Huyu mbwatukaji wa hovyo sana, anafikiri baada ya hiyo miaka 2 rais atakuwa yeye? Samia yupooo!
Wewe unawaza urais tu kwa sababu ndiye mungu wako .
Biblia iko sahihi sana unaposema rushwa hupofusha macho .
Yaani ukiangalia kwenye mitandao utaona mpaka baadhi ya viongozi wa dini wamekua vipofu kwa sababu ya rushwa na hofu hata ya kutamka neno haki.
Leo viongozi wa baadhi ya dini wanaogopa kusema wazi kuwa bila haki amani ya nchi itayumba.
Watu hawaoni ubaya wa sheria kwa sababu wapo madarakani na familia zao zinanufaika.
Jifunzeni kitu kwa yule polisi anayefukuzwa kwenye nyumba za serikali wakati ametumikia kwa miaka zaidi ya 30 kwa kutii na uvumilivu hata pale alipodhulumiwa haki yake.
Yule polisi anatamani pangekuwa na watu wa kupigania haki yake mapema lakini hana watu.
Aliodhani ni wenzake hawana habari naye kwa sababu hao hao ndio waliokula pesa zilizopaswa kulipwa kwake .
Hana pa kukimbilia maana sheria za dhulma zinambana .Waliokula na kudhulumu malipo yake wapo salama zaidi kwa sababu wapo kwenye mfumo usiojali malalamiko ya watu . Pale amejitoa tu muhanga lakini maisha yake yako hatarini kwa sababu serikali iliyopo haitaki kuambiwa ukweli wala kulaumiwa zaidi ya kusifiwa kama Mungu.
Yule polisi atufungue macho tudai sheria za haki na katiba inayowajali watu wote ndani ya nchi hii.
Katiba iliyopo inapigania maslahi ya walioshiba na kuvimbiwa. Ndio maana wanaCCM wote wanaufyata wanapoona kakikundi kadogo kanakazimisha mtu asiye na maono yoyote kugombea urais bila kupingwa kwa sera na maono juu ya Taifa hili . Mtu asiye na maono hawazi namna ya kuwasimamia na kuwaelimisha watanzania namna ya kutumia rasilimali zao wenyewe. Anawaza tu kuuza kila kitu halafu watanzania wabaki kama manamba kwenye nchi yao.
Fuatilia uone kama ni sahihi Zoezi la kuhakiki wapiga kura liko sawa !!
Yaani nchi kwa sasa ina vijana zaidi ya mil. 30 halafu zoezi hilo linafanyika kwa siku zisizozidi kumi . Yote ni kwa sababu ya kutumia watumishi wa halmashauri .Yaani kusambaza tu vifaa vya kujiandikishia na kuhakiki ni zaidi ya wiki mbili lakini zoezi la kuandikishwa ni siku kama tisa au nane tu. Sasa hapo kitakachofanyika ni kutengeneza majina feki ili kuwafurahisha waliowatuma.
Ujinga huo waliufanya kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa .
Wanaandika majina feki na kutoa takwimu za uongo .
Hivi tangu 2015 mpaka leo wamekufa watu wangapi na wameongezeka wangapi ?
Watajuaje kuwa wengine ni marehemu wasiporudia na kuhakiki kwa watu wote na iwe ni zoezi la lazima na lifanyike bila kujali mtu atampigia wapi kura ili kwanza watolewe marehemu na kuandikisha wapya .
Kila kitu kinachofanywa na wanasiasa na wateule wa Rais kipo kimaslahi binafsi na sio taifa.
Hivi kama inawatumia wafanyakazi wa umma wanaolipwa na serikali kama walimu na polisi na watumishi wengine kwa nini wasifanye kazi hiyo kama Sehemu ya majukumu yao kwa mwajiri .
Walipwe wale tu wanaotoka nje ya ajira kama Migambo basi.
Tunpoteza pesa nyingi kulipa watumishi ambao ni kazi yao kwa mwajiri .
Basi ni bora tume itangaze nafasi za kuomamia uchaguzi kwa Wasio na ajira ili walipwe na wafanye kazi chini ya tume na sio mkurugenzi.
Zoezi la uhakiki wa Daftari la'mpiga kura liendelee mpaka mwezi wa nne miezi miwili ili watu wote wajiandikishe na marehemu waondolewe kwenye daftari la wapiga kura .
Nchi gani inapata viongozi waliochaguliwa na wafu .
CCM wanapenda madaraka sasa watanzania wengi wanataka rais na bunge lake waongezewe muda mpaka tume na katiba ifanyiwe marekebisho lakini pia daftari la mpiga kura lifanyiwe maboresho na majina yabandikwe mapema kila mtu aone orodha ya watu hai sio marehemu .
Nchi hii sio mali ya Samia wala CCM wala polisi bali ni ya watu wote mil.64. Sasa kama karibu nusu ya watanzania hawakubaliani na mfumo wa kupata wawakilishi basi ni bora ufanyiwe kazi kuepusha Shari . Watu karibu mil 40 hawataki mfumo wa uchaguzi hasa vijana .CCM mnataka mtumie majeshi kuwaua wote kwa sababu ya Kumfurahisha Mzanzibari mmoja na mkwe wake . ? Hapana hayo marekebisho hayana ubaya wowote kwa polisi wala jeshi zaidi ya hofu ya mafisadi wachache wanaoogopa kunyimwa kura.