Tundu Lissu akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema na Wananchi wasio na itikadi ya chama chochote mkoani Dodoma ametoa hoja kali ambazo CCM hawana uwezo wa kuzijibu zaidi ya kupanic na kukimbilia kwenye vyombo vya habari viwahurumie wasirushe mikutano ya Tundu Lissu.
Mosi, amezungumza kuwa jipya na la ajabu kwenye utawala huu ni Rais kujenga uwanja mkubwa Chato wakati marais waliopita hawakufanya maajabu haya, amesisitiza Tundu Lissu.
Pili, ni kitendo cha Rais kupeleka mbuga Chato. Hili ni ajabu kuu ambalo halijawahi kufanyika amesisitiza Tundu Lissu.
Tatu, Lissu amesisitiza kuwa watu wamedhalilishwa, hasa viongozi wa serikali na akina Mama kwa kauli chafu zinazotolewa.
Lissu amesisitiza hii nchi sio kila mtu ni mjinga na unaweza kuwadanganya kirahisi. Kuna watu werevu na wanakwenda kuwaambia wananchi kwa miaka mitano madudu yaliyofanyika.
Je, haya maajabu ni kweli yamefanyika huko Chato?
Je, wakazi wa Lindi, Dodoma, Mbeya, Ruvuma, Arusha, Mtwara, Kilimanjaro mnafahamu maajabu haya ya huko Chato?
Kwa hoja hizi ambazo hata mimi sikuzijua kwa miaka mitano, sasa nimeamshwa usingizini.
Hoja haipigwi rungu, bali hujibiwa kwa hoja. Hii ni kauli ya Dkt Jakaya Kikwete
CCM oyeee oyeeee oyeeee, jibuni hoja hizo!
Ndugu Mbegu ya shambani, Tundu Lissu ni kweli watu wote sio wajinga, kwa hivyo naye TL ajue ni hivyo sie sio wajinga. Tokea amekuja na kuchaguliwa kupeperusha Bendera ys Chadema, hakuna Jipya alilokuja nalo, ila ni lile lile la kumshutumu na kumuandama Magufuli.
TL kama anajiona ni mbadala wa Rais Magufuli, atupe kisomo cha atakacho tufanyia tofauti na Magufuli, Maendeleo gani katuletea, Amezunguka Ulaya na USA, lipi lenye manufaa kwa wananchi alilolipata, zaidi ya kufuatilia ya Magufuli.
Pia ajue kuwa yeye ndiye aliyeamshwa kutoka usingingizini, sie tuko macho, tumeyaona mazuri na mabaya aliyoyafanya Magufuli, yeye alikuwa ughaibuni, sisi tumeyaishi.
Hapa hakuna hoja, bali kuna malalamiko na kilio. WATANZANIA WENGI WANOGOPA MWENDO WA LISSU ULIVYO, ANAONYESHA KUJIWEKEZA ZAIDI KWENY KULIPIZA KISASI, ZAIDI YA KUWALETEA WALALA HOI MAENDELEO.