Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Hajaleta maendeleo yoyote acha uongo, watoto bado wanakaa chini hawana madawati, maji hakuna, umeme hakuna.

Ukiona biashara za vitunguu na mbogamboga zinapangwa barabarani bila mpangilio wowote ujue nchi hiyo haina maendeleo.
 
ukikua utayajua ameumiza wengi amesomesha namba wengi zamu yake kuisoma october
Hehee, nikue mara ngapi, kama ulikuwa na vyeti feki, au unapata hela burebure mianya imezibwa, jilaumu mwenyewe.
October ndio chepeo la mwisho kwenye jeneza la chadema, ACT is next
 
Hiyo Stigler usiisemee maana haijafikia hata nusu kukamilika, na kwa sababu hatuujui mkataba unasemaje yaweza kuwa kama gas ya Mtwara.

Unaijua CCM au unaisikia tu TBC?
 
Nashukuru hili la uchumi wa kati mmelielewa! Viva JK.
 
Yaani unaacha kulipa wastaafu stahiki zao unaenda kujenga uwanja wa ndege Chato, ukiulizwa unasema ipo TZS, una akili au tope?
 
Sasa unataka amkosoe nan? kama si Magufuli anaeiongoza serikali?
 
Ni vitu gani vipya alivyofanya Magufuli ambavyo watangulizi wake (Mwl. Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete) hawakuvifanya?
Labda kujenga Chato International Airport na Kubeba wanyama kwenye malori kwenda kuwapandikiza huko kwao Chato ila vingine vilivyobaki ni marudio tu.
 
Alafu kule kibiti wanaambiwa jogoo oyeeee wanaitika oyeeee ha ha ha ha ha ha ha ha ccm bhana
 
Pamoja na hayo ni lazima pia tupate taarifa sahihi ya mabaya yaliyofanya na serikali hii, kwani kuna ubaya gani kujua mabaya waliyoyanya kwa miaka hii mitano, mbona mazuri tu ndo yanoimbwa kila siku huko TBC, Ninyi ni malaika kwamba hamjafanya mabaya? hata hivyo taarifa ni haki yetu ya kikatiba. Na kama unatarajia kuoa huwa hatu trace taarifa nzuri tu za mchumba ni muhimu kujua kwa undani udhaifu wa mchumba pia ili maamuzi sahihi yafanyike.
 
Mkuu huwezi ukaanza kutatua tatizo bila kulidefine,kutafuta route cause na mwisho kuja na soln.Ninyi mlioozoea kuambiwa Tanzania itakuwa Kama ulaya in 5 years Kisha mkashangilia bila kuambiwa how and why kwa miaka 60 mmeshindwa ndo mnashindwa kumuelewa Lissu
 
Tanzania hii hakuna anayelalamika kila siku kamaMagu na hakuna hata mmoja anyepinga kila kitu kama Magu kama si yeye kupinga kila kitu basi miaka mitano mizima kipato kisingeongezeka dollar 36 tu ili kuufikia uchumi wa kati wakati wenzie walikuwa wanapandisha uchumi kwa zaidi ya dollar mia tatu
 
Lisu kasema ukweli ila Namuomba sana Lisu, aache kuongea vibaya vibaya, awe anaeleza tu mabaya lakini asioneshe maneno makalimakali au kutukana.

Lisu tuko nyuma yako, kura utapata labda ziibiwe kama ilivyozoeleka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…