Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Tanzania haiwezi kuishi bila dunia ila dunia inaweza kuishi bila Tanzania



..unajua wakati wa utawala wa muingereza kulikuwa na sheria zinazowabana wazawa wasijihusishe na biashara au ujasiriamali.

..kwa mfano, kulikuwa na masharti magumu kwa wazawa kupata mikopo ukilinganisha na waasia au wazungu.

..sasa tulipopata uhuru ilitakiwa wazawa wapate ahueni ktk kupata mikopo, ku-accumulate mitaji, na kufanya biashara kubwa.

..bahati mbaya ni kwamba mwaka 1967 azimio la arusha likaanzishwa na kufunga milango ya opportunities za kimitaji na kibiashara kwa wazawa.

..mwaka 1984/85/86 milango ya biashara ilipokuja kufunguliwa wazawa walikuwa wameshadumaa. ndugu zetu wa kiasia waliweza ku-pick up faster kwasababu shughuli za biashara zipo ktk familia zao for two or even three generations. pia wao walibakiwa na mitaji yao ingawa haikuwa mikubwa.

..milango ya biashara ilipofunguliwa wazawa tulikuwa kama tumeshtukizwa tusijue nini cha kufanya kutokana na jinsi tulivyokuwa tumebanwa na azimio la arusha.

..mfanyabiashara kama Mo Dewji ameendeleza mali za baba na babu yake. Aliko Dangote ametokea familia ya wafanyabiashara, ambapo babu yake alikuwa mfanyabiashara mkubwa. kwa hapa Tanzania mzawa kama Mzee Mengi, Ali Mufuruki, etc biashara zao zilikuwa ni first generation.

..Azimio la Arusha limechelewesha wazawa kuingia ktk biashara na uwekezaji mkubwa.

..binafsi siamini kama kuna mikoa au maeneo ambayo yangeweza kuachwa nyuma. Kuna maeneo hapa nchini tumeaminishwa kwamba ni masikini lakini ukweli ni kwamba yana mali nyingi sana.

Kwa mfano, tumeaminishwa kwamba mikoa ya kusini ni masikini, lakini ukweli ni kwamba korosho ambayo inastawi huko ni utajiri uliojificha. Binafsi naamini nchi yenye ina baraka za kipekee kwa maana kwamba hakuna mkoa ambao haustawi zao kubwa la kibiashara. Majuzi nimesikia kwamba korosho zinastawi maeneo ya Dodoma na Singida.

cc tindo
 
Hapa tunaongea mambo mawili tofauti.

Jambo la kwanza ni serikali kufanya shughuli za kiuchumi, kwa mfano viwanda vya umma, mashirika ya umma, nasikia kulikuwa na hadi maduka ya serikali.

Jambo la pili ni kutokuwepo uchumi huria, yaani watu binafsi kutoruhusiwa kufanya biashara.

Sijui sana suala la pili maana kama ni kweli kwamba watu binafsi walizuiwa kufanya biashara kwa sababu ya siasa za azimio la Arusha, hilo lilikuwa kosa kubwa kimkakati.

Mi nimejikita sana kwenye suala la kwanza: kwa nini ujamaa wetu haukunufaisha viwanda vya serikali, mashirika ya serikali, n.k.

Hoja yangu ni kwamba uendeshaji wake ulikuwa mbovu sana kutokana na viwango vya maarifa na weledi vya wasimamizi wa hizo taasisi.

Lakini mantiki yake ilikuwa sahihi, kwamba kwa nchi changa, inayoanza kujijenga kiuchumi, hatua za mwanzo za kuwaweka watu sawa kielimu na kifursa na kwamba faida yoyote inayopatikana inufaishe watu wote, ilikuwa muhimu sana.

Siasa za kijamaa hazikuwa Tanzania pekee. Israel pia walikuwa na Kibutz ambayo ilikuwa vijiji vyao vya kijamaa.
 
Wale genetically born Wana akili, Sasa we linganisha na watu wako hata kutengeneza choo hawaeezi wanajisaidia porini Kama ngedere,
Sisi bado Sana ku catch up na dunia inabidi tusaidiwe Kwanza Kuna generation zitakuja kustaarabika baadaye
Jianaume kabisa linasema lisaidiwe choo...utakuja usaidiwe had mkeo.. Kwan wazungu walisaidiwa na nan ....
 
Jianaume kabisa linasema lisaidiwe choo...utakuja usaidiwe had mkeo.. Kwan wazungu walisaidiwa na nan ....
Ccm bana, kila siku mnatuonyesha ufunguzi wa miradi ya vyoo inayofadhiliwa na wahisani, kawaulize ccm
 
ni ngumu kwakweli tz kuishi bilaa dunia, wakijitoa hata kwa 80% ndiyo tutajua maana yake. mkikumbuka wakati tunaingia kwenye vita vya kagera marafiki zetu waligoma kutukopesha silaha tukanunua kwa sehemu kubwa kwa pesa yetu cash kilichotupata mpaka leo bado tumefunga mikanda. Global fund inafanya kazi kubwa sana kwenye sekta ya afya, huku kupungua kwa malaria,vifo vya mama na mtoto, chanjo kutokemeza polio,ndui,ukoma n.k ni mabeberu ndiyo wanatoa. mikopo inayotufanya tufanye miradi mikubwa ni mabeberu ndiyo wanatoa. kwa hiyo kwa kiasi kikubwa kuina ukweli kwenye hilo. lakini ubishi lazima tuwe nao tukilaza vichwa chini ooh watatula kwelikweli si ujaua mjasiriamali akipata upenyo wa kutengeneza faida atautumia vizuri sana na kwa bahati mbaya hawanaga shukurani
 
Closed economy sio suluhu au sio suluhu kwa kila nchi. Hizo nchi za magharibi zilikuwa na closed economy?

Tatizo la nchi zilizokuwa au zinazojaribu kuwa za kijamaa ni kufifisha ubunifu huru wa watu binafsi. Kila kitu ifanye serikali au kupitia serikali.

Kila kitu ni mlolongo wa mambo ya kirasimu.
 
School boy!
Mfano rahisi Ni mambo wanayofanya viongozi wa ccm yanadhibitisha na kudhibitisha uduni wa akili ya mtu mweusi
Kwa mujibu wa tafiti

Bisha nikupe mifano
i) Utafiti upi unaothibitisha mtu mweusi anauduni wa akili kwasababu ya mambo yanayofanywa na viongozi wa ccm?

ii) Huo utafiti umefanywa na nani? support this with very reliable attachment so that the public can appraise your integrity.
 
Watu wenye sifa hizo walikuwepo, ni wazungu, lakini hawakuamini au kukubali katika kujitoa sadaka ya ujamaa kwa ajili eti ya nchi ya watu weusi.So

Bepali hawezi kukubali ujamaa kwasababu nyingi, ila moja ya sababu kubwa ni uvamizi wa maeneo. Kwa mfano Marekani, watu wa asili wa Bara America wanafahamika ni akina nani. Sasa usitegemee mvamizi (mzungu kutoka ulaya) akakubali kwenda sawa na wenyeji(Red Indies).

Ni sawa na Kaburu wa afrika ya kusini yule nae ni mvamizi hawezi kukubali ujamaa.

Kuna mijizi mingine kule Australia imejaaa tele, usitegemee ikaunga mkono ujamaa. Sababu moja katika nyingi zilizopo ni hawataki waende sawa na wenyeji akati wapo kwenye ardhi ya wizi.
 
Tungeedelea na utaratibu wa awali tungekuwa kama style ya South Africa leo. Una utajiri wa kutupwa na umaskini wa kutupwa ndani ya nchi moja. Cha kushangaza matajiri ni watu wa rangi moja na maskini ni watu wa rangi nyingine.

Maarifa mazuri kama haya mue mnahubiri hata huko mliko watu wafahamu huu ukweli mchungu.

Tanzania kiuchumi tumeaanza kukaza mwendo, ila kwa mambo mengi Tanzania ni heaven.
 
Kama na wewe ni mchumi,kazi ipo
 
usisikilize wehu! Watu tunataka uhuru lakini wehu wanataka kuendelea kuwa watumwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…