SoNotorious
JF-Expert Member
- Sep 11, 2011
- 2,422
- 859
Pasco tangu UHURU bunge la Tanzania halijawahi kutunga sheria!!!!!! Lenyewe linajadili na kupitisha sheria zilizotungwa na serikali!!!!!
ni kweli
Pasco tangu UHURU bunge la Tanzania halijawahi kutunga sheria!!!!!! Lenyewe linajadili na kupitisha sheria zilizotungwa na serikali!!!!!
Maneno yaliyomfukuzisha Ibilisi peponi ni pale alipotamka neno Mimi umniumba kwa Moto (Naar) badala ya neno Mwangaza (Nur). Nina-refer Kitabu cha Koran, Sura ya 7:11-13.
Pia yamerudiwa maneno hayo katika Sura 38: 76
Asante sana kwa baraka za Eid. Ibilisi angetoka tu mbinguni, hata angesema Nuur bado angekamatwa kwa kiburi chengine, kama hayo maneno katika Isa: 14:4Asante sana Mkuu kwa mistari murua. Hata hivyo japo ni nje kidogo ya mada, naomba kuuliza: hivi Ibilisi angetamka vinginevyo, yaani Nur badala ya Naar, unadhani angesalimika? Kwa mistari uliyo-refer inaonekana kilichomtimua Ibilisi ni ile kujiona bora kuliko Adam aliyeumbwa kwa udongo regardless yeye (Ibilisi) aliumbwa kwa nini.
Katika Biblia kuna kisa, japo tofauti na hicho, lakini ndicho kilichomwondoa Ibilisi Mbinguni:
"Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka Mbinguni,
Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu;
Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano,
Katika pande za mwisho za kaskazini", Isa 14:13
"Nitapaa kupita vimo vya mawingu,
Nitafanana na Yeye aliye juu", Isa 14:14
Mistari hiyo na hasa huo nilio-underline ndio ulimtoa Ibilisi almaarufu kama Lusifa au Shetani au Mkuu wa Mapepo na Majini au Baba wa Uovu kutoka Mbinguni.
Eid Mubarak.
Mkuu Jogi,mkuu Pasco, huyu Ana Makinda si alichaguliwa na kuridhiwa na bunge? pamoja na uchafu wa chenge, tumeshuhudia bunge likimpitsha kuwa mwenyekiti wa kamati NYETI ya bunge?!!!! Nikubaalie japo mara hii tu kuwa, tatizo linalotumaliza ni zimwi CCM.
Veting pamoja na ccm ni sawa kunywa panadol kama tiba ya malaria!!!!!!
Tuivurumishe ccm, tuwashughulikie akina chenge & co. tutengeneze protocal za haki na wajibu kuwa mzegamzega mmoja, then veting itakuwa na mantiki.
Mkuu Jogi, 7. Japo CUF ni mke wa CCM kwa upande wa Zanzibar, hiyo ni "marriage of convinience", hivyo inavunjika wakati wowote "conveniences" zikimalizika, hivyo Chadema inacho kibarua kigumu cha kumtongoza huyu mke wa mtu kumhakikishia akikubali kutoka nje ya ndoa, yeye sasa hatakuwa mke tena, bali atageuka mume na 2015 ni yeye sasa ndie atageuka kidume na kumuoa huyo mume aliyenae sasa kwa sababu mume huyo ategeuzwa mke!.
8. Hakuna ubishi kuhusu nguvu ya CUF kule Zanzibar na Chadema itake isitake, ipende isipende, ili kujihakikishia njia
nyeupe ya kuwa mpangaji wa magogoni kwa 2015, ni lazima ikubali kuisupport ya CUF kwa upande Zanzibar ili CUF
nao wakubali kuisupport Chadema huku bara!. Chadema wakae chini na CUF, waainishe maeneo ya strong holds za
kila mmoja na kuachiana maeneo hayo ili 2015, kuepuka kumfaidisha kunguru kwa vita vya panzi!.
Wasalaam.
Pasco.
Nadhani majaji wote walioteuliwa na Jakaya ni feki ima wameteuliwa kwa kufuata ushikaji udini ushirika na upuuzi mwingine. Msishangae yule mwizi wa EPA Mwanaidi Majaar siku moja akazawadiwa ujaji baada ya kuuchoka ubalozi au kustukiwa na nchi anakowakilisha maslahi ya bosi wake. Sitashangaa siku moja Andrew Chenge au Chikawe kuzawadia ujaji. Siku hizi ujaji ni si big deal anymore, ni ukuadi wa kawaida wa kuuza na kudhalilisha haki. Nani mara hii kasahau majaji kama Augustine Shangwa aliyeteuliwa baada ya kunyonga kesi ya Mrema iliyodai Mkapa alihongwa shilingi 500,000,000? Hao ndiyo majaji wetu wa vodafaster.
kuna taarifa kwamba pamoja na mambo mengine mahakama inatoa ushirikiano kwa lissu ili kufichua urojo wa mkuu.
Serikali yatuma watu wake kununua nakala za jamhuri katika mitaa ya posta.
Watu wapiga photocopy nakala ya jamhuri ili kuutafuta ukweli.