..Mwalimu aliwafukuza wafanyabiashara wakubwa na kutaifisha viwanda, mabenki, etc.
..watu hawakuondoka kwa hiari yao, walinyang'anywa mali na biashara zao.
..hatua hizo za utaifishaji za Mwalimu Nyerere zilisababisha zao kama la mkonge kuporomoka.
..zao hilo liliporomoka kwasababu Mwalimu Nyerere hakuwa na watu wenye ujuzi na uzoefu wa kuendesha mashamba, viwanda, na biashara ya mkonge.
..Na kipindi hicho Tanzania tulikuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa mkonge duniani.
..Mwalimu pia alianzisha mfumo wa vijiji vya ujamaa na mpango huo ulitiliwa mkazo mkubwa maeneo ya kusini mwa Tanzania.
..wananchi walikuwa wanahamishwa toka maeneo waliyoishi kwa muda mrefu, na kupelekwa maeneo mapya ya vijiji vya ujamaa.
..wakati wa zoezi hilo wako wananchi wengi waliacha mashamba yao ni kwenda maeneo mapya. mpango wa vijiji vya ujamaa ulisababisha kilimo kuathirika sana mikoa ya kusini na kupelekea zao la korosho kuporomoka.
..kuna viwanda vilikuwa vinafanya vizuri kabla ya zoezi la utaifishaji lakini navyo viliporomoka kwasababu walioteuliwa kuviongoza walikuwa hawana ujuzi wala uzoefu ktk kuendesha viwanda hivyo.
..Mwalimu hakutakiwa kutaifisha mali za watu, alichotakiwa kufanya ni kuanzisha makampuni ya serikali/umma yafanye kazi bega kwa bega na makampuni ya watu binafsi.
..Ni lazima tuwe wakweli kuhusu nini kilisababisha uchumi wetu ukaporomoka wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.
NB:
..kipindi chote cha utawala wa Mwalimu Nyerere isipokuwa kipindi kifupi cha mwaka 1980--84 Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi zilizokuwa zikipokea misaada mingi zaidi kutoka nchi za magharibi.
Tunakubaliana kwamba ujamaa + kukosa ujuzi na maarifa ni kuleta majanga.
Tusichokubaliana (pengine ni mimi au wewe kutokuwa na stori kamilifu) ni sababu zilizosababisha wazungu kuondoka.
Kama nakumbuka vizuri hotuba/mahojiano na Nyerere kabla na baada ya uhuru, ilikuwa Nyerere analazimisha weusi kwa wazungu waishi kama raia wa nchi moja chini ya sheria moja na usawa mmoja.
Wazungu walizoea kuishi kama first class citizens -- kibao kugeuka na kuambiwa lazima waanze kusimamiwa na kulipa kodi inayokusanywa na waliokuwa third class citizen (second class walikuwa waasia), hii haikuwakaa vyema.
Kuambiwa kwamba mashule wanayoyasimamia wao hata mtoto wa aliyekuwa Mnyapara anapaswa asome, hii haikuwakaa vyema.
Ndicho hasa kilichomsukuma Nyerere aanzishe Azimio la Arusha.
Alitaka kuona nchi inakua bila kumuacha mtu yeyote nyuma.
Asikwambie mtu, Tanzania inaweza kuwa kwenye mahesabu ya kiuchumi iliachwa nyuma kwa siasa za Nyerere, lakini ni siasa hizo hizo zilizofanya nchi yetu kila mmoja ana fursa sawa, hata leo hii.
Tungeedelea na utaratibu wa awali tungekuwa kama style ya South Africa leo. Una utajiri wa kutupwa na umaskini wa kutupwa ndani ya nchi moja. Cha kushangaza matajiri ni watu wa rangi moja na maskini ni watu wa rangi nyingine.
Si kila kingaacho ni dhahabu, Tanzania ina nafuu sana kwa utaratibu wetu huu wa sasa, na tunaweza kusonga mbele kwa pamoja bila mtu kuachwa nyuma.