Mandingo
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 5,964
- 7,862
Aliyemfanyia LLM hata mimi namfahamu
Muweke hapa tumjue!
Aliyemfanyia LLM hata mimi namfahamu
Hapo kwenye blue ninakubaliana na wewe kuwa Lissu hakuwa makini wa kusahihisha kile alichokiandika, lakini kukosea jina la mhusika hakumfanyi mhusika aliyekusudiwa kuepukana na shutuma. Ni kweli sio Moshi ni Mushi, lakini Sekela itabaki pale pale ispokuwa tu wote wawili Sekela Cyril Mushi na Sekela Cyril Moshi wawe ni majaji
Hili la uzoefu na usomi mzuri, hakumfanyi mtu asiwe na makosa kwa vigezo hivyo tu. Kama utaangalia, mafisadi na wafanya madudu wengi ni watu wenye elimu na uzoefu mkubwa, na zaidi, mtu anaweza kuwa na sifa zote hizo pamoja na uaminifu mkubwa, lakini siku akiteleza na kufanya madudu, anaagaliwa kosa lake la sasa na sio uadilifu wake wa nyuma. Hata Ibilisi kabla ya kulaaniwa na Mungu alikuwa mcha Mungu mzuri, lakini kwa neno moja tu aliposema ameumbwa kwa Moto badal ya Mwanga, alifukuzwa toka peponi.
...
Hili la uzoefu na usomi mzuri, hakumfanyi mtu asiwe na makosa kwa vigezo hivyo tu. Kama utaangalia, mafisadi na wafanya madudu wengi ni watu wenye elimu na uzoefu mkubwa, na zaidi, mtu anaweza kuwa na sifa zote hizo pamoja na uaminifu mkubwa, lakini siku akiteleza na kufanya madudu, anaagaliwa kosa lake la sasa na sio uadilifu wake wa nyuma. Hata Ibilisi kabla ya kulaaniwa na Mungu alikuwa mcha Mungu mzuri, lakini kwa neno moja tu aliposema ameumbwa kwa Moto badal ya Mwanga, alifukuzwa toka peponi.
kamwe msinifananishe mimi na asenga abubakar mpare na asenga wa morogoro tofaut sana ;uhuu ndio ukweli mliutoa bila kujadili acheni kula mavi ili mpate akili nzuri.mavi si chakula,yana haribu akili.
Watu wengine bana, wewe unajaribu kujibu hoja kwa kutumia mipasho? Wewe mpuuzi sana, tena sana.
Maneno yaliyomfukuzisha Ibilisi peponi ni pale alipotamka neno Mimi umniumba kwa Moto (Naar) badala ya neno Mwangaza (Nur). Nina-refer Kitabu cha Koran, Sura ya 7:11-13.Mkuu hapo kwenye red tujuze tafadhali. Una-refer maandiko au kitabu gani? Hii ni mpya kwangu.
11. Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu.
12. Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha? Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa Moto, naye umemuumba kwa udongo.
13. Akasema: Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe u miongoni mwa walio duni.
.76. Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa Moto, na yeye umemuumba kwa udongo
RIPOTI YA TUNDU LISSU NA KESI MAARUFU YA KIBALAGHASHIA
Hivi karibuni, Mheshimiwa Tundu Lissu alisoma Bungeni ripoti yake ya utetezi ambayo ameipeleka kwa kamati ya maadili ya Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ambapo katika ripoti yake hiyo Mheshimiwa Lissu amebainisha mambo mbalimbali ambayo mengi ni tuhuma nzito dhidi ya Majaji wa Mahakama Kuu, tuhuma ambazo tayari zimeshasambazwa kwa umma hata kabla hazijajadiliwa na kamati husika ya maadili ya Bunge,kwa kufanya hivyo ni wazi kuwa, Majaji waliotajwa wamehukumiwa hata kabla tuhuma hizo hazijathibitika, lakini pia mhimili nzima wa Mahakama na Idara zake zimehukumiwa na kufanywa ionekane kuwa Mahakama nchini zinafanya shughuli zake kwa namna ya hovyo na kwa maana hiyo, ni wazi imani ya watu katika chombo hiki muhimu cha kutoa haki itashuka kwa jamii.
Ingwa Mheshimiwa Lissu kwa makusudio,ama kwa makosa ya kibinadamu ama kutokana na hulka yake ya kukurupuka ameainisha vipengele vingi ambavyo HAVIKO SAHIHI ama vinahitaji ufafanuzi wa kina, moja ya vipengele hivyo;
Katika Ripoti hiyo, inataja kuwa UAMUZI wa Jaji Kiongozi kumhamisha hakimu kwa maamuzi asiyokubaliana nayo UNATUMIKA na kukubaliwa kama HUKUMU ama ADHABU kwa Hakimu huyo. Ripoti ya Mheshimiwa TUNDU inaonesha kwamba maamuzi ambayo Jaji kiongozi hakukubaliana nayo yanahusu kesi aliyoiita maarufu ya kibalaghashia Kumbukumbu zangu zinanionyesha kwamba kesi hiyo iliwahi kuripotiwa kwa mshangao katika magazeti kadhaa, kwamba, hakimu mmoja amehukumu mtu kwenda jela kwa kuvaa kibalaghashia mahakamani.
Kwa nchi kama Tanzania ambako vazi la kibalaghashia ni vazi rasmi katika baadhi ya dini, haikutegemewa kwa hakimu huru na mwenye busara kumfunga mtu kwa kuvaa kibalaghashia mahakamani. Kwa namna suala hilo lilivyovuta hisia za watu wengi hapa nchini na mbaya zaidi HISIA ZA UDINI, nisingeshangaa hata kidogo kama hakimu kama huyo angechukuliwa hatua yeyote ya kinidhamu achilia mbali kuhamishwa ambako Mhe. TUNDU LISSU nakulalamikia na kuonesha kuwa JAJI KIONGOZI amekosea na alimuonea Hakimu huyo.
Mahakama kama chombo cha kutoa haki kinapaswa kujiweka katika hali ambayo kila mtu atakiona kama chombo huru kisichokuwa na muegemeo wowote wa KISIASA, KIDINI AU KIKABILA. Maamuzi mabovu kama hayo hayakupaswa kutolewa na chombo kama Mahakama. Najiuliza TUNDU LISSU analenga nini katika kutetea hili.???
Lakini pia, nijuavyo ni kuwa uhamisho kwa mahakimu na majaji ni utaratibu wa kawaida wa kazi na wala hamna hakimu yeyote mwenye hatimiliki ya kuwa Dar es salaam ama kufanya kazi Dar. Wala mahakimu walioko mikoani hawako huko kwa sababu ya adhabu wala mahakimu waliopo Dar es salaam hawako Dar kwa sababu ni weledi zaidi ya walio mikoani.
Udhaifu huu wa hoja ya Mhe. Tundu Lissu unaibua Upya HISIA ZA UDINI zilizojitokeza hapo kabla wakati wa kesi hiyo. Pia, Lissu analeta mkanganyiko mkubwa baada ya Ripoti yake hiyo ambayo inachukua sura ya kutaka kulifanya Bunge ni chombo cha kuisimamia mahakama, na hivyo kupoteza tafsir na mantiki ya mihimili mitatu ya serikali ya Tanzania. Kwa mujibu wa ibara ya 107 A, mamlaka ya kufasir sheria na kutoa haki yako mikononi mwa mahakama. Hakuna hata sehemu moja katika Katiba ambapo Bunge limepewa mamlaka yoyote ya kuisimamia na kuishauri mahakama.
Nafasi ya Bunge kuirekebisha mahakama katika mfumo wa checks and balance ni kwa njia ya kutunga sheria TU. Kwa kitendo cha kuisoma ripoti hiyo katika hadhara ya Bunge na kulitumia Bunge kuidhalilisha mahakama na majaji wake ni wazi Mhe. TUNDU analenga kulichonganisha Bunge na Mahakama.
Kiukweli hapa Tanzania, hatuna kabisa "The doctrine of Separation of powers" kilichopo ni kiini macho, na alichokifanya Tundu Lissu ni kuuthibitisha tuu udhaifu huu!.
Kazi ya bunge zaidi ya kutunga sheria, pia ni kuisimamia serikali, na kuithibiti mahakama!. Kazi ya Mahakama ni kutafsiri sheria, kuithibiti serikali na kulidhibiti bunge, na kazi ya serikali ni to provide kwa bunge na mahakama na kuendesha nchi kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na bunge, na kusimamiwa na mahakama!. Hivyo kila chombo ni big brother aki watch over and above mhimili mwingine ili kujenga hizo checks and balance, lakini kwa Tanzania ni shaghala bagala, Serikali ndio kila kitu, ikifuatiwa na bunge na mwisho ni mahakama!.
Rais wetu ni sehemu ya bunge, anaweza kulivunjilia mbali bunge as he pleases!, bunge likishatunga sheria, sheria hiyo haiwi sheria mpaka rais aikubali, na akiikataa bunge halina uwezo wa kufanya lolote, kwa sababu rais anaweza kulivunjilia mbali anytime!. Hivyo mbele ya rais, bunge si lolote sii chochote!.
Rais ndiye anayemteua Jaji Mkuu, bila any imput toka bunge, mahakama ikitoa capital punishment, adhabu hiyo haitekelezwi mpaka rais airidhie, rais anaweza kuamua kutotekeleza adhabu yoyote, kuwasamehe wafunga wowote, na kwa Tanzania hata kuzuia wahalifu kama ile mijizi ya EPA kupewa msamaha bila kufikishwa mahakamani ambapo ni uvunjaji wa katiba ya JMT, lakini hakuna mwenye uwezo wa kumfanya chochote rais, hivyo mbele ya rais, mahakama sii lolote, sii chochote!.
Kwa mtaji huo, Lissu is very right, bunge linapaswa kuidhibiti mahakama na ilipaswa jaji mkuu aridhiwe na bunge kama anavyoridhiwa waziri mkuu!. Bunge pia ndilo lilipaswa liwe supreme kwa sababu ndilo lililochaguliwa na watu, na sio serikali!. Hapa kwetu serikali ndio kila kitu, rais wetu ni Alfa na Omega!.
Pasco.
..nilipoisoma makala ya
Tundu Lissu akiitaja kesi ya "kibaragashia" I knew this was coming.
..Tundu Lissu alitakiwa awe makini zaidi na zaidi na kuielewa hadhira
anayo-deal nayo.
..ukiachilia suala la "kibaragashia," naamini hoja ya Tundu Lissu imejaa
madai mazito na serikali inapaswa kuyafanyia kazi.
..Tundu Lissu hajaidhalilisha mahakama. Raisi ndiye ameidhalilisha
mahakama yetu kwa kuteua majaji wenye maadili na rekodi zenye
mawaa.
aidha wewe na tundu lisu huwa mnalewa wote pale chako nichako hadi siku ile alitaka kuvua nguo na kupanda kwenye meza huwezi sapoti sababu zake za kiwivu wa kikekwahiyo hapa unaongelea issue moja tu, KIBALAGHASHIA. Huna jingine.
Kati ya yoooote aliyoyasema Tundu Lisu, wewe umeoba Kibalaghashia tu baaaasi! Na umetumia mfanp huo kwa maoni na mtazamo wako wa kidini kuona kwamba Lisu amekosea saaana kuhusu madai ya ukiukaji wa taratibu katika kuteua majaji?!
Akili mchuzi wa nazi.