Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Tanzania haiwezi kuishi bila dunia ila dunia inaweza kuishi bila Tanzania


Wameadvance kwasababu wamesimamia misingi yao ya kujitegemea na kujiweka mbali na ubepali.
 
Tunakubaliana kwamba ujamaa + kukosa ujuzi na maarifa ni kuleta majanga.

Tusichokubaliana (pengine ni mimi au wewe kutokuwa na stori kamilifu) ni sababu zilizosababisha wazungu kuondoka.

Kama nakumbuka vizuri hotuba/mahojiano na Nyerere kabla na baada ya uhuru, ilikuwa Nyerere analazimisha weusi kwa wazungu waishi kama raia wa nchi moja chini ya sheria moja na usawa mmoja.

Wazungu walizoea kuishi kama first class citizens -- kibao kugeuka na kuambiwa lazima waanze kusimamiwa na kulipa kodi inayokusanywa na waliokuwa third class citizen (second class walikuwa waasia), hii haikuwakaa vyema.

Kuambiwa kwamba mashule wanayoyasimamia wao hata mtoto wa aliyekuwa Mnyapara anapaswa asome, hii haikuwakaa vyema.

Ndicho hasa kilichomsukuma Nyerere aanzishe Azimio la Arusha.

Alitaka kuona nchi inakua bila kumuacha mtu yeyote nyuma.

Asikwambie mtu, Tanzania inaweza kuwa kwenye mahesabu ya kiuchumi iliachwa nyuma kwa siasa za Nyerere, lakini ni siasa hizo hizo zilizofanya nchi yetu kila mmoja ana fursa sawa, hata leo hii.

Tungeedelea na utaratibu wa awali tungekuwa kama style ya South Africa leo. Una utajiri wa kutupwa na umaskini wa kutupwa ndani ya nchi moja. Cha kushangaza matajiri ni watu wa rangi moja na maskini ni watu wa rangi nyingine.

Si kila kingaacho ni dhahabu, Tanzania ina nafuu sana kwa utaratibu wetu huu wa sasa, na tunaweza kusonga mbele kwa pamoja bila mtu kuachwa nyuma.
 
Kuna mtu anataka kuishi bila majirani..kwamba yeye na familia yake ati wanajiweza...wakati 80% ya wanafamilia hao wanakula nusu mlo kwa siku, yaani kipato cha kaya dola 2 hadi 3 kwa siku.
Kwahiyo unataka waende wakavizie vyakula vya majirani?

Fanya kazi kwa juhudi upate vya kwako.
 
Fikra muhimu kama hizi msiishie kusema mtandaoni tu, mseme hata huko nyumbani, mtaani hata sehemu za kazi. Zikiishia mtandaoni kumbuka kuna watu simu janja hawana.
 
Wale watu wanaakili hilo ulijue tofauti na huku porini tunako ishi mbona huyo muungu wenu wa chato kasema yy ataifanya Tanzania kama ulaya

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Wale genetically born Wana akili, Sasa we linganisha na watu wako hata kutengeneza choo hawaeezi wanajisaidia porini Kama ngedere,
Sisi bado Sana ku catch up na dunia inabidi tusaidiwe Kwanza Kuna generation zitakuja kustaarabika baadaye
Mkuu umeuwa nzi kwa nyundo.
 
Wale genetically born Wana akili, Sasa we linganisha na watu wako hata kutengeneza choo hawaeezi wanajisaidia porini Kama ngedere,
Sisi bado Sana ku catch up na dunia inabidi tusaidiwe Kwanza Kuna generation zitakuja kustaarabika baadaye
- Wewe mpaka sasa bado hujastarabika.
- Wewe ni muoga huna fikra za kujiamini kwanza ili ufanikiwe.
 
Wale genetically born Wana akili, Sasa we linganisha na watu wako hata kutengeneza choo hawaeezi wanajisaidia porini Kama ngedere,
Sisi bado Sana ku catch up na dunia inabidi tusaidiwe Kwanza Kuna generation zitakuja kustaarabika baadaye
Acha uzwazwa, shida kwakiwango kikubwa ndizo zinaleta ubunifu. Huwezi buni kitu ambacho kipo.
 
Kwa anko Magu kujitenga ametengeneza hata kimpumu?
Usitufananishe TZ na wavuta bangi wa Korea ama Cuba hizo chapa hatuwezi kufanana nazo hivyo tusijitenge na dunia tutaumia Sana
 
Dogo baba ako, afu tuendelee :-

Utafiti upi unaozungumzia?, kama ndio huo utafiti wa kizungu kukuaminisha wewe ni inferior kwa kila kitu huo ni ujinga wako.
School boy!
Mfano rahisi Ni mambo wanayofanya viongozi wa ccm yanadhibitisha na kudhibitisha uduni wa akili ya mtu mweusi
Kwa mujibu wa tafiti

Bisha nikupe mifano
 
We mwenyewe unasema Korea kasikazini inashirikiana na Urusi, China afu unataka ufananishe na alichokisema TL, Hata hivyo hukuona Pamoja kwamba USA na Korea kaskazini uhusiano wao sio mzri lakini viongozi wao wakuu walishahi kukutana ili kuiweka diplomasia mbele badala ya ubabe tu.
 

..Azimio la Arusha lina component mbili ambazo ni maadili ya viongozi, na siasa ya ujamaa na kujitegemea.

..kwa uelewa wangu halikuhusisha masuala ya mashule yaliyokuwa yakipokea watoto wa kizungu na kiasia, pia halikuhusisha masuala ya nafasi za kiutawala kuchukuliwa na waafrika.

..ukisoma literature mbalimbali za azimio la arusha utaona sehemu ambapo linazungumzia ukosefu wa maadili miongoni mwa waafrika waliopewa nafasi za uongozi ambapo inadaiwa kuliibuka tabaka la "wabenzi," kwa maana ya waafrika walioanza kuendesha magari ya mercedes benz.

..baada ya uhuru kulikuwa na program inaitwa AFRICANIZATION, hii ilikuwa ni program ya kuwapandisha madaraja watumishi wa serikali wa kiafrika ili washike nafasi za madaraka na maamuvi ktk civil service, na taasisi nyingine kama polisi na jeshini.

..Actually habari za chinichini zinasema Mwalimu hakuwa muumini mkubwa wa Africanization. Inasemekana radicals kama Mzee Kawawa ndio waliokuwa mstari wa mbele kuutekeleza bila kuyumba mpango wa Africanization.

..sasa wazalendo waliopata nafasi kupitia program ya Africanization ndiyo walianza kuishi kibwanyenye ndio walikuwa walengwa wa component ya maadili ya viongozi ktk azimio la arusha.

..Mimi kwa maoni yangu Azimio la Arusha ndiyo limesababisha wazawa tuwe nyuma kiuchumi. Azimio liliwatisha wazawa na kuwakatisha tamaa kujiingiza ktk biashara kubwa, ukulima mkubwa, na ujasiriamali. Entrepreneurial spirit ya taifa letu ilikufa kabisa kutokana na azimio la arusha. Pia limesababisha waTz tuwe na wivu na tuchukie matajiri hata waliopata utajiri kwa njia za halali. Watanzania tumekuwa na tabia ya "bora tukose wote."
 
Ni sahihi pia kusema Lissu hauwezi kuishi bila Robert Amsterdam & Partners LLP
 
Nakubali kwamba huo ubwanyenye uliojitokeza katika azimio la Arusha ndicho miongoni mwa vile ninavyoviita "watu wetu kutokuwa na elimu na maarifa" ya kutuongoza katika uchumi shindani. Uchina na Urusi ya wakati ule kuna mijitu ilikuwa imeshiba kimaarifa na ujamaa wao ulienda sambamba na weledi. Kuna tofauti kubwa kati ya meneja wa kiwanda cha serikali anayeongoza kwa kufuata weledi na kanuni za ushindani wa kibiashara kwa ajili ya maslahi ya umma, na meneja wa kiwanda cha serikali asiye na maarifa wala weledi wala ubunifu wowote.

Watu wenye sifa hizo walikuwepo, ni wazungu, lakini hawakuamini au kukubali katika kujitoa sadaka ya ujamaa kwa ajili eti ya nchi ya watu weusi.

Suala kwamba tuengeendelea na siasa hizo tungekuwa mbali kiuchumi....may be!

But kwa gharama kubwa sana, maana kuna mikoa na watu ingekuwa ndoto kutoboa. Usiende mbali chukulia mfano South Africa.

Nakwambia hiyo nchi ni nchi mbili maskini na tajiri ndani ya nchi moja, na ubaguzi uliokithiri kunakosababishwa na pengo la walio nacho na wasio nacho. Ujamaa sio mbaya kivile, ni namna mnavyouendesha.


So
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…