Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Wakuu,
Chama cha Madereva wa Malori kilitoa tamko ikiwa mwenzao hajapatikana ndani ya siku 2 kuanzia Jumapili wangefanya mgomo, hii ni baada ya mwenzao kudaiwa kuchukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa polisi, ambapo jitihada za kumtafuta katika vituo mbalimbali hazikuzaa matunda.
Baada ya tamko hilo polisi ndio wametoka kusema wanamshikilia🤣🤣🤣 yaani Polisi wamekuwa WAHUNI kuliko wale aliowasema Polepole. Mpaka muone watu wanataka kukinukisha ndio mnatoa pua zenu, kazi kwelikweli.
====
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Godlove Materu hajulikani alipo baada ya kukamatwa na watu wasiojulikana.
Godlove Materu (45), mkazi wa Chapwa, Mji wa Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe, alikamatwa na Askari Polisi na siyo na watu wasiojulikana, na anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa tuhuma za jinai zinazomkabili.
Mtuhumiwa alipanga na kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Tunduma na viunga vyake.
Uchunguzi umekamilika na hatua zingine za kisheria zinafuata.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuzipuuza taarifa zote zinazosambazwa bila uthibitisho kutoka kwa mamlaka au vyanzo rasmi.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Songwe
Pia soma Madereva wa malori waipa Serikali siku 2 mwenzao apatikane, la sivyo watagoma

TAARIFA KWA UMMA
KUKAMATWA KWA GODLOVE MATERU-TUNDUMA-SONGWE.