Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Akizungumzia hali ya uungwaji mkono na Wananchi baada ya kuwasusia maandamano ambayo yamekuwa yakiitishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
"Watu wameenda wapi?, mwaka 2011 (Arusha) kulikuwa na maandamano ya CHADEMA kupinga yaliyokuwa yametokea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2010, maandamano yale yalipigwa marufuku na jeshi la polisi lakini viongozi wa chama na wanachama wetu, wafuasi na wananchi wa Arusha walijitokeza kwa maelfu na walisambaratishwa kwa ukatili mkubwa sana, walipigwa mabomu, watu waliuawa na tukakatazwa kwenda kufanya shughuli ya mazishi tukalazimisha kwa nguvu ya umma kwenda kufanya mazishi kwa wale waliokuwa wameuawa..."
"Mwaka 2012/13 tukapigwa mabomu uwanja wa Soweto Arusha pale pale kwa maandamano kama hayo, tulifanya maandamano Morogoro muuza magazeti anaitwa Arizona akauawa na polisi lakini tukalazimisha tukafanya mkutano kwasababu wananchi walikuwa wanatuunga mkono..swali ni wameenda wapi?, kwanini wananchi hawatusikilizi tena?, shida yetu ni nini?, tumewakosea nini wananchi wale waliokuwa tayari kutufia! Sasa hivi Mwenyekiti anaitisha maandamano anaenda yeye na binti yake...." mimi naamini kuna mambo tumefanya tumewakosea imani .
Pia, Soma:
- Mwenyekiti wa CHADEMA, Songwe: Tumekaa tumeona tusimame na Tundu Lissu na siyo kama tunampuuza Mbowe
- Freeman Mbowe: Shutma za Lissu dhidi yangu ni za uongo