Tunduma: Polisi wakiri kumkamata Dereva wa Malori. Yadaiwa alipanga kufanya uhalifu

Kamanda wa Polisi tafadhali usikubali ofisi yako kuchafuliwa na wahuni wachache, toa na orodha ya majina ya ndugu walioambatana na mtuhumiwa wakati anakamatwa, onyesha logbook aliyosaini wakati anaingizwa sero, taja jina la mwenyekiti aliyeshuhudia wakati mtuhumiwa anakamatwa na mwisho kabisa weka hadharani majina ya ndugu aliyeleta chakula siku ya kwanza asubuhi, mchana, jioni hadi siku hao "wahuni" wanafanya press na useme kabisa "hakuna ndugu/jamaa hata mmoja alifanya juhudi za kuomba dhamana"
******* hawawezi kufuata hizo sheria mwendo kufanya kazi km wapo kwenye vijiwe fulani hivi, hayo yote uliyoyataja hawajafanya hata moja sanasana walikua wanaelekea kumuua
 
Wakuu,

Chama cha Madereva wa Malori kilitoa tamko ikiwa mwenzao hajapatikana ndani ya siku 2 kuanzia Jumapili wangefanya mgomo, hii ni baada ya mwenzao kudaiwa kuchukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa polisi, ambapo jitihada za kumtafuta katika vituo mbalimbali hazikuzaa matunda.

Baada ya tamko hilo polisi ndio wametoka kusema wanamshikilia🤣🤣🤣 yaani Polisi wamekuwa WAHUNI kuliko wale aliowasema Polepole. Mpaka muone watu wanataka kukinukisha ndio mnatoa pua zenu, kazi kwelikweli.

====

TAARIFA KWA UMMA

KUKAMATWA KWA GODLOVE MATERU-TUNDUMA-SONGWE.
​

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Godlove Materu hajulikani alipo baada ya kukamatwa na watu wasiojulikana.

Godlove Materu (45), mkazi wa Chapwa, Mji wa Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe, alikamatwa na Askari Polisi na siyo na watu wasiojulikana, na anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa tuhuma za jinai zinazomkabili.

Mtuhumiwa alipanga na kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Tunduma na viunga vyake.

Uchunguzi umekamilika na hatua zingine za kisheria zinafuata.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuzipuuza taarifa zote zinazosambazwa bila uthibitisho kutoka kwa mamlaka au vyanzo rasmi.

Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Songwe

View attachment 3541316
Dah! Kipindi hiki si kizuri kukamatwa kabisa. Kama watu hawakukufatilia ipasavyo basi ujue ndo kwa heri. Nasikia wanakawaida ya kuwasajiri watuhumiwa kwa jina tofauti na halisia so ndugu wakija kukutafuta wanapewa kitabu cha orodha ya majina ya waliokamatwa unakuta jina lako haliko kumbe wamekuandika John Marwa badala ya jina lako halisi la George James ili tu ndugu na jamaa wahangaike kila kituo kukutafita na kila kituo unakuta wanasema hawajapokea mtu wa jina kama hilo ila inakuwa mtuhumiwa yuko kituo hikohiko ila kabadirishwa jina kwa maksudi kabisa.
 
Ilitosha watu wangekuwa wameachia madaraka
Nchi zetu hasa za Africa hatunaga utamaduni huo wakuachia ngazi pindi kiongozi anapokosea cause tunauroho sana wa madaraka na madaraka kwetu ni kama ajira na nafasi yakujitajirisha.
Wangekuwa wawajibikaji tungeona Bibi kizi akiachia ngazi kwa tukio la Oct29 pia hata Mangungu tungeona anaachia ngazi ya uenyekiti Simba pale ila ametuganda wana Simba hata akipigwa mitama yumo tu😆😆😆
 
Wakuu,

Chama cha Madereva wa Malori kilitoa tamko ikiwa mwenzao hajapatikana ndani ya siku 2 kuanzia Jumapili wangefanya mgomo, hii ni baada ya mwenzao kudaiwa kuchukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa polisi, ambapo jitihada za kumtafuta katika vituo mbalimbali hazikuzaa matunda.

Baada ya tamko hilo polisi ndio wametoka kusema wanamshikilia🤣🤣🤣 yaani Polisi wamekuwa WAHUNI kuliko wale aliowasema Polepole. Mpaka muone watu wanataka kukinukisha ndio mnatoa pua zenu, kazi kwelikweli.

====

TAARIFA KWA UMMA

KUKAMATWA KWA GODLOVE MATERU-TUNDUMA-SONGWE.
​

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Godlove Materu hajulikani alipo baada ya kukamatwa na watu wasiojulikana.

Godlove Materu (45), mkazi wa Chapwa, Mji wa Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe, alikamatwa na Askari Polisi na siyo na watu wasiojulikana, na anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kwa tuhuma za jinai zinazomkabili.

Mtuhumiwa alipanga na kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Tunduma na viunga vyake.

Uchunguzi umekamilika na hatua zingine za kisheria zinafuata.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa wito kwa wananchi kuendelea kuzipuuza taarifa zote zinazosambazwa bila uthibitisho kutoka kwa mamlaka au vyanzo rasmi.

Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Songwe

View attachment 3541316
"Alipanga kufanya uhalifu"
Polisi nao wamekuwa wabashiri...wanabet na uhuru wa wadanganyika!

Taasisi ya kwanza kuifumua na kuiunda kisasa ni hii,frankly ni kama hawajui PGO!
 
Kamanda wa Polisi tafadhali usikubali ofisi yako kuchafuliwa na wahuni wachache, toa na orodha ya majina ya ndugu walioambatana na mtuhumiwa wakati anakamatwa, onyesha logbook aliyosaini wakati anaingizwa sero, taja jina la mwenyekiti aliyeshuhudia wakati mtuhumiwa anakamatwa na mwisho kabisa weka hadharani majina ya ndugu aliyeleta chakula siku ya kwanza asubuhi, mchana, jioni hadi siku hao "wahuni" wanafanya press na useme kabisa "hakuna ndugu/jamaa hata mmoja alifanya juhudi za kuomba dhamana"
Hayo yote yakifanyika jua litazamia mashariki na magufuli atafufuka
 
Raia wanaishi kama ndege hii sio sawa yaani mtu anawaza kumyakua harafu anakaa kimya mpaka ikitokea kitu ndio wanatoa tamko wanakosea sana sana kwa kutengeneza uadui usio wa lazima na Wananchi sijui kama huwa wanawaza vizuri kweli..
 
Kulikuwa na shida gani iwapo wangelifuata procedures za ukamataji kwa mujibu wa sheria, kukawa na mwenyekiti S/M pale, ita madereva wenzake, Polisi jitambulishe nk nk, kungelitokea huo mtanziko kweli?

Kwa nini Polisi sasa hivi wanapenda sana kutengeneza taharuki?
Jeshi letu linashangaza sana kiukweli, ni kama weledi wameuweka pembeni
 
Tatizo la nchi yetu, ni serikali kuwa msimamizi mkuu wa sheria na ndio mvunja sheria namba moja.

Serikali inayoshindwa kujiheshimu, ni majanga kwa wananchi wake!
 
Kulikuwa na shida gani iwapo wangelifuata procedures za ukamataji kwa mujibu wa sheria, kukawa na mwenyekiti S/M pale, ita madereva wenzake, Polisi jitambulishe nk nk, kungelitokea huo mtanziko kweli?

Kwa nini Polisi sasa hivi wanapenda sana kutengeneza taharuki?
Kwenye polisi kukamata mhalifu hakuna Sheria ya kuwaita wafanyakazi wenzie bali uongozi wa mtaa tu
 
Back
Top Bottom