Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Yaani ajenge nchi aache kujenga Chato,?hayo majengo aliyojenga siyo yake binafsi,Hayati Nyerere hakujenga tulimcheka,Hayati Mkapa kazikwa juzi tumesema hakujenga kwao,Kikwete baba wa watu hakuwa na makuu lakini tulisema anazurura sana hadi tukahesabu safari zake humuhumu Jf,Chato hapajajengwa kwa Siri,nasidhani kama Kuna kilichoandikwa jina la Magu huko,wapinzani ni vizuri kujitathmini upyaa,maendeleo aliyoleta Magufuli ni makubwa a mbayo hata 2015 niliyotegemea Lowassa ashinde ayalete Magufuli kamzidi parefu,sisi wenyewe tunajua hata ukitaka kujenga kanyumba kakuishi,lazima ufunge mkanda kidogo,kwa hoja hizi Lisu kushinda ni ngumu,inaonekana hakujipanga vyema yupo too emotional than logical.
Hajaleta maendeleo yoyote acha uongo, watoto bado wanakaa chini hawana madawati, maji hakuna, umeme hakuna.

Ukiona biashara za vitunguu na mbogamboga zinapangwa barabarani bila mpangilio wowote ujue nchi hiyo haina maendeleo.
 
ukikua utayajua ameumiza wengi amesomesha namba wengi zamu yake kuisoma october
Hehee, nikue mara ngapi, kama ulikuwa na vyeti feki, au unapata hela burebure mianya imezibwa, jilaumu mwenyewe.
October ndio chepeo la mwisho kwenye jeneza la chadema, ACT is next
 
Burigi chato ilikuwa ni game reserve yeyet kaipa hadhi kuwa national park na nyingine tano ..... Jamaa ameaim kutanua utalii kwa mikoa ambayo haikuwa na utalii kabisa... Translocating animals sion kwamba ni shida..... Kama mnaijua kitulo national park ilikuwa na ndege na maua tu ila wameintroduce wanyama now...... Jamaa inawezekana akawa hajui hata tuna new parks.

Ni umeme kias gan unatoka kidatu au nyumba ya Mungu.... Na je new hydropower itakuwa na technologia ile ilee ya zamani au ni mpya na umememe umekuwa mwingi zaid.

Kuna hospital mpya ya kanda ya mtwara kubwa kweli. Kuna mrad mkubwa wa maji Arusha

Idadi ya watalii iliongezeka japo aliongeza kodi na nyie cdm mkamtishia watalii hawatakuja kwa kodi kubwa mbona walikuja. Na leo still wanakuna japo dunia inajanga la corona stil wanaiamin Tanzania sababu kuna rais anaethubutu.

Mwambie tundu atuambie ataifanyia nn hii nchi sio kumpaka mtu matope most of the Tanzanians saw what magu did for them wapo weng wanampenda na watamchagua.

Sio kumuita mtu msomi kila mtu ni msomi katika nyanja yake. Mtu kasoma hkl yake dah watu wamepiga nuclear physics huko, watu tumesoma degree ngumu kama veterinary medicine ila tumetulia wala hatuinui mikia.
Hiyo Stigler usiisemee maana haijafikia hata nusu kukamilika, na kwa sababu hatuujui mkataba unasemaje yaweza kuwa kama gas ya Mtwara.

Unaijua CCM au unaisikia tu TBC?
 
haoni reli? haoni madini? haioni dodoma? haoni ndege? haoni vituo vya afya? haoni meli? haoni elimu bite, haioni ubungo? haoni majizi kushughulikiwa? haoni makusanyo yakodi kuongezeka? haoni ccm safi? Nk. Nk. Haoni?

akatafute shughuli nyingine ya kufanya, akaombe hko ulaya ama ajiajiri mahali
Nashukuru hili la uchumi wa kati mmelielewa! Viva JK.
 
Kwamba Chato haipo Tanzania kwa hiyo Magufuli ameenda kujenga uwanja Wa ndege na mbuga ya wanyama katika nchi nyingine kwa kutumia kodi za watanzania.

Mbona maajabu mengi yapo, Lissu hajui kwamba kwenye ikulu ya Dodoma pia kuna mbuga ya wanyama?

Kwa hiyo Lissu anataka kuwaambia nini wananchi Wa Singida?
Yaani unaacha kulipa wastaafu stahiki zao unaenda kujenga uwanja wa ndege Chato, ukiulizwa unasema ipo TZS, una akili au tope?
 
Sasa unataka amkosoe nan? kama si Magufuli anaeiongoza serikali?
seedfarm,

Tundu lisu haijelew na hatopata urais anatakiwa awe na hoja utatusaidia vip kuondokana na umaskin na changamoto zenu lakin inakua kama amepaniki na ana chuki ns uadui wa personal na magu maana analalama tu kila siku magu hiv magu vilee ukisema hajafanya kitu si sahihi hutakiw kua muongo kwamfano nidhamu kazin na matumiz mazur ya pesa za uma sasa kila kitu unapinga pinga tu kama punguani
 
haoni reli? haoni madini? haioni dodoma? haoni ndege? haoni vituo vya afya? haoni meli? haoni elimu bite, haioni ubungo? haoni majizi kushughulikiwa? haoni makusanyo yakodi kuongezeka? haoni ccm safi? Nk. Nk. Haoni?

akatafute shughuli nyingine ya kufanya, akaombe hko ulaya ama ajiajiri mahali
Ni vitu gani vipya alivyofanya Magufuli ambavyo watangulizi wake (Mwl. Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete) hawakuvifanya?
Labda kujenga Chato International Airport na Kubeba wanyama kwenye malori kwenda kuwapandikiza huko kwao Chato ila vingine vilivyobaki ni marudio tu.
 
Alafu kule kibiti wanaambiwa jogoo oyeeee wanaitika oyeeee ha ha ha ha ha ha ha ha ccm bhana
 
Kosa kingine kwa Tundu lissu
Lissu hatakiwi kumshambulia Magufuli
Lissu anatakiwa atuambie atafanya Nini,kukomaa na Magufuli ni sawa na kuzidi kujipunguzia kura tu
Hivi kujenga hospital kubwa 69 sio maajabu
Kukarabati shule za sekondari ambazo haziguswa toka mkoloni si maajabu
Chadema mjipange sana na lissu wenu mtajikuta mmeishiwa maneno baada ya wiki moja tu toka kuanza kampeni
Pamoja na hayo ni lazima pia tupate taarifa sahihi ya mabaya yaliyofanya na serikali hii, kwani kuna ubaya gani kujua mabaya waliyoyanya kwa miaka hii mitano, mbona mazuri tu ndo yanoimbwa kila siku huko TBC, Ninyi ni malaika kwamba hamjafanya mabaya? hata hivyo taarifa ni haki yetu ya kikatiba. Na kama unatarajia kuoa huwa hatu trace taarifa nzuri tu za mchumba ni muhimu kujua kwa undani udhaifu wa mchumba pia ili maamuzi sahihi yafanyike.
 
Kosa kingine kwa Tundu lissu
Lissu hatakiwi kumshambulia Magufuli
Lissu anatakiwa atuambie atafanya Nini,kukomaa na Magufuli ni sawa na kuzidi kujipunguzia kura tu
Hivi kujenga hospital kubwa 69 sio maajabu
Kukarabati shule za sekondari ambazo haziguswa toka mkoloni si maajabu
Chadema mjipange sana na lissu wenu mtajikuta mmeishiwa maneno baada ya wiki moja tu toka kuanza kampeni
Mkuu huwezi ukaanza kutatua tatizo bila kulidefine,kutafuta route cause na mwisho kuja na soln.Ninyi mlioozoea kuambiwa Tanzania itakuwa Kama ulaya in 5 years Kisha mkashangilia bila kuambiwa how and why kwa miaka 60 mmeshindwa ndo mnashindwa kumuelewa Lissu
 
seedfarm,

Tundu lisu haijelew na hatopata urais anatakiwa awe na hoja utatusaidia vip kuondokana na umaskin na changamoto zenu lakin inakua kama amepaniki na ana chuki ns uadui wa personal na magu maana analalama tu kila siku magu hiv magu vilee ukisema hajafanya kitu si sahihi hutakiw kua muongo kwamfano nidhamu kazin na matumiz mazur ya pesa za uma sasa kila kitu unapinga pinga tu kama punguani
Tanzania hii hakuna anayelalamika kila siku kamaMagu na hakuna hata mmoja anyepinga kila kitu kama Magu kama si yeye kupinga kila kitu basi miaka mitano mizima kipato kisingeongezeka dollar 36 tu ili kuufikia uchumi wa kati wakati wenzie walikuwa wanapandisha uchumi kwa zaidi ya dollar mia tatu
 
Lisu kasema ukweli ila Namuomba sana Lisu, aache kuongea vibaya vibaya, awe anaeleza tu mabaya lakini asioneshe maneno makalimakali au kutukana.

Lisu tuko nyuma yako, kura utapata labda ziibiwe kama ilivyozoeleka
Tundu Lissu akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema na wananchi wasio na itikadi ya chama chochote mkoani Dodoma ametoa hoja kali ambazo CCM hawana uwezo wa kuzijibu zaidi ya kupanic na kukimbilia kwenye vyombo vya habari viwahurumie wasirushe mikutano ya Tundu Lissu.

Mosi, amezungumza kuwa jipya na la ajabu kwenye utawala huu ni Rais kujenga uwanja mkubwa Chato wakati marais waliopita hawakufanya maajabu haya, amesisitiza Tundu Lissu.

Pili, ni kitendo cha Rais kupeleka mbuga Chato. Hili ni ajabu kuu ambalo halijawahi kufanyika amesisitiza Tundu Lissu.

Tatu, Lissu amesisitiza kuwa watu wamedhalilishwa, hasa viongozi wa serikali na akina Mama kwa kauli chafu zinazotolewa.

Lissu amesisitiza hii nchi sio kila mtu ni mjinga na unaweza kuwadanganya kirahisi. Kuna watu werevu na wanakwenda kuwaambia wananchi kwa miaka mitano madudu yaliyofanyika.

Je, haya maajabu ni kweli yamefanyika huko Chato?

Je, wakazi wa Lindi, Dodoma, Mbeya, Ruvuma, Arusha, Mtwara, Kilimanjaro mnafahamu maajabu haya ya huko Chato?

Kwa hoja hizi ambazo hata mimi sikuzijua kwa miaka mitano, sasa nimeamshwa usingizini.

Hoja haipigwi rungu, bali hujibiwa kwa hoja. Hii ni kauli ya Dkt Jakaya Kikwete

CCM oyeee oyeeee oyeeee, jibuni hoja hizo!
 
Back
Top Bottom