Tundu Lissu: Siku zote kupoteza mtu 'Calibre' ya Dkt. Slaa ni hasara. Agoma kujibu kama Mbowe anatosha nafasi ya uenyekiti

Ngoja waje wakereketwa wa Chadema Lissu anazidi kumwaga mboga taratibu taratibu maana wanazi walimwita Slaa mla mihogo na kusema Chadema ni kubwa kuliko Slaa
 
Siku zote nimekua na heshima ya kipekee kwa Dr. Slaa, pamoja na kuzingua sana na kuendelea kuzingua, bado wengi tulijizuia kumjadili sababu ya kazi mzuri aliyokwishaifanya
 
Asante kwa mawazo yako.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]kwamba hao waandishi wanatumwa na Ccm?
Simaanishi CCM wanatuma waandishi, nachomaanisha, majibu anayotoa Lissu kwenye maswali anayoulizwa, jamaa wako pembeni kutafuta "gap" walitumie kuingiza ajenda zao kwa manufaa ya chama chao, awe makini.
 
Simaanishi CCM wanatuma waandishi, nachomaanisha, majibu anayotoa Lissu kwenye maswali anayoulizwa, jamaa wako pembeni kutafuta gap walitumie kuingiza ajenda zao kwa manufaa ya chama chao.
Sawa
 
Hadi leo huwa sioni kosa la DK.Slaa

Ila kwavle tunasiasa maji taka ambazo wakubwa ndio wanaamua nani aonekane mzuri na nani aonekane mbaya ndio DK.Slaa akafanywa aonekane mbaya.

Ila mtu kusimamia lile analoliamini sioni ubaya wake na yeye ndio alikuwa sahihi kabsaa kuliko viongozi waliobadili gia angani.

Viongozi wa Chadema walipaswa waombe msamaha kwa uongo waliousema juu ya Lowasa kwa watanzania ingewatofautisha sana na vyama vingine lakini matokeo yake wanafanana tu.

Siasa za uongo uongo ndio zinaonekana za maana kuliko za kusimamia jambo unaloliamini ndio zinaonekana za usaliti.
 
Dr. Slaa alishiriki mchakato wa kumkubali Lowassa kuja kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CDM, CCM kwa kujua adhari za Lowassa kisiasa ikaamua kuharibu mambo wakapitia kwa mchumba wa Dr. Slaa na kumwaga sumu kali huku fedha na ahadi za vyeo zikitawala.
Sasa Baada ya mchumba kuonjeshwa asali DR. akafichwa ndani kwa siku kadhaa...... Alipoibuka akaandaliwa press - yeye akaiita ni Press ya kuisimamisha nchi. Baada ya siku chache Mzee mwingine wa CUF na yeye akasema nafsi inamsuta akajiongoka UKAWA.
Kibaya kwake nchi haikusimama, na kiuhalisia kabisa Lowassa alishinda Urais, na kwa leo hao wazee wawili wanaishi huku nafsi zao zikiwasuta.
 
Simaanishi CCM wanatuma waandishi, nachomaanisha, majibu anayotoa Lissu kwenye maswali anayoulizwa, jamaa wako pembeni kutafuta "gap" walitumie kuingiza ajenda zao kwa manufaa ya chama chao, awe makini.

Nimesikiliza interview yote.

muuliza maswali bwana Lambert ameuliza maswali mengi na mazuri.

Lissu naye amejibu maswali hayo kwa kirefu na kwa ufasaha.

Swali lililoni-impress kuliko yote ni kuhusu msimamo wa Lissu kuhusu vita vya Ukraine.

Sikutarajia Lissu awe na ufahamu wa historia ya Urusi mpaka enzi za Napoleon.
 
Mimi siamini katika watu wazuri kwa maslahi ya chama.
Naamini watu wazuri kwa maslahi ya nchi.
Vyama vinapita lakini nchi itabaki.
Mtu akiwa na uwezo hata kama yupo CHAUMA au DP au CHADEMA, kwa nini asitumike kwa maslahi ya nchi!!??
Yaani ni tatizo kubwa sana mtu kama Lissu kutomtumia kwa manufaa makubwa ya nchi,eti kisa tu ni CHADEMA.
 
Hajagoma kujibu swali bali ni wewe ndiye uliyegoma kuelewa ......!!
 
Labda Lissu anaweza kutufahamisha Dr Slaa aliondokaje kwenda Canada na baadae akaibukia Ubalozi
 
Duuuh, that feels like long time ago! Tumeona mengi miaka ya hivi karibuni!
 
Lissu hakuweka wazi hiyo sababu halisi ya Dr. Slaa kuondoka Chadema ila sisi huku tunabwatuka tu, wanasiasa huwa wanatuchora sana tunapokuwa tunajadili vitu tusivyovielewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…