Nakubali kwamba huo ubwanyenye uliojitokeza katika azimio la Arusha ndicho miongoni mwa vile ninavyoviita "watu wetu kutokuwa na elimu na maarifa" ya kutuongoza katika uchumi shindani. Uchina na Urusi ya wakati ule kuna mijitu ilikuwa imeshiba kimaarifa na ujamaa wao ulienda sambamba na weledi. Kuna tofauti kubwa kati ya meneja wa kiwanda cha serikali anayeongoza kwa kufuata weledi na kanuni za ushindani wa kibiashara kwa ajili ya maslahi ya umma, na meneja wa kiwanda cha serikali asiye na maarifa wala weledi wala ubunifu wowote.
Watu wenye sifa hizo walikuwepo, ni wazungu, lakini hawakuamini au kukubali katika kujitoa sadaka ya ujamaa kwa ajili eti ya nchi ya watu weusi.
Suala kwamba tuengeendelea na siasa hizo tungekuwa mbali kiuchumi....may be!
But kwa gharama kubwa sana, maana kuna mikoa na watu ingekuwa ndoto kutoboa. Usiende mbali chukulia mfano South Africa.
Nakwambia hiyo nchi ni nchi mbili maskini na tajiri ndani ya nchi moja, na ubaguzi uliokithiri kunakosababishwa na pengo la walio nacho na wasio nacho. Ujamaa sio mbaya kivile, ni namna mnavyouendesha.
So
..unajua wakati wa utawala wa muingereza kulikuwa na sheria zinazowabana wazawa wasijihusishe na biashara au ujasiriamali.
..kwa mfano, kulikuwa na masharti magumu kwa wazawa kupata mikopo ukilinganisha na waasia au wazungu.
..sasa tulipopata uhuru ilitakiwa wazawa wapate ahueni ktk kupata mikopo, ku-accumulate mitaji, na kufanya biashara kubwa.
..bahati mbaya ni kwamba mwaka 1967 azimio la arusha likaanzishwa na kufunga milango ya opportunities za kimitaji na kibiashara kwa wazawa.
..mwaka 1984/85/86 milango ya biashara ilipokuja kufunguliwa wazawa walikuwa wameshadumaa. ndugu zetu wa kiasia waliweza ku-pick up faster kwasababu shughuli za biashara zipo ktk familia zao for two or even three generations. pia wao walibakiwa na mitaji yao ingawa haikuwa mikubwa.
..milango ya biashara ilipofunguliwa wazawa tulikuwa kama tumeshtukizwa tusijue nini cha kufanya kutokana na jinsi tulivyokuwa tumebanwa na azimio la arusha.
..mfanyabiashara kama Mo Dewji ameendeleza mali za baba na babu yake. Aliko Dangote ametokea familia ya wafanyabiashara, ambapo babu yake alikuwa mfanyabiashara mkubwa. kwa hapa Tanzania mzawa kama Mzee Mengi, Ali Mufuruki, etc biashara zao zilikuwa ni first generation.
..Azimio la Arusha limechelewesha wazawa kuingia ktk biashara na uwekezaji mkubwa.
..binafsi siamini kama kuna mikoa au maeneo ambayo yangeweza kuachwa nyuma. Kuna maeneo hapa nchini tumeaminishwa kwamba ni masikini lakini ukweli ni kwamba yana mali nyingi sana.
Kwa mfano, tumeaminishwa kwamba mikoa ya kusini ni masikini, lakini ukweli ni kwamba korosho ambayo inastawi huko ni utajiri uliojificha. Binafsi naamini nchi yenye ina baraka za kipekee kwa maana kwamba hakuna mkoa ambao haustawi zao kubwa la kibiashara. Majuzi nimesikia kwamba korosho zinastawi maeneo ya Dodoma na Singida.
cc tindo