Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

Kazi gani, wakati yeye ndiye chanzo cha Mbunge wake kuropoka kama kama mtu aliyefumaniwa Chooni.
Mkuu siasa inahitaji uvumilivu wa hali ya juu. Lugha kama hii uliyoitumia hapa haifai,cha msingi ni kubishana kwa hoja za msingi na zinazojenga na mwisho wa siku wananchi ndiyo wenye maamuzi ya mwisho.
 
Mkuu samahani mizaha kama hii inalishushia hadhi jukwaa hili,Sidhani kama kweli chai na juice vinapatikana Ikulu peke yake Tanzania nzima au viongozi hao wamekosa fedha za kununua chai na juice mpaka waende ikulu.
huo ndio ukweli, walivoonja ya mara ya kwanza wamenogewa, sasa wanaitaka tena
 
Heading na content haviendani mkuu...binafsi nilidhani utakuja na hoja za kutokukubaliana na kauli ya Freeman Mbowe.

Lakini nikionacho ni maelezo tu ukieleza tu hali ya mambo ilivyotukia...umeshindwa hata kuweka bayana hizo hoja za Lissu ambazo kwazo Mh. Jakaya Kikwete anaziona ni za kizandiki...

Msamehe tu mkuu, ameona ndio namna pekee ya uzi wake kusomwa! Ama kweli upumba.vu ni kipaji!!
Maneno kaweka meeengi ila kinachoongelewa sasa ndio hakipo!
 
CHADEMA kama wanajitakia mema na waendelee kukubalika na kuungwa mkono na wananchi, ni vema wakajitafakari na kupima upya uwezo na busara za watu wanaowakabidhi madaraka
 
Mbowe is smarter than JK..siku zote hawawaachi watu wao ktk mapambano haya.....
 
wewe umemezwa na ushabiki wa kutotaka kuona LISSU akiguswa, ndiyo wale wale mnaomvimbisha kichwa LISSU na kupelekea kujisemea kama mwendawaizmu.

Ungejua kuwa mtu uliyemuandikia hivyo wala hata haguswi na mambo yenu ya kushabikia vyama na kusahau mustakabali wa Taifa letu nadhani ungefuta hayo uliyoandika...

Imefika mahali lazima wananchi mtambue kuwa aseme Lissu au aseme Kikwete, kinachotakiwa ni kupata Katiba yenye rutuba na sio kuanza kupishana kauli...

JK alichotakiwa kufanya sio kuanza kulumbanisha kauli, au kuanza kuwanyooshea vidole wafuasi wenzake wa CCM au kina Lissu & Co...kumbuka katiba ya JMT inamtambua JK kama Rais wa Watanzania(pasipo kuzingatia itikadi zao) na sio Mwenyekiti wa CCM

ALitakiwa atoe tamko lenye kuashiria hitimisho la mnyukano uliojitokeza kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania...lazima ujue hao kina Lissu au CCM wataendelea kuzozana na wala hawataweza kuwa kitu kimoja...
 
Sikubaliani kabisa na maneno ya MBOWE kuwa, Rais JAKAYA KIKWETE kumshambulia TUNDU LISSU wakati wa hotuba yake kuwa alimuonea kwa madai kuwa maneno ya LISSU hayakuwa yake bali ni ya kambi rasmi ya upinzani.

Nadiriki kusema kuwa wanachokifanya hivi sasa CHADEMA ni kujaribu kumusafisha LISSU na tabia yake ya siku nyingi kutoa maneno ya kizushi, dhihaka kwa serikali na mbwebwe nyingine nyingi ambazo kwa uhakika wanaolitakia amani taifa letu, ndani ya Bunge(wale wa chama tawala na upinzani), nje ya bunge, wasomi na hata wananchi wa kawaida walishaanza kuingiwa wasiwasi na utimamu wa akili ya Mbunge huyu.

Siku chache zilizopita , LISSU amepambwa sana kwenye vyombo vya habari, wapambe wake, kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mtu tishio, lakini hakuna aliyesimama na kusema siyo yeye aliye tishio bali ni chama kwa ujumla, ila leo ambapo Rais ameonesha kukerwa na pengine sasa kama mkuu wa nchi anaona anakoelekea LISSU ni hatari kwa amani ya nchi yetu ndipo wanaibuka akina MBOWE na kusema kuwa yale yalikuwa maneno ya Kambi ya Upinzani na kwamba Rais hajamtendea haki na kwamba amuombe msamaha, kwa lipi mpaka rais amuombe msamaha LISSU kama siyo kumkosea adabu mheshimiwa Rais na kuendelea kulea ugonjwa kwa vile LISSU ataona kama amepewa go ahead na mkubwa wake kuendelea kusema hovyo.

MBOWE anasemaje Rais amuombe radhi LISSU wakati huo wanampongeza kwa hotuba yake huku wakisema amewaaibisha wana CCM ambao walionekana kuunanga muungano wao vyama vitatu, muungano ambao kimsingi umekosa mashiko hasa baada ya hotuba ya Rais JAKAYA KIKWETE. Wanamtaka Rais awaite kwenda ikulu kufanya nini kama kweli wanaona LISSU ameonewa?

You know the words but you miss their meaning! Psychophancy is a form of mental disorder; Brother Bonsoiree please seek psychiatric assitance before it is too late!!!
 
Mkuu, naona wewe ndo hujaelewa kabisa. Mbowe katika maelezo yake anasema kuwa alichosema Lissu kina baraka ya kambi ya upinzani kitu ambacho sicho. kama maneno ya uongo, uzandiki na uzushi ni msimamo wa kambi ya upinzani, basi sina imani kabisa na chadema

Mkuu nimemuelewa ndugu mleta mada kwa mujibu wa alivyojitahidi kufafanua...

Suala ambalo nilitaka mleta mada kwa upeo wake atufafanulie, je hayo mawazo ya Tundu Lissu ambayo Bw Mbowe ameyaita ni baraka kutoka Kambi Rasmi ya Upinzani yana mantiki yoyote?

Je aliyoyazungumza Bw. Lissu yana maslahi na tija katika upatikanaji wa Katiba Mpya?

NB:
Tambua kuwa mvutano huu sasa umegeuzwa kuwa ni jambo la kisiasa na sio jambo la umma...
 
CHADEMA kama wanajitakia mema na waendelee kukubalika na kuungwa mkono na wananchi, ni vema wakajitafakari na kupima upya uwezo na busara za watu wanaowakabidhi madaraka

Kwa hiyo wewe umejitafakari na kujipima upya uwezo na busara zako kwamba una uwezo wa kuishauri CDM kwamba viongozi wake hawafai?! Akili nyingine bwana!!!?? teh teh!!!!!!!!!!!!
 
Sikubaliani kabisa na maneno ya MBOWE kuwa, Rais JAKAYA KIKWETE kumshambulia TUNDU LISSU wakati wa hotuba yake kuwa alimuonea kwa madai kuwa maneno ya LISSU hayakuwa yake bali ni ya kambi rasmi ya upinzani.

Nadiriki kusema kuwa wanachokifanya hivi sasa CHADEMA ni kujaribu kumusafisha LISSU na tabia yake ya siku nyingi kutoa maneno ya kizushi, dhihaka kwa serikali na mbwebwe nyingine nyingi ambazo kwa uhakika wanaolitakia amani taifa letu, ndani ya Bunge(wale wa chama tawala na upinzani), nje ya bunge, wasomi na hata wananchi wa kawaida walishaanza kuingiwa wasiwasi na utimamu wa akili ya Mbunge huyu.

Siku chache zilizopita , LISSU amepambwa sana kwenye vyombo vya habari, wapambe wake, kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mtu tishio, lakini hakuna aliyesimama na kusema siyo yeye aliye tishio bali ni chama kwa ujumla, ila leo ambapo Rais ameonesha kukerwa na pengine sasa kama mkuu wa nchi anaona anakoelekea LISSU ni hatari kwa amani ya nchi yetu ndipo wanaibuka akina MBOWE na kusema kuwa yale yalikuwa maneno ya Kambi ya Upinzani na kwamba Rais hajamtendea haki na kwamba amuombe msamaha, kwa lipi mpaka rais amuombe msamaha LISSU kama siyo kumkosea adabu mheshimiwa Rais na kuendelea kulea ugonjwa kwa vile LISSU ataona kama amepewa go ahead na mkubwa wake kuendelea kusema hovyo.

MBOWE anasemaje Rais amuombe radhi LISSU wakati huo wanampongeza kwa hotuba yake huku wakisema amewaaibisha wana CCM ambao walionekana kuunanga muungano wao vyama vitatu, muungano ambao kimsingi umekosa mashiko hasa baada ya hotuba ya Rais JAKAYA KIKWETE. Wanamtaka Rais awaite kwenda ikulu kufanya nini kama kweli wanaona LISSU ameonewa?

Ni wazi na kwa ukweli usiopingika kwamba Kikwete kamuonea Lissu kwa sababu zifuatazo

1 Kama kikwete ameona kwamba Lissu ni mnafiki,mzandiki na malina yooooote aliyoyatumia na aliyoona kwamba akiyatumia atakuwa amemuumiza sana Lissu ni kwanini ameurudisha huo muswada bungeni?

2 Hata Rais nae hayo majina aliyoyatumia kwa Lissu yanamfaa kwanini amekubali kurudisha kitu ambacho chimbuko lake ni fitina,majungu na uzandiki?

3 Kikwete anajipa imani kwamba yeye ni mkweli kwa kiasi gani? Na ikigundulika baadae kwamba alikurupuka kutoa majina hayo yote kwa Lissu afanyiwe nini? Sababu muswada unarudi bungeni utaanza kujadiliwa upya je ikionekana hayo maneno Rais aliyatumia kimakosa na kosa wanalo waliomshauri je?

4 Rais ataendelea kuwa kiongozi wa kuongea mipasho hadi lini? Rais anatakiwa awe na msimamo,aonyeshe njia,akemee,aagiize ,aamuru kukamata lakini ni ajabu Rais kukalia mipasho tu,na kama Lissu alikuwa na makosa uwezo wa kumuita wakajadili alikuwa nao,inasaidia nini kutoa kashfa ikigundulika umemkosea atamuomba samahani kama alivyotoa kashfa? Inatakiwa Rais awe na busara kidogo,sasa sijui ni Rais mwenyewe au walioandika hiyo hotuba ndio waliandika mtusi hayo?
 
sahihi kabisa mkuu, tatizo la watanzania wa sasa wengi wao wamebakia kwenye ushabiki wa vyama na sio maslahi yao binafsi kama raia wa kitz,
hao wanaoendelea kubishania vyama waacheni waendelee ila naunga mkono alichozungumzia rais kwenye hotuba yake,
watz tuangalie suala zima lakatiba ya nchi yetu na sio malumbano yasiyo na msingi wowote
Ungejua kuwa mtu uliyemuandikia hivyo wala hata haguswi na mambo yenu ya kushabikia vyama na kusahau mustakabali wa Taifa letu nadhani ungefuta hayo uliyoandika...

Imefika mahali lazima wananchi mtambue kuwa aseme Lissu au aseme Kikwete, kinachotakiwa ni kupata Katiba yenye rutuba na sio kuanza kupishana kauli...

JK alichotakiwa kufanya sio kuanza kulumbanisha kauli, au kuanza kuwanyooshea vidole wafuasi wenzake wa CCM au kina Lissu & Co...kumbuka katiba ya JMT inamtambua JK kama Rais wa Watanzania(pasipo kuzingatia itikadi zao) na sio Mwenyekiti wa CCM

ALitakiwa atoe tamko lenye kuashiria hitimisho la mnyukano uliojitokeza kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania...lazima ujue hao kina Lissu au CCM wataendelea kuzozana na wala hawataweza kuwa kitu kimoja...
 
Heading na content haviendani mkuu...binafsi nilidhani utakuja na hoja za kutokukubaliana na kauli ya Freeman Mbowe.

Lakini nikionacho ni maelezo tu ukieleza tu hali ya mambo ilivyotukia...umeshindwa hata kuweka bayana hizo hoja za Lissu ambazo kwazo Mh. Jakaya Kikwete anaziona ni za kizandiki...

Ndio wasomi wetu hawa kaka. Hatuna jinsi.
 
:A S-confused1::A S-confused1:Hoja ni mkuu wa kaya kumshambulia na kumtaja mtu binafsi mpaka kwa jina TL kwa mambo ya kuambiwa.ww unaona ni sahihi?
kwann asijiulize upande watatu wa sarafu.

kwa tz kusema ukweli unahatarisha amani ya nchi lkn kusema uongo ndio kulinda amani?

NI HATARI MTU KUWA VUGUVUNGU AMUA KUWA BARIDI AU MOTO-PRINCIPLE OF NATURAL JUSTICE
 
Kuna kitu wana CCM wengi hawajui na hawapendi jifunza...JK kaongea alichoongea dhidi ya Lissu akidhani kuwa CDM wapo km CCM.CCM kuna kauli za bahati mbaya.... kuna kauli binafsi ambazo zinapingana na misimamo ya chama..

MAra zote CCM wamekuwa wakituma vibaya sana kuwepo madarakani na kuwa na Rais aliyepewa nguvu nyingi..Haya maringo n uzembe ndiyo yamefanya watumie ubabe kutojibu wala kuwajibisha mtu wakati kauli km "Kaskazini wasahau shika nchi", "kauli km Mfumo Christ", "kauli km Chadema ni chama cha wachaga", "kauli na mikutano ya siri ya kuwapiga wachaga vita"....

Wakati JK anamshambulia Lissu , hakuwa na clue kuwa Lissu pamoja na kuwa na uwezo mkubwa kisheria, kiutendaji na mengine ,mara zote huwa yupo consistent na mitazamo ya chama...Hii ni Tofauti kabisa na Zitto na SHibuda...Lissu km wana CDM wengine ambao hata CDM km Chama huwa wanasimama kidete kuwatette na kuwalinda wanachama wake popote.
JK sasa anaambiwa kitu na Mbowe ambacho hakuwahi jua wala hajui hadi sasa..pamoja na kuambiwa kuwa hizo ni kauli za chama na si Lissu.....ni kitu kipya sana kwa JK NA HAKUNA MJADALA RAIS ANAHITAJI KUOMBA MSAMAHA....Rais inabidi akumbuke kuwa hata Bungeni alipoongea Wenje .....CUF wakaja juu sana na CCM wakaanza unafiki nyuma ya mgongo....kwa kujenga Taswira kuwa wenje alikosea..Mbowe aliposimama aliweka sawa kuwa alitaka maridhiano tuu ila ile ni kauli ya chama na itabaki kuwasahihi.....

JK na MaCCM wote warudi ndani wakajifunze CDM kuwa hakuna kauliz abahati mbaya au za binfsi ktk za kaina Sita, Lowassa,JK, Pinda, Membe,Nape,Kinana, mangula ,Makamba etc ambazo hata kwa zenyewe hazilingani.
 
wewe umemezwa na ushabiki wa kutotaka kuona LISSU akiguswa, ndiyo wale wale mnaomvimbisha kichwa LISSU na kupelekea kujisemea kama mwendawaizmu.
Aliyemjibu mtu anayejisemea kama mwendawazimu tumwiteje?.
 
Mkuu nimemuelewa ndugu mleta mada kwa mujibu wa alivyojitahidi kufafanua...

Suala ambalo nilitaka mleta mada kwa upeo wake atufafanulie, je hayo mawazo ya Tundu Lissu ambayo Bw Mbowe ameyaita ni baraka kutoka Kambi Rasmi ya Upinzani yana mantiki yoyote?

Je aliyoyazungumza Bw. Lissu yana maslahi na tija katika upatikanaji wa Katiba Mpya?

NB:
Tambua kuwa mvutano huu sasa umegeuzwa kuwa ni jambo la kisiasa na sio jambo la umma...

mKUU, alichozungumza Lisu kwa maneno ya Mbowe ni msimamo wa kambi ya upinzani. kutokana na hali hiyo, huwezi kusema kuwa huo ni msimamo wa umma. chadema hawawezi kuwasemea watanzania kwani kila mtu ana utashi wa kufikiri na kutambua. tatizo kubwa chadema wamelifanya suala la katiba kuwa ni suala la kisiasa
 
Back
Top Bottom