Tundu Lissu: Wenje atoe video recording ya mjadala wa tuhuma dhidi yake na wenzake kupokea pesa za Abduli na mama yake

Tundu Lissu: Wenje atoe video recording ya mjadala wa tuhuma dhidi yake na wenzake kupokea pesa za Abduli na mama yake

inatekenje amekiri mwenyewe kwamba kuna video recording ya mjadala wa tuhuma dhidi yake na wenzake kupokea pesa za Abduli na mama yake. Ni kweli. Walirekodi kikao hicho chote kwa video.

Ili kuondoa ubishi wa suala hili ninawashauri watoe video recording yote ya kikao hicho. Wasikate vipande vipande wala wasihariri chochote. Watoe video nzima ya mjadala huo ili wanachama na Watanzania wajue ni akina nani walituhumiwa kwa kupokea pesa ya Abduli na mama yake, ushahidi niliouwasilisha dhidi yao na wao wenyewe walijiteteaje!!!View attachment 3181258
Chadema yangu inateketea taratiiibu! Kama sio kiki, au kazi ya intelijensia ya chama, kuwapoteza maboya ccm, ni kitu harisi kabisa kinatokea, basi naiona njia ya kifo iliyopitiwa na nccr msgeuzi, cuf! Na hapo kuna mkono wa ccm na TISS,chadema kwishney
 
Lisu anahongeka, tena sana tu. Nyie msiomjua ndio mnasema hahongeki. Lisu alikatiwa mshiko (alihongwa) na mbowe wakati wa sakata la Lowassa kukodisha chama ili agombelee urais. Mwanzo alikuwa upande wetu wapinga Lowassa, alipokatiwa cha juu akatusaliti mchana kweupe kwa tamaa ya pesa. Tangu wakati huo nilimuondoa kwenye orodha ya viongozi wa kisiasa wenye misimamo imara. Lisu ni tapeli tu kama matapeli wengine wa kisiasa.
Mkuu unaweza kutoa ushahidi wa hicho unachokisema. Hii itakuwa ni njia sahihi ya kumzuia kuendelea kugombea na kupunguza maneno.
 
Majadiliano ya ndani ya kamati kuu hayawezi kutolewa hadharani hiyo ni kukibomoa chama hata kana Lissu ataonekana muongo.

Lissu ajibu tuhuma zilizotolewa na Wenje katika mahojiano ya Wenje na waandishi. Je Lissu anadaiwa na Wenje? Je Lissu alimtumia Abdul email ya madai yake. Lissu alisaidiwa logistics za matibabu Nairibi na Wenje. je ni kweli kikao cha Masaki kiliahirishwa sababu ya Lissu kuumwa tumbo na siyo kuwa alikikwepa kama alivyodanganya mwanzo?
Kuna baadhi ya maswali lissu alishajibu, ukweli lissu kaweka wazi mapema sana hilo
 
Lissu amenyooka kama rula, nyeusi nyeusi...ndio maana ma ccm hayamtaki kwasabb hahongeki kudadek!!!.
Na ukijiona mambo yako ni mengi yanakona kona usije kujiroga ukawa na watu kama kina lisu itakula kwako mapema sana..
Hapo hakuna deal isee..
 
Ezekia Wenje amekiri mwenyewe kwamba kuna video recording ya mjadala wa tuhuma dhidi yake na wenzake kupokea pesa za Abduli na mama yake. Ni kweli. Walirekodi kikao hicho chote kwa video.

Ili kuondoa ubishi wa suala hili ninawashauri watoe video recording yote ya kikao hicho. Wasikate vipande vipande wala wasihariri chochote. Watoe video nzima ya mjadala huo ili wanachama na Watanzania wajue ni akina nani walituhumiwa kwa kupokea pesa ya Abduli na mama yake, ushahidi niliouwasilisha dhidi yao na wao wenyewe walijiteteaje!!!View attachment 3181258
Kweli sisi ni shithole country

Badala mjadala uwe
Ushahidi unatosheleza kumvindicate Abdul na rushwa Kisha afunguliwe mashtaka

Hivi ingekuwa nchi makini TAKUKURU si wangeisha mpeleka ABDUL na wenzake mahakamani

Mbona ushahidi uko wazi
 
Chadema yangu inateketea taratiiibu! Kama sio kiki, au kazi ya intelijensia ya chama, kuwapoteza maboya ccm, ni kitu harisi kabisa kinatokea, basi naiona njia ya kifo iliyopitiwa na nccr msgeuzi, cuf! Na hapo kuna mkono wa ccm na TISS,chadema kwishney
Hapo sio CHADEMA tu. Kumbuka Abdul ni nani.
 
Mtu asiye na akili timamu, ndio anaweza kuona maelezo ya wenje yamenyooka
Kwani wewe huoni wanao mshabikia wenje ni CCM na wanamshabiki ma kwa sababu ya wizi, jambo lolote ukiona linashabikiwa na CCM ujue ndani yake kuna wizi
 
Tundu Lissu haaminiki tena, maelezo ya Wenje yamenyooka sana.
Abdul anahangaika Ili Lissu alipwe pesa zake, Je yeye Abdul ananufaika na nini kwenye harakati zakufatilia mapesa ya Lissu?. Kama alivyosema Wenje?.
 
Ila Chadema mmeionyesha dunia kuwa nyie ni kikundi Cha wahuni wasio na malengo. Migogoro na minyukano ndani ya chama chenu kimeyapa MaCCM kutawala mpaka yachoke yenyewe. Pumbav zenu
 
Ezekia Wenje amekiri mwenyewe kwamba kuna video recording ya mjadala wa tuhuma dhidi yake na wenzake kupokea pesa za Abduli na mama yake. Ni kweli. Walirekodi kikao hicho chote kwa video.

Ili kuondoa ubishi wa suala hili ninawashauri watoe video recording yote ya kikao hicho. Wasikate vipande vipande wala wasihariri chochote. Watoe video nzima ya mjadala huo ili wanachama na Watanzania wajue ni akina nani walituhumiwa kwa kupokea pesa ya Abduli na mama yake, ushahidi niliouwasilisha dhidi yao na wao wenyewe walijiteteaje!!!View attachment 3181258
Lissu wakati anarekodiwa nayeye hakurekodi kuweka mizania sawa?
 
Utetezi wake hauwezi kushawishi watu.

Wenje anapinga madai ya kuhongwa kwa hoja nyepesi kuwa mbona anaendelea kuisema negative administration ya Samia.

This is weak argument
Sure,at the same time anaongea kirahisi tu eti nilikutana na Abdul kwenye sherehe nikaona atusaidie Lissu kulipwa hii error in argument kabisa na conclusion yake inaonyesha Abdul anafahamiana naye ila anamislead umma
 
Sasa hiyo hongo ilikuwa ya nini kama hakuna chochote kilichobadilika kutoka kwa hao wanodaiwa kuhongwa kumnufaisha muhongaji?!
Wewe kweli ni kipofu na hata mauaji yanayo endelea chadema uyaoni wewe unadhani hakuna watu wanao tumika ndani yake na kina abdul kufanikisha hayo mauaji ...kama Wenje ni damu damu na abdul mbona ajaonyesha kutumia huo uhusiano wao kuzuia mauaji wa watu wa chadema ambayo chadema inasema yanafanywa na serikali ya samia ...wenje na wengine ndani ya chadema wanatumika na serikali ya samia kama majasusi ya USA yaliyopo ndani ya makundi ya kigaidi bila ya magaidi wenzao kujua ...jasusi la Marekani likiwa ndani ya vikundi vya kigaidi ufanya ugaidi kamili ili lisijulikane kuwa ni jasusi
 
Lissu ameingia mkenge wa Diaspora. Infact hao diaspora walimuuguza sana tundu. Ameingizwa mkenge na yeye kwa kulewa sifa bila kusikia na kujua madhaifu yake akauvaa mkenge kichwa kichwa. Umewahi kuona diaspora hata mmoja akimkemea Msigwa? Msigwa yupo wapi sasa hivi?
Tulia Lissu Awanyooshe
 
Back
Top Bottom