Ndiyo shida kubwa ya Lisu, hajui kabisa kuzungumzia shida za wananchi masikini wa kijijini,
Huwezi kumsikia Lisu akizungumzia uchumi, ajira, barabara, maji yeye ni kuzungumzia mambo yanayomhusu yeye tu yani uchaguzi.
John Heche anaeleweka haraka kwa wananchi kwa sababu anazungumza namna atakavyotatua shida zao na siyo kuzungumzia shida za wanasiasa tu
Kwanza hongera sana kwa kuwa kumbe unafuatilia kwa karibu na umakini ziara na shule ya
NO REFORMS, NO ELECTION inayotolewa kwetu sisi wananchi na miamba hii miwili Tundu Lissu na John Heche. Kama hiumwelewi mmoja wapo, hiyo ni shida yako binafsi. Wengine tunawaelewa wote vizuri sana kuliko sana yenyewe....
Lakini nakuonea huruma kweli kwa sababu ni mjinga na mpumbavu pekee asiyeweza kumwelewa Tundu Lissu jinsi anavyowasilisha elimu hii ya kaulimbiu ya NO REFORMS NO ELECTION kwa lugha rahisi kueleweka kwa kila mtu hata ambaye hakusoma shule kabisa, akitumia takwimu za kiuchaguzi za wakazi wa eneo/mji anapofanyia mkutano wake ktk ku - justify kila hoja...
Tundu Lissu kubwa anayoifanya ni kuelezea na kuufahamisha umma uhusiano uliopo kati ya KATIBA na MFUMO MBOVU WA UCHAGUZI na jinsi unavyoathiri maisha yao ya kila siku...
Anasema ili nchi iendelee, iondokane na umasikini inahitaji mambo manne: WATU, ARDHI, UONGOZI BORA na SIASA SAFI....
Nchi yetu ya Tanzania ina WATU zaidi ya 64,000,000 na ARDHI kubwa ya kutosha yenye kila kitu juu yake (maziwa, bahari, mito, misitu, madini, mbuga za wanyama na mali asili zingine nyingi). Tatizo la nchi yetu ni kukosa mambo mawili ya mwisho: UONGOZI BORA na SIASA SAFI....
VIONGOZI BORA wanatokana na SIASA SAFI. Nchi ikiwa na SIASA CHAFU na hovyo kama hizi za CCM kutumia mifumo mibaya ya uchaguzi kujipendelea, hakika tutakuwa na UONGOZI MBOVU wenye viongozi vilaza, wajinga, wabinafsi, wezi, mafisadi, wafiraji, walafi wa madaraka wasioweza kutumia fursa ya baraka utajiri wa maliasili iliyonayo nchi yetu kuondoa matatizo ya kijamii ya wananchi kama ambavyo CCM yenu imeshindwa kwa miaka zaidi ya 64 sasa...
Katika mfumo na msingi huu, unawezaje kuondoa shida za watu iwapo tatizo kubwa likiwa ni viongozi wenyewe....?
Na hii ndiyo maana sasa kwa hali ilivyo sasa, nakubaliana kabisa na CHADEMA ya Tundu Lissu kuwa ili shida za nchi yetu ziishe au zipungue, tunahitaji kubadilisha mfumo wetu wa utawala kwa kubadilisha mfumo wa uchaguzi unaoingiza viongozi madarakani ili tuwe na mfumo unatuwezesha wananchi kuchagua viongozi wanaowataka kwa UHURU, HAKI na UWAZI tofauti na ilivyo sasa ambapo CCM hujiweka wenyewe madarakani. Na hiki ndicho chanzo cha shida za wananchi kutotatuliwa na ndiyo msingi wa kuanzishwa kwa movement hii ya
====NO REFORMS NO ELECTION====
Kwa hiyo, ndugu
Maswa Yetu ni vyema ukaelewa kuwa shida zote za nchi hii na wananchi wake iwe ni
huduma ya maji, umeme, barabara mbovu, uchumi mbovu, maisha magumu ya kiuchumi ya wananchi, huduma mbovu za afya, elimu, usafiri nk nk msingi au shina na mizizi yake iko ktk KATIBA MBOVU iliyojenga MFUMO USIO HAKI WA CHAGUZI ZETU katika nchi kiasi cha kutupatia viongozi wa hovyo, wezi, mafisadi, wasiowajibika kwa wananchi na wasio na uwezo wwa kubuni na kutatua changamoto za wananchi na nchi hii...?
Kama hujui haya, basi sitakosea kabisa kusema kuwa, kumbe wewe ni mjinga na mpumbavu kwa wakati mmoja.....!
Haiwezekani watu tunaodhani mna elimu na ufahamu wa kuelewa mambo haya kwa haraka ili kuelimisha wengine na kusukuma mabadiliko ya mfumo wa utawala wa nchi yetu ili tuepukane kuwa na viongozi mizigo tu unakuwa hujui au unajifanya hujui na unatumia ujinga wako na kutoelewa kwako kueneza ujinga huu kwa watu masikini wa nchi hii...
Shame on you brother...!