Huyo Lisu kawaida yake kulia lia, kabla ya kugombea urais TLS alipiga kelele sana, akashinda hakuna lililofanyika, yeye ni Makamu mwenyekiti hata haelewi nafasi yake anapaswa kufanya nini, maana hata ukimuuliza yeye kafanya nini tangu ashike hiyo nafasi haelewi, waulize wafuasi wake sasa, utaambulia matusi asubuhi mpaka jioni lakini nao hawana jibu.
Halafu wanakwambia Lisu ni kichwa anapaswa awe mwenyekiti, afanye nini, alichoshindwa kukifanya sasa?
Leo anagombea uwenyekiti chadema anajiona ni malaika aliyeshuka, lakini yeye ndiye huwa anahujumiwa tu kila siku, kila mahala, na keshaanza kulilia anatilia mashaka matokeo hata uchaguzi haujafanyika.
Labda atashinda, sasa ukiwauliza wafuasi wake atafanya nini, eti atakomesha Rushwa za Mbowe, Wakati hata sasa hawana ushahidi wowote wa Mbowe kupokea rushwa, wanasema Abdul na Mama yake, ushahidi hawana.
Lisu anawaburuza lakini watajuata ikitokea bahati mbaya akashinda.
Mini nashauri afukuzwe akishindwa, ili abebe wafuasi wake waende waendako, na wakiweza waanzishe chama chao.