Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Tanzania haiwezi kuishi bila dunia ila dunia inaweza kuishi bila Tanzania

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Tanzania haiwezi kuishi bila dunia ila dunia inaweza kuishi bila Tanzania

Cha msingi huyu Mgombea na watu wenye fikra kama zake wanatakiwa kujua, sio kwamba Tz haitaki uhusiano na mataifa mengine iwe west or east, lakini JPM focus yake kwa sasa ni kurekebisha mambo yetu ya ndani ili tuweze kufanya biashara yenye tija zaidi na nchi zote .
Hivyo hili la kusema tunajitenga au hatutaki mahusiano na nchi zingine ni ndoto au propaganda za hao wanaoropoka ili kukuonyesha JPM kama mtu Mbaya n.k
Na wao waenezao chuki wapate pakupita kwa ujinga wetu wenyewe.
Well said, Big up sana mkuu...naona we umenielewa kuzidi wote [emoji123]
 
Tundu Lisu re uchumi
Uchumi uko wa aina mbili open economy ambayo nchi haiwezi ishi bila kutegemea nchi ingine

Aina ya pili ya uchumi ni closed economy ambapo nchi hukataa kuishi kwa kutegemea nchi nyingine kabisa
Nchi zote zilizoendelea zilianza na closed economy mfano China mwaka 1949 Mao tse Tung alitangaza mapinduzi ya kiutamaduni alifunga mipaka yote akasema kila kitu kinachohitajika china wachina wenyewe wagundue vingine wafe hakuna kuna ku mport wala kuexport chochote China iwe elimu au bidhaa au huduma

Wachina wakaingia kazini kugundua vitu kibao kuanzia dawa za kichina nk Baadaye uchumi wa china ukafunguliwa yeye ndio biggest exporter wa Bidhaa world wide anakopesha hadi marekani

Magufuli kuna vitu kufanya ni close economy ili ku save pesa za kigeni ili kujenga Maendeleo ya ndani badala ya hizo pesa kupelekwa nje kwa kisingizio cha semina,warsha na safari za Raisi na ujumbe wake ulaya na marekani
We nae unavituko model za 1960 unataka Ku apply 2020?? ,hizo foreign reserve alizo save hadi sasa zipo ngapi???
 
Mwambie Lissu kwa sasa mashirika ya ndege, Ethiopia imeongeza kutoka 4 flights mpaka 14, Qartar 3 mpaka 12. Hivyo hivyo kwa KLM. Uhusiano upi anautaka?

Ule wa viongozi kupishana angani hatuataki Kwa sababu ulikuwa ni miradi ya watu kupiga masurufu ya safari. Wako watumishi wa serikali wamekuwa mamillionea kupitia huo mradi.
Good
 
Watz na ccm yenu mnashindwa kutengeneza hata toothpick tu halafu mnajilinganisha na North Korea. Pumbavuuu
Wewe na chadema yako, una wazo gani la kiteknolojia, ambalo Tz ya Wana CCM imekufanya ushindwe kuliempliment?? Au umejisikia kubweka tu hapa 🤔?
 
Wakuu habarini za jioni,

Natumai mko salama na mnaendelea na majukumu yenu.

Nimeona niulete huu uzi wa mheshemiwa Tundu Lisu hapa tuujadili ili tuone kama kweli hoja hii ina mashiko . Nimemsikiliza huu mheshimiwa (Tundu Lisu) akiwa Shinyanga anasema kuwa Tanzania haiwezi kuishi bila Dunia ila Dunia inaweza kuishi bila Tanzania, na akasema akishinda uraisi basi atahakikisha anarudisha mahusiano mema ya Tanzania na nchi za magharabi ambazo Magufuli anaonekan a kujitenga nazo.

Je ni kweli kuwa Tanzania haiwezi kuendelea bila mahusiano mema na nchi za kibepari ? Kama ni kweli Je vipi kuhusu nchi kama Korea Kaskazini na Cuba ambazo ni kama zimetengwa na ulimwengu hasa mataifa makubwa lakini mbona wanaishi ?

Ukiangalia korea kaskazini ina uhusiano na China na Urusi pekee lakini Je mbona wanaendelea kusonga mbele na wameweza hadi kutengeza silaha za Nuclear kuwatisha hadi wamarekani, nawasilisha
Magufuli hajajitenga na mataifa ya Magharibi yeye amejikita kazini Jambo ambalo mataifa ya Magharibi hawataki kuliona, ndio maana kumpa nchi Lissu ni sawa na kuiuza kwa mabeberu.
 
NDUGU HUU UCHUMI WA MAO Ulipingwa sana China na watu kama Deng Xping,, waliamini kabisa kwamba Mao alifanya makosa makubwa kuifunga China na Dunia,,. dENG xPING ALIWEKWA KIZUIZINI na Mao kwa zaidi za ya miaka 8. Baadaye baaada ya Kufariki Mao, Deng XPING Alikuja transform huo mfumo kwa kuingiza chembe chembe nyingi za kibepari.
Na hata sasa Cuba nao wanafanya haya haya.

Hat NORTH KOREA wapo taabani kabisa ukifananisha na wenzao wa South Korea,, hata East Germany ambayo pia ilikuwa na sera hizo za closed economy hali yao ilikuwa Mbaya ukifananisha na West Germany kabla ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlin na kwa kweli CHINA wanamshukulu sana kiongozi wao DENG XPING aliyebadilisha mambo,, kwa kuiingiza sera za ubepari ambazo Mao Hakutaka hata kusikia. Na ndio maana taifa likapiga hatua kubwa sana

Na RUSSIA hii ya PUTIN siyo Russia ya Lenin, wala Stalin ,,kwa sasa wameingiza sana sera na mtazamo wa kipebari kwenye uchumi wao na waliachana kabisa na sera za closed economy.

KWAIYO NI SAHIHI KWAMBA DUNIA INAWEZEKANA BILA TANZANIA, LAKINI TANZANIA HAIWEZEKANI BILA DUNIA,,.
Mifumo yote miwili ya uchumi (Ujamaa-Socialism na Ubepari-Capitalism) ina faida zake na hasara zake pia, lakini kwa haraka ni kwamba kwenye ubepari (capitalism) uchumi unakuwa kwa haraka kwa sababu ya uhuru wa kibiashara na ushindani ingawa maskin wanakuwa wengi mno kuliko matajiri, na kwenye Socialism-Ujamaa uchumi unakuwa kwa pole pole ama kwa kawaida sana ila watu wote mnakuwa almost level sawa za kiuchumi, yaani si maskini sana wala si matajiri sana
 
Lakini usisahau kuwa tumekopa fedha nyingi za mabeberu kwa hi miaka 5 ya Magufuli
Si kweli kwamba kwa hii miaka mitano ya magufuli, pesa tulikuwa tunakopa tangu nyuma tena kikwete kakopa sana kuliko hata magu
 
Usidhani wote mburula humu! Corona tumeishinda kwa kuwa hatupimi tungeendelea kupima ungeona maajabu!! Kwanza naamini ni immunity zetu tu!!
Kama hatupimi mbona na tuna korona mbona hatufi ? Mbona kenya tu hapa majiran wanakufa
 
Najua akili yako imekutuma kwenye Impliment, siko huko Mimi [emoji23][emoji23] Kama hujaelewa tafuta dictionary.Afu ndo unataka kujiafanya ubongo mkubwa[emoji848]?
Ulichoandika ndio jibu la swali nililouliza ?

Kama swali dogo tu nimekuuliza, umeshindwa kulijibu, badala yake unajishika kiuno na kujichekesha kama dadapoa ndio unategemea utamshawishi mtu amchague babu yenu jiwe
 
Wakuu habarini za jioni,

Natumai mko salama na mnaendelea na majukumu yenu.

Nimeona niulete huu uzi wa mheshemiwa Tundu Lisu hapa tuujadili ili tuone kama kweli hoja hii ina mashiko . Nimemsikiliza huu mheshimiwa (Tundu Lisu) akiwa Shinyanga anasema kuwa Tanzania haiwezi kuishi bila Dunia ila Dunia inaweza kuishi bila Tanzania, na akasema akishinda uraisi basi atahakikisha anarudisha mahusiano mema ya Tanzania na nchi za magharabi ambazo Magufuli anaonekan a kujitenga nazo.

Je ni kweli kuwa Tanzania haiwezi kuendelea bila mahusiano mema na nchi za kibepari ? Kama ni kweli Je vipi kuhusu nchi kama Korea Kaskazini na Cuba ambazo ni kama zimetengwa na ulimwengu hasa mataifa makubwa lakini mbona wanaishi ?

Ukiangalia korea kaskazini ina uhusiano na China na Urusi pekee lakini Je mbona wanaendelea kusonga mbele na wameweza hadi kutengeza silaha za Nuclear kuwatisha hadi wamarekani, nawasilisha
Hahaaa hivi mnauwezo wa kujitengenezea dawa?
Vipi chanjo mtazipata wapi?
Mna viwanda vingapi vya magari?
Je, mnamitambo ya kuzalisha mashine?
Msiwatumbukize watanzania kwenye shimo ambalo hawataweza kutoka kamwe.

TL kasema ukweli. Na ukweli siku zote huwa ni mchungu
 
Hoja yako ni msingi mkuu....ila mimi ninachopinga kwa lisu, si kweli kwamba Tanzania imejitenga na Marafiki iliyokuwa nayo....alichofanya magufuli ni kujitenga na marafiki ambao walikuwa ni wanyonyaji na wala si kweli kuwa mpaka sasa tumebaki bila rafiki....mfano : Tangu mwaka 1999 tumekuwa tukiibiwa dhahabu, tukidanganywa kwamba ni mchanga unaenda kuchenjuliwa nje ya nchi sijui japan,,, alivoingia magu akapiga marufuku wachenhjulie hapa hapa....kama hawataki wasepe wakate tu na uhusiano kama wanataka maana huu ni urafiki wa kijambazi kabisa , nafikir umenielewa aina ya urafiki ninaoumaanisha
Haya basi tuambie kwa sasa huo mchanga una chenjuliwa wapi?
 
N.Korea ina technology ya juu,pamoja na vikwazo inajikongoja lakini China inaipa msaada mkubwa,Tanzania tecknolojia 0%,ikijitenga inakufa
Nafikiri issue siyo kujitenga, Tanzania haijitengi ila inachagua marafiki wenye faida na siyo marafiki wanyonyaji
 
Hawa chadema walimwita JK vasco dagama, hawahawa wanasema JPM hasafiri, hivi niwaulize ulishasikia queen elizabeth kasafiri? Kwahiyo UK Ina uhusiano mbaya na mataifa?
 
Back
Top Bottom