Sikubaliani kabisa na maneno ya MBOWE kuwa, Rais JAKAYA KIKWETE kumshambulia TUNDU LISSU wakati wa hotuba yake kuwa alimuonea kwa madai kuwa maneno ya LISSU hayakuwa yake bali ni ya kambi rasmi ya upinzani.
Nadiriki kusema kuwa wanachokifanya hivi sasa CHADEMA ni kujaribu kumusafisha LISSU na tabia yake ya siku nyingi kutoa maneno ya kizushi, dhihaka kwa serikali na mbwebwe nyingine nyingi ambazo kwa uhakika wanaolitakia amani taifa letu, ndani ya Bunge(wale wa chama tawala na upinzani), nje ya bunge, wasomi na hata wananchi wa kawaida walishaanza kuingiwa wasiwasi na utimamu wa akili ya Mbunge huyu.
Siku chache zilizopita , LISSU amepambwa sana kwenye vyombo vya habari, wapambe wake, kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni mtu tishio, lakini hakuna aliyesimama na kusema siyo yeye aliye tishio bali ni chama kwa ujumla, ila leo ambapo Rais ameonesha kukerwa na pengine sasa kama mkuu wa nchi anaona anakoelekea LISSU ni hatari kwa amani ya nchi yetu ndipo wanaibuka akina MBOWE na kusema kuwa yale yalikuwa maneno ya Kambi ya Upinzani na kwamba Rais hajamtendea haki na kwamba amuombe msamaha, kwa lipi mpaka rais amuombe msamaha LISSU kama siyo kumkosea adabu mheshimiwa Rais na kuendelea kulea ugonjwa kwa vile LISSU ataona kama amepewa go ahead na mkubwa wake kuendelea kusema hovyo.
MBOWE anasemaje Rais amuombe radhi LISSU wakati huo wanampongeza kwa hotuba yake huku wakisema amewaaibisha wana CCM ambao walionekana kuunanga muungano wao vyama vitatu, muungano ambao kimsingi umekosa mashiko hasa baada ya hotuba ya Rais JAKAYA KIKWETE. Wanamtaka Rais awaite kwenda ikulu kufanya nini kama kweli wanaona LISSU ameonewa?