analenga hivyo. Aliingia CDM akiwa na SP yake ambapo kuna wakati alikuwa anapata wakati mgumu na wenzake[ila hajaonyesha hivyo ili kuongeza ukubalikaji wake kwa uongozi na mwisho wanachama/wananchi. Karume naye alikwishaliona hili na kuna uwezekano wa kiasi fulani naye kwa upande wa Zbar ukasiki anagombea urais. TLS kwa wote hawa imekuwa ni kama njia ya kuwawezesha kufika kule wanapotaka ila kwa bahati mbaya wote wameweka TLS mahala pabaya. Ninasikia kuwa wanasheria wa serikali[ sina uhakika sana] nao wanataka kuanzisha umoja wao.
 
Nimesoma habari ya gazeti la Mwananchi kuhusu swala la Lissu kujiandaa na Urais 2020 hivyo kufanya idadi ya wagombea waliokwisha kutangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya Chadema kinyume kabisa na miongozo ya chama hicho kwa watia nia wake kuwa wawili mpaka sasa yaani Lissu na Lowassa.

Miongozo ya CHADEMA inawataka watia nia wa Urais kutangaza nia hiyo mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi mkuu ili kuepusha mpasuko ndani ya Chama. Aidha yuko Mbowe nae anataka kugombea Urais ila hatangazi ili apate nafasi ya kuwaengua wanaotangaza mapema wakati ukifika.

Kwa tunaomjua Lissu tunaamini kabisa kuwa hawezi kuwa kwenye nafasi kubwa kama Urais kwa sababu kubwa kuwa hayuko settled. Lissu anapaswa kuwa na chombo au mtu wa juu yake kumdhibiti. Lissu ni kama Lema, Wenje na sampuli hizo. Ni waongeaji, wakosoaji na wakitumwa kusemea jambo wana uwezo mkubwa wa kufanya.

Udhaifu wao mkubwa ni kwamba hawawezi kukaa kwenye kikao dakika 20 bila kutoka nje. Wako mbio mbio muda wote. Hawana ubunifu wao ni watekelezaji tu, ni watu wa visasi na makundi, wamekubuhu kwenye fitina hawa wote ndio walimpoteza Lytonga Mrema kwa kumgombanisha na wenzake akina Marando sasa wameshamgombanisha Mbowe na waliokuwa wapenzi wake akina Zitto, Dr. Slaa sasa wanataka Urais.

Dhambi kubwa ya Zitto na Dr Slaa CHADEMA ilikuwa ni kutangaza kugombea Urais. Waliosimamia mkakati wa kuvunja ndoto zao ni hawa vijana wa Lytonga Mrema waliotoka nae NCCR kwenda TLP halafu wakamtelekeza kule na kukimbilia CHADEMA. Kwasababu ni wabaguzi dhambi ile hawajawahi kuiacha ni sawa na kula nyama ya mtu.

Mimi binafsi namuunga mkono Lissu kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa sababu ndio pekee ninayemuona ana ujasiri wa kupambana na Mbowe japo hana mkakati. Simuungi mkono kwa sababu yeye atakuwa mwenyekiti mzuri kuliko Mbowe la hasha ila atavunja mwiko na kufungua mlango uliofungwa miaka mingi wa kupokezana vijiti ndani ya CHADEMA.

Aidha Lissu atatoa changamoto kwa siasa za upinzani nchini na kuzinogesha. Nampa tahadhari Lissu kuwa kama amesharubuniwa na Mbowe kuwa ataachiwa Urais na yeye aachie uenyekiti ameshashindwa kabla ya kuanza.

Kwa sasa Lissu focus kwenye Uenyekiti wa CHADEMA kwanza Urais unakuja tu wenyewe.

Nakutakia uponaji wa haraka Kamanda
Mkuu kama kuna mtu anatakiwa kuwa na mtu juu yake ili kumdhibiti ni JPM, lakini ndo Raisi saivi
 
TLS hakupata fursa ya kuonyesha uwezo au udhaifu wake.
Mkuu, hizo facts ulizoandika hazielezei ubora wa mtu kama kiongozi wa kitaifa ama la. Hizo facts ziko very shallow kulingana na context nzima ya cheo kama cha Uraisi. Raisi bora anapaswa afanye nini, then hayo anayopaswa kuyafanya yalitakiwa yalinganishwe na uwezo wa TAL akipimwa kwa vigezo vya uongozi wake katika siasa na TLS. Mambo uliyoandika ni vijembe vya kwenye taarabu na kwa wasomaji makini tunaona una expose your ignorance
 
Back
Top Bottom