Uchaguzi 2020 Tundu Lissu Watanzania waliungana siku ulipopigwa risasi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu Watanzania waliungana siku ulipopigwa risasi

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Lengo la kukupiga risasi lilikua Ni kukuua,ufe kabisa halafu usiwepo Tena juu ya uso wa Dunia. Naamini baadhi wangelipwa kwa kazi ya Kukuondoa na wengine wangepongezana. Hata hivyo Kuna mamilioni ya Watanzania waliungana kwa kulia na kuugulia, walifanya vitu ambavyo havijawahi kufanyika hapa dunia.

Waislam, wakristu na Dini nyingine walifanya maombi, ibada, matambiko na kila Aina ya kafara ili kuwalaani waliokuua.

Hata hivyo kubwa kuliko yooote, ni baadhi ya Watanzania walisoma visomo,watu walisoma Ala Albadir Kama kulipa kisasi ili waliokuua wapatwe na majanga ama wafe na wao. Watu walisali sara za kulipiza visasi, watu walilaaani, watu walifunga na kuomba Mungu alipize.
Mbali na hayo watu walijitokeza sehemu mbalimbali za nchi hii kujitolea Damu, ili wewe uamke. Tunashukuru Mungu Uliamkia Kenya na kuponea Uberigiji.

Watu walichangishana fedha ili utibiwe.

Hata hivyo Mambo ya kushangaza hayo yooote yaliyofanyika yalipigwa marufuku sijui na nani.

Kwa Nini nayasema haya? Ni kwamba watu wanakuelewa,wanaelewa kazi zako,wanaelewa kuwa wewe Ni Mtanzania halisi na mtetezi wa Haki na mali za nchi.wanakielewa Chama Chao, Chadema, Kama Cha ma Cha kuwatetea wanyonge.

Tundu Lisu Sasa hivi wewe Ni mlemavu,hakuzaliwa hivyo,Bali umetengenezewa ulemavu. Mimi Lee, Sina Cha kukulipa,ila nitakupigia kura ya ndio kwako wewe,mbunge wako na Diwani wako,na, nitashawishi watu wengi kadri niwezavyo wafanye Kama Mimi.

Watu wanawakubali Viongozi wenzio wa Chadema, na wanajua magumu wanayopotia.

Ndio maana pale VIONGOZi wa Chadema walipowekwa ndani kionevu na walipowekwa adhabu ya kulipa faini kubwa za kionevu kuliko zote Duniani, watu wote,bila kujali vyama vyao waliwachangia mmoja baada ya mwingine, na wote wakatolewa.

Watu wana imani na Chadema na pia Wana imani na wewe. Kwa hayo yooote mnayoyapitia watu wema Tanzania nzima wameamua kukupa kura za ndio za kumwaga. Utapata kura mamilioni mbele ya mpinzani wako. Kwa lugha rahisi Utamzidi mshindani wako kwa zaidi ya kura kwa mamilioni.utampiga gepu ya kura milioni tano na hiyo Ni baada ya kuiba Sana ili Kuondoa aibu.
 
Kuishi kwa Lisu hadi leo bado ni maajabu yasiyoelezeka.
 
Back
Top Bottom