Mshaurini basi kuwa yeye ni mbunge, ni mnadhimu wa bunge kambi ya upinzani, yuko kwenye kamati za bunge, ni waziri kivuli wa sheria, ni kiongozi wa ngazi ya juu wa chama kikuu cha upinzani, ni Rais msaafu wa TLS etc.
Sasa hivi vyeo vyote alivitafuta ima kwa kushawishiwa au kwa utashi wake mwenyewe pengine ilikufikia malengo flani katika kutumikia wananchi na matamanio binafsi.
Ukweli ni huu yote haya yanaenda na wajibu muhimu wa Usalama wa Taifa hili. Kwa vyeo hivyo nilivyo vitaja ziko siri za nchi kazijua kutokana na vyeo hivyo na moja kwa moja siri hizo zinagusa maslahi mapana ya usalama wa taifa hili. Kwa hiyo yeyote anayofanya huko aliko asije akajikuta kageuku kuwa Snowden wa TZ, Kama alitaka majukumu haya ajue pia ana wajibu wa lazima kwa Taifa hili. Asifikiri atatathminiwa kama just anaother personal linapokuja suala la usalama na maslahi ya kiusalama ya Taifa hili. Haiwezekani akakutana na Wazungu hovyohovyo na haijulikani ana trade nini nao wakati inajulikana ziko siri za nchi anazijua kupitia nyadhifa zake hizi. Ushauri huu ni wa bure kwake toka huku kijiweni.