Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Ndege zinazeeka na hivyo zitahitaji vipuri ambavyo ni bei sana ( pengine hujui: vipuri vya ndege vina expire date.)

Mashirika makubwa yanafungwa kwa kushindwa hii biashara. Kujaribu si kubaya lakini kujaribu tu ili mradi uonekane umejaribu ni jambo la ajabu kabisa.
Tumejifunza Rwanda wamejaribu wameweza hao wengine hatuwafatishi na hatuogopi kukosea maana tutakuwa tumejifunza kumbuka kukosea sio kushindwa na hatukati wala hatukatishwi tamaa! we learn from the best...
 
Kosa kingine kwa Tundu lissu
Lissu hatakiwi kumshambulia Magufuli
Lissu anatakiwa atuambie atafanya Nini,kukomaa na Magufuli ni sawa na kuzidi kujipunguzia kura tu
Hivi kujenga hospital kubwa 69 sio maajabu
Kukarabati shule za sekondari ambazo haziguswa toka mkoloni si maajabu
Chadema mjipange sana na lissu wenu mtajikuta mmeishiwa maneno baada ya wiki moja tu toka kuanza kampeni
Mbona ameshasema atawafanyia Nini,Tena kaanza kusema juu ya wakulima na wafugaji.Umeiaikiliza vizuri hotuba yake?
Mimi sijaona popote alipomshambulia Magufuli,Bali kaeleza aliyoyafanya Magufuli amabyo Lissu anaona sio sahihi.
Sasa atapataje kura bila Kuonesha aliyepokea madarakani kakosea Nini na yeye atafanya nini? Ndio maana Hakuna namna lazime amtaje.
 
Unataka kutuambia Marais wote walio pita hawakuwahi kununua ndege? Wakati kuna walio nunua tukala majani?

Kwamba shule hazikuwepo? Mimi nilisoma Uarabuni?

Kwamba hosipitali hazikuwepo tulitibiwa wapi? Hebu tuache utani kwenye mambobya msingi jamani.
Mkuu huo sio utani jamaa alichoandika ni kweli, nasisitiza si utani.
 
Hakuna nidhamu wala nini, ni kuwa watumishi ni waoga! Nidhamu ya woga, wakiachiwa tu watalipiza kisasi!
Nakubaliana na wewe hajajenga nidhamu makazini,Bali kajenga woga na hofu kwa wafanyakazi.
Nidhamu hujengwa kwa kuweka mazingira rafiki kwa mwajili na mwajiliwa,ili kila upande uone unanufaika na mwenzake.
Mwajili aone mwajiliwa mtu Ni muhimu na mwajiliwa aone mwajili Ni mtu muhimu.
 
Tundu Lissu akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema na wananchi wasio na itikadi ya chama chochote mkoani Dodoma ametoa hoja kali ambazo CCM hawana uwezo wa kuzijibu zaidi ya kupanic na kukimbilia kwenye vyombo vya habari viwahurumie wasirushe mikutano ya Tundu Lissu.

Mosi, amezungumza kuwa jipya na la ajabu kwenye utawala huu ni Rais kujenga uwanja mkubwa Chato wakati marais waliopita hawakufanya maajabu haya, amesisitiza Tundu Lissu.

Pili, ni kitendo cha Rais kupeleka mbuga Chato. Hili ni ajabu kuu ambalo halijawahi kufanyika amesisitiza Tundu Lissu.

Tatu, Lissu amesisitiza kuwa watu wamedhalilishwa, hasa viongozi wa serikali na akina Mama kwa kauli chafu zinazotolewa.

Lissu amesisitiza hii nchi sio kila mtu ni mjinga na unaweza kuwadanganya kirahisi. Kuna watu werevu na wanakwenda kuwaambia wananchi kwa miaka mitano madudu yaliyofanyika.

Je, haya maajabu ni kweli yamefanyika huko Chato?

Je,wakazi wa Lindi, Dodoma, Mbeya, Ruvuma, Arusha, Mtwara, Kilimanjaro mnafahamu maajabu haya ya huko Chato?

Kwa hoja hizi ambazo hata mimi sikuzijua kwa miaka mitano, sasa nimeamshwa usingizini.

Hoja haipigwi rungu, bali hujibiwa kwa hoja. Hii ni kauli ya Dkt Jakaya Kikwete

CCM oyeee oyeeee oyeeee, jibuni hoja hizo!
Kama hayo kweli ameongea lisu basi miongoni mwa wagombea ambao kichwani ni zero huyu anaongoza. Hiyo mbuga unaihamishaje kutoka sehemu moja kwenda nyengine? Mwambieni azungumzie issues zitakazowatoa wafuasi wake hapo walipo kiuchumi.
 
Na
haoni reli? haoni madini? haioni dodoma? haoni ndege? haoni vituo vya afya? haoni meli? haoni elimu bite, haioni ubungo? haoni majizi kushughulikiwa? haoni makusanyo yakodi kuongezeka? haoni ccm safi? Nk. Nk. Haoni??
akatafute shughuli nyingine ya kufanya, akaombe hko ulaya ama ajiajiri mahali
Kuna haja kubwa kuweka kigezo kinachomtaka mgombea urais awe ametembelea wilaya zote za nchi , hiyo itawasaidia kujua magnitude ya KAZI wanayoiomba. Waingereza wanasema TO SEE IS TO BELIEVE.
 
Siyo u
Kosa kubwa la Magufuli ameenda Chato ndani kujenga uwanja mkubwa wa ndege huku akijua kuwa hauna faida yoyote zaidi ya hasara. Yani ni kama kwa mfano Tundu Lissu awe Rais kisha akajenge uwanja mkubwa wa ndege Ikungi.

Ukiwa unaenda Chato unaupita mji mkubwa wa Geita kisha unaenda mji mdogo wa Katoro then Chato. Yani sijui alitumia findings zipi kujenga huko Chato! Sijui!

Yani ni kama marehemu Mkapa airuke Mtwara mjini, airuke Masasi mjini kisha aende Lupaso akajenge uwanja mkubwa wa ndege. Huu ni ujinga wa aina yake.
Siyo ubinafsi,hiyo ni rushwa na matumizi mabaya ya Mali ya umma.Unajiuliza huo uwanja wa chato unajengwa ili uhudumie kina nani hasa?Je,ni kipaumbele cha nchi au Jiwe na chato yake?
 
Fatilia viongozi wa mageuzi kina Mohammad rajah Al mahtoom, Putin, J. zemin nk. Hakunaga maendeleo bila kuumia, Kama mwanaume ulitahiriwa Kama mwanamke Alizaa basi hujua hilo!! Chamuhimu malengo ya JPM ni Tanzania yamaendeleo tena yakasi
Maendeleo gani hayo mbona sisi hatuyaoni mnatumia darubini gani kuyazoom hayo maendeleo?

Magu atupishe tuijenje nchi kwa umoja na amani
 
Kwa hoja Lissu is the Best.

Kiutendaji Magufuli amejaa ubinafsi na kupenda kuabudiwa kiasi amekaa kimya alipofananishwa na Masihi Wa Bwana.. Ameshindwa kuleta Umoja Wa Kitaifa kwa kupendelea Kanda yake zaidi.

Lissu utendaji wake kwenye sheria sote tumeona jinsi anavyotetea wanyonge dhidi ya sheria kandamizi za Serikali ya Magufuli.

Bora Lissu.
Haya na atawale baada ya Magufuli kumaliza muda wake
 
Mmeanza kumezeshwa maujinga kichwani na tundu? Chato hainahaki kujengwa uwanja wa ndege? Mbona KIA Ipo vijijini? Endeleeni kumskiliza huyo mropokaji asiyeweza kuona mazuri ya wengine.
Bunge lilipitisha?
Je Chato Kuna umuhimu wowote kushinda Mwanza?
Kama uwanja wa Ndege wa DSM umeongezwa kwa Nini wa Mwanza usiongezwe ambao unapokea wageni wengi na kusafirisha wageni wengi zaidi?
Je kwa umbali wa Chato na Mwanza kunahitajika kuwa na viwanja viwili karibukaribu? Yaani wa Mwanza na wa Chato?
 
haoni reli? haoni madini? haioni dodoma? haoni ndege? haoni vituo vya afya? haoni meli? haoni elimu bite, haioni ubungo? haoni majizi kushughulikiwa? haoni makusanyo yakodi kuongezeka? haoni ccm safi? Nk. Nk. Haoni??
akatafute shughuli nyingine ya kufanya, akaombe hko ulaya ama ajiajiri mahali
Kwani hakukuwa na reli? Tazara, reli yaa kati?

Hakuna jipyaa
 
Ati huyu.. anataka kuongoza nchi hii!!!.. mipasho mipasho ipo kwa damu yake. Yeye anataka kuongoza.. ili akae Ikulu.. kupiga mipasho kwa Mh. Magufuli.. anaonyesha ana wivu sana na mafanikio ya Magufuli.. wivu mubaya sana.. nyie munao mushangilia humu.. ni basi tu hamuwezi badili gia angani.. humu ila rohoni kura kwa Magufuli.. tumewazoea.. 2010.. 2015.. 😃😃😃 si mukubali kwamba anawatia aibu.. nyie wafuasi wapenda maisha ya mukato.. aliyoziba Rais wenu mpendwa JPM.. yaani hana hata sera.. akiwongea ni upupwu tu anashusha.. BTW akimaliza mazoezi tarehe 27 Okitoba 2020.. atakwenda shangilia kumaliza ndoto ya kupiga michapo.. tumbo tu mbele.. tamaa ya kupenda kutawaliwa na mabeberu.

Magufuli 2020💯
Mukato!!
 
Maendeleo gani hayo mbona sisi hatuyaoni mnatumia darubini gani kuyazoom hayo maendeleo?

Magu atupishe tuijenje nchi kwa umoja na amani
Hivi mnaamini nchi itajengwa na rais Tundu na makamu wake Salumu? Mawaziri ndokina Lema, sugu, esta, haule, nabii shilla. .. Hahahahaaaa haya pambaneni
 
Kwani chato ipo Kenya?
Masikini huelewi lolote,unahitaji kufahamishwa taratibu.

Ni hivi ndugu,viwanja vya ndege Ni gharama,na Kuna Mikoa Haina kabisa viwanja.sasa ilipaswa kwanza kujenga Mikoa ambayo Haina kabisa viwanja.
Sasa Chato iko karibu na Mwanza na iko karibu na Kagera huko kote Kuna viwanja ambavyo sio vya viwango vya Kimataifa.Akina Nyerere waliyaona hayo.
Hivyo ilikua Ni vyema kuviboresha na kuwa viwanja vya Kimataifa Uwanja wa Mwanza amabapo Mwanza Ni jiji linalokua kwa kasi ya kufa Mtu na kuuweka viZuri Uwanja wa Kagera.

Kwa mahitaji ya Uwanja wa ndege Chato haihitaji kabisa.
Hkuna faida yoyote ya kiuchumi kujenga Chato zaidi Ni Ubinafasi tu.
Hata hivyo umejengwa bila baraka za bunge hi sio kawaida.
 
Back
Top Bottom