Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Tumejifunza Rwanda wamejaribu wameweza hao wengine hatuwafatishi na hatuogopi kukosea maana tutakuwa tumejifunza kumbuka kukosea sio kushindwa na hatukati wala hatukatishwi tamaa! we learn from the best...
 
Mbona ameshasema atawafanyia Nini,Tena kaanza kusema juu ya wakulima na wafugaji.Umeiaikiliza vizuri hotuba yake?
Mimi sijaona popote alipomshambulia Magufuli,Bali kaeleza aliyoyafanya Magufuli amabyo Lissu anaona sio sahihi.
Sasa atapataje kura bila Kuonesha aliyepokea madarakani kakosea Nini na yeye atafanya nini? Ndio maana Hakuna namna lazime amtaje.
 
Mkuu huo sio utani jamaa alichoandika ni kweli, nasisitiza si utani.
 
Hakuna nidhamu wala nini, ni kuwa watumishi ni waoga! Nidhamu ya woga, wakiachiwa tu watalipiza kisasi!
Nakubaliana na wewe hajajenga nidhamu makazini,Bali kajenga woga na hofu kwa wafanyakazi.
Nidhamu hujengwa kwa kuweka mazingira rafiki kwa mwajili na mwajiliwa,ili kila upande uone unanufaika na mwenzake.
Mwajili aone mwajiliwa mtu Ni muhimu na mwajiliwa aone mwajili Ni mtu muhimu.
 
Kama hayo kweli ameongea lisu basi miongoni mwa wagombea ambao kichwani ni zero huyu anaongoza. Hiyo mbuga unaihamishaje kutoka sehemu moja kwenda nyengine? Mwambieni azungumzie issues zitakazowatoa wafuasi wake hapo walipo kiuchumi.
 
Na
Kuna haja kubwa kuweka kigezo kinachomtaka mgombea urais awe ametembelea wilaya zote za nchi , hiyo itawasaidia kujua magnitude ya KAZI wanayoiomba. Waingereza wanasema TO SEE IS TO BELIEVE.
 
Siyo u Siyo ubinafsi,hiyo ni rushwa na matumizi mabaya ya Mali ya umma.Unajiuliza huo uwanja wa chato unajengwa ili uhudumie kina nani hasa?Je,ni kipaumbele cha nchi au Jiwe na chato yake?
 
Fatilia viongozi wa mageuzi kina Mohammad rajah Al mahtoom, Putin, J. zemin nk. Hakunaga maendeleo bila kuumia, Kama mwanaume ulitahiriwa Kama mwanamke Alizaa basi hujua hilo!! Chamuhimu malengo ya JPM ni Tanzania yamaendeleo tena yakasi
Maendeleo gani hayo mbona sisi hatuyaoni mnatumia darubini gani kuyazoom hayo maendeleo?

Magu atupishe tuijenje nchi kwa umoja na amani
 
Haya na atawale baada ya Magufuli kumaliza muda wake
 
Mmeanza kumezeshwa maujinga kichwani na tundu? Chato hainahaki kujengwa uwanja wa ndege? Mbona KIA Ipo vijijini? Endeleeni kumskiliza huyo mropokaji asiyeweza kuona mazuri ya wengine.
Bunge lilipitisha?
Je Chato Kuna umuhimu wowote kushinda Mwanza?
Kama uwanja wa Ndege wa DSM umeongezwa kwa Nini wa Mwanza usiongezwe ambao unapokea wageni wengi na kusafirisha wageni wengi zaidi?
Je kwa umbali wa Chato na Mwanza kunahitajika kuwa na viwanja viwili karibukaribu? Yaani wa Mwanza na wa Chato?
 
Kwani hakukuwa na reli? Tazara, reli yaa kati?

Hakuna jipyaa
 
Mukato!!
 
Maendeleo gani hayo mbona sisi hatuyaoni mnatumia darubini gani kuyazoom hayo maendeleo?

Magu atupishe tuijenje nchi kwa umoja na amani
Hivi mnaamini nchi itajengwa na rais Tundu na makamu wake Salumu? Mawaziri ndokina Lema, sugu, esta, haule, nabii shilla. .. Hahahahaaaa haya pambaneni
 
Kwani chato ipo Kenya?
Masikini huelewi lolote,unahitaji kufahamishwa taratibu.

Ni hivi ndugu,viwanja vya ndege Ni gharama,na Kuna Mikoa Haina kabisa viwanja.sasa ilipaswa kwanza kujenga Mikoa ambayo Haina kabisa viwanja.
Sasa Chato iko karibu na Mwanza na iko karibu na Kagera huko kote Kuna viwanja ambavyo sio vya viwango vya Kimataifa.Akina Nyerere waliyaona hayo.
Hivyo ilikua Ni vyema kuviboresha na kuwa viwanja vya Kimataifa Uwanja wa Mwanza amabapo Mwanza Ni jiji linalokua kwa kasi ya kufa Mtu na kuuweka viZuri Uwanja wa Kagera.

Kwa mahitaji ya Uwanja wa ndege Chato haihitaji kabisa.
Hkuna faida yoyote ya kiuchumi kujenga Chato zaidi Ni Ubinafasi tu.
Hata hivyo umejengwa bila baraka za bunge hi sio kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…