Hii nadhani ni ya muda kidogo Nyani. Fatma sasa hivi kabadilika sana kuhusu kumkosoa huyo wa kudemka. Nafuatilia karibu kila siku Maria Space kule Twitter na kama mtu humjui kwamba hana chama basi utahitimisha kwamba ni Chadema.
Heshima kwa shangazi
Wengi hawamuelewi shangazi...
Shangazi anazungumza kiuwakili zaidi... anauliza na kuongea kama yupo mahakamani anamtetea mtu... wengi wanafikiri anakisimamia chama cha majangili. Alichokuwa anatafuta ni majibu ya uwazi na uhalisia (ukisikiliza vizuri hata Lissu mwanzo hakuelewa lakini kabla ya kujibu aligundua sio shangazi anauliza bali ni wakili anauliza kama yupo mahakamani)
Anywho...
Ushabiki maandazi ndio unalipoza taifa
Hii mada ni ushabiki maandazi
Watu wanafurahi kuona au kusikia watu wamepishana mahala padogo..
Kila mtu Ana mawazo tofauti tuheshmu mawazo ya watu kuliko kushangilia watu wanapopishana kauli. Leo kuna wanaofurahia chadema wamepishana lugha wengine Mbowe yupo magereza wanaona ni 'alijitakia' Mbowe anaipenda Tz na watu wake kutoka moyoni wapo wanaikipenda chama na matumbo yao bila kujali wananchi wanataka nini. Mbowe hapiganii Katiba Mpya kwa sababu yeye atanufaika bali watoto na wajukuu na vitukuu wa kila Mtz wa vyama tofauti itikadi tofauti dini tofauti imani tofauti watafurahia na kujivunia nchi yao na kuwaenzi wazee wao (Mbowe na wengi wenye kulipenda Taifa)
Hebu watu wajaribu kugeuka nyuma then watazame mbele Wamtazame Muumba Wao
Upendo ni tunda la roho
Serikali inafurahia mkoroganyo uliopo sasa bila kufikiri yatakapomwagika hakuna atakayekwepa hukumu hii
Watawala upo ugumu gani wa kukaa na Vyama vya upinzani mkazungumza mlijenge Taifa
Huku kujimwambafai hakutawasaidia kipindi kirefu
Kila jambo Lina muda
Ushabiki maandazi ukome
Usifurahi Juu ya mwenzio apatapwo na shida huijui kesho yako....
Mbowe tunasema hivi "Bwana Akuangazie Nuru ya Uso Wake ..... Asikuache Ukaangamia.... Daniel aliokolewa kwenye midomo ya simba nawe utaokooewa kutoka kwenye mikono dhalimu....... Watesi wako watalikiri jina lako na uaminifu wako Juu ya Taifa..... Mungu Akulinde Akupiganie Akushindiye...