Tundu Lissu vs Fatma Karume

Hahaha, Ok Nyani, no need to be Sorry, ila ni vizuri ujiweke clear upo upande gani, hamna "Ukweli" duniani, Ukweli kwako unaweza kuwa uongo kwa mwingine. Ukweli ni relative thing
Mimi nazungumzia ukweli wangu.

Ya wengine nawaachia wengine.
 
Haijawai kuwa upande wa Haki ndo huelewi kitu. hivyo tulia
 
Zile tweet zake sasa hivi hazipo...na ushangazi wake kwa makamanda upo shakani
Ni kama yuko biased!

Magufuli angefanya hivi hivi alivyofanya Samia sasa hivi, kangekuwa kako mstari wa mbele kumchana Magufuli!

Not principled at all.
 
Fatma alikuwa mmoja wa wapiga debe wakubwa wa Mheshimiwa Rais wa sasa. Aliamini kuwa kama mwanamke mzanzibari halafu muislamu utawala wake utatofautiana sana na uliomtangulia. Alisema hulka yake haiko hivyo. Alitaka apewe muda ili aweke mambo sawa. Lakini matukio ya hivi karibuni yamembadilisha mawazo na sasa hivi ni critic mkubwa wa utawala uliopo. Amekiri kuwa alikosea.

Amandla....
 
“Amekiri kuwa alikosea” wapi? Kuna video au andiko lake popote pale linaloonyesha amekiri?
 
Swali la Fatma zuri sana...sema watu ni wavivu kusikiliza na kufikiri...Fatma amechokoza mada..na amejaribu kuwasilisha jinsi watu baadhi wanavyochukulia chadema...amempa nafasi lissu kudadavua mengi

Nashangaa mleta mada anajaribu ku personalize
 
Hii nadhani ni ya muda kidogo Nyani. Fatma sasa hivi kabadilika sana kuhusu kumkosoa huyo wa kudemka. Nafuatilia karibu kila siku Maria Space kule Twitter na kama mtu humjui kwamba hana chama basi utahitimisha kwamba ni Chadema.
 
Huu mjadala niliufuatilia vizuri sana. Na kwa jinsi ambavyo nimemuelewa Fatma Karume, ni kwamba anahisi CHADEMA wanafanya wafanyayo sasa kwa Samia kwavile ni mwanamke. Akawa anasema kipindi cha Magufuli wapinzani waliufyata, ila now wanaprovoke Samia kutoka na gender yake.

Baada ya kongamano la katiba kuzuiwa Mwanza, uhamuzi wa Mbowe kwenda Mwanza kusimamia ilo swala, Fatma alilitafsiri kama dharau kwenda kinyume na kauli ya Samia ( kwavile ni mwanamke).

Fatma ni feminist.

Lissu kuna kauli yake moja niliielewa sana. "Samia ni Mama kwa watoto wake,Rais kwa sisi wengine. Kauli ya Rais sio sheria, akikosea, atakosolewa"
 
“Amekiri kuwa alikosea” wapi? Kuna video au andiko lake popote pale linaloonyesha amekiri?
Ukimfuatilia kwenye twitter yake utaikuta. Amekiri kuwa Maria alikuwa sahihi kutomuamini Rais wa sasa toka mwanzo. They are now on the same page.

Amandla....
 
Hii nadhani ni ya muda kidogo Nyani. Fatma sasa hivi kabadilika sana kuhusu kumkosoa huyo wa kudemka. Nafuatilia karibu kila siku Maria Space kule Twitter na kama mtu humjui kwamba hana chama basi utahitimisha kwamba ni Chadema.
Hmm okay!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…