Mugabe one
JF-Expert Member
- Nov 15, 2016
- 2,327
- 1,683
Wana CCM kuweni na akili kama hamna akili kuweni na huruma! Hili sio jambo la kufurahia wala kushangilia.Unyang'anyi kwa kutumia Silaha Poleni CHADEMA na Jamii ya Vibaka wenzake.
Soon mtapata majibu.Karibu tunakusubiri
Sio polisi tu, kuna ofisi za CCM, nyumba zao na Mali zao. Tunaanza na izo pia then tunaamia za serikaliWananchi watoe mfano inapokanyagwa haki iwe na polisi au nani ili wajifunze ,tuache woga hawataacha . Kwa kumalizia hebu niwekeeni majina yote ya polisi na maofisa waliohusika tuwashtakie kwa Mungu tumechoka ata radi zifanye kazi.
Mmejua kuwa ni waalifu sasaivi kipindi cha uchaguzi eeeh???? Mtajua hamjui mwaka huu!!! Subirini muoneMnawapitisha wahalifu kugombea na mmnataka NEC ndio iwakinge kwa uhalifu wao sababu tu ' wanagombea nafasi yeyote ile uchaguzi mkuu' , haikubaliki, mhalifu ni mhalifu.
Anavunja sheria anavuja sheria na sio kisingizio kuwa anagombea Urais, Ubunge , Udiwani. Wenye kutafuta kupitia njia hiyo kujisafisha wasikubaliwe kabisa.
Tunaiwasha sasaKwani wewe huwezi kuiwasha hiyo sigara ?🤔
Wananchi wenyewe tumeshaamua hatua za kuchukua. Hatusubiri Chadema, CCM watajuta mwaka huuChadema na upinzani kama hamuwezi kuchukua hatua achaneni na siasa mjiunge na CCM kulia lia hakuwezi kuwasaidia... Yaani mnataka kushika dola kwa msaada wa CCM? yaani CCM ndio iwasaidie kwenye harakati zenu za kuchukua dola?.. acheno utoto nyie.
Asante sana.Sasa tuna uhakika na tunachokijadili
Kabisa mkuu nimekuelewa sanaHawawezi kuona makosa yao wakati Viongozi wa Dini wameamua kuungana na watesi na kushangilia dhulma kwa binadamu wenzao kwa sababu tu ya mahaba ya kivyama na Kikabila.
Katiba iliyopo inababisha nchi kuwa na vitendo vya kikatili kwa kisingizio vya kulinda amani. Amani imekua ni jambo la kutumia nguvu kuwasababisha wenye uroho na ulevi wa madaraka kuendelea kubaki kwenye madaraka.
Tatizo kubwa ni MTU mmoja kuwa na madaraka makubwa ya kuteua hata watu wa kabila lake tuu au dini yake tuu au ukanda wake tuu bila kuulizwa au kuwajibishwa kikatiba.
Katiba imetoa mwanya mkubwa sana kwenye uteuzi. Ndio maana MTU kama Sabaya bado yupo Kwenye Ofisi ya umma inayogharamikiwa na asilimia kubwa sana kwa kodi ya wapinzani wa Ukanda huo. Yupo pale kuwaumiza walipa kodi kwa sababu tu ya kulinda kiti chake kinachompa chakula.
Hali ikiendelea hivi kwa vyama vya siasa kufanya Uhuni wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa vyombo vya dola wanaolinda maslahi yao kikanda au kidini au kikabila mwishowe watapoteza mvuto kwa jamii.
Afrika bado kuba Ukabila ,Udini, ukanda na ushabiki wa kivyama mbali kabisa na Utaifa na uzalendo wa kweli. Ili kuondoa udini ,ukabila,ukanda na uvyama ni lazima watu wafanye siasa kwa Haki na usawa na pia kujenga utaifa na kuondoa huu uhunu. Ukichunguza vizuri utagundua kuwa hata ukatili na ubabe unafanywa kwa misingi hiyo hiyo ya kulinda hayo. Na wanayoyafanya wanakua na wazo hilo hilo kuwa sasa ni zamu ya dini yetu ,kabila letu ,ukanda wetu n.k watatukoma.
Waafrika tubadilike na tukatae kugawanywa na watu wachache walioahidiwa madaraka au wanaolinda madaraka yao na familia zao kwa mgongo wa zamu yetu.
Lakini hawasikii.Tena akaiambia "TOSHEKENI NA MISHAHARA YENU" mijinga sana hiyo mijitu
Kuna ushahidi wowote au ni kubambikizana tu? Kwa mfano baadaye ikionekana kuwa polisi hawakuwa na ushahdi watawalipa fidia ya usumbufu (reparation)? Sijui sheria za usumbufu hapa kwetu zinasemaje, ila kipindi hiki cha uchaguzi iwapo itaonekana hawakuwa na kosa lolote wanaweza kudai fidia ya kuwaharibia chance zao kuwa madiwani kwa miaka mitano ijayo.Mgombea Udiwani wa CHADEMA Kata ya Majengo mjini Tunduma Boniface Mwakabanje ambae alikuwa anashikiliwa kwa ishu ya uraia, leo mchana amefikishwa Mahakamani na kupewa kesi ya 'Armed robbery' shitaka hili halina dhamana so kapelekwa magereza.
Uchaguzi 2020 - Tunduma yazuka vurugu na mabomu ya machozi yapigwa na polisi
View attachment 1546927
Mgombea Udiwani wa Chadema Kata ya Majengo mjini Tunduma Boniface Mwakabanje
====
Kufuatia kuwepo kwa matendo na matukio yanayoashiria kuwepo kwa mipango ya kuhujumu, kuharibu na kuvuruga Uchaguzi Mkuu, mwezi Oktoba, 2020, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinatamka ifuatavyo, kuhusu yanayoendelea kwenye maeneo hayo;
1. Tunduma
Tunaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua hatua za haraka dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa Kanuni na Maadili yq Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, vinavyofanywa na mamlaka za kiserikali ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe na Mkuu wa Wilaya ya Momba, kuratibu mipango ya kuhujumu wagombea ubunge na udiwani wa Chadema wasiweze kurejesha fomu.
Mipango hiyo tayari imeanza kutekelezwa ambapo Mgombea wa Udiwani Kata ya Majengo, Boniphace Mwakanjabe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Tunduma, baada ya kukamatwa jana, leo amefikishwa mahakamani akibambikiwa tuhuma za uvamizi wa kutumia silaha, kwenye kesi Na. 125/2020.
Wagombea wengine wa udiwani; Moses Mshami (Muungano), Florini Mwalongo (Maporomoko), na Hosea Kibwana (Kiloleni) wanatafutwa na polisi kwa ajili ya kuunganishwa kwenye kesi hiyo.
Aidha, kutokana na mipango hiyo yenye lengo la kuharibu uchaguzi, polisi wamemkamata Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Songwe, Stella Fiao ambaye amefunguliwa kesi Na. 126/2020 na kubambikiwa tuhuma za kutokuwa raia wa Tanzania, huku viongozi wengine wa Chadema, akiwemo Mwenyekiti wa Mkoa Ndugu Issakwisa Thobias Lupembe (Mwenyekiti wa Mkoa), Hamza Hussen Mpongolela, Kiswigo Mwakabanje, Eliah Mwabukusi, Mosses Ambilikile Mshani, Frowini Kasiani Mwalongo, na Osiah Anthony Kibwana, wakiendelea kusakwa ili waunganishwe kwenye kesi Na. 125/2020.
2. Masasi-Ndanda
Jeshi la Polisi leo majira ya asubuhi lilimkamata Mgombea wa Ubunge Jimbo la Ndanda, Castor Joseph Mmuni kwa namna ambayo ni kinyume cha utaratibu wa kisheria, kwa tuhuma ambazo hazijajulikana wazi, ambapo awali alivamiwa, kukamatwa kuwekwa kwa nguvu ndani ya gari na kutoweka kabla haijabainika kuwa anashikiliwa Kituo cha Polisi mjini Masasi.
3. Ruangwa;
Hadi sasa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ruangwa ameendelea kumnyima fomu Mgombea Ubunge wa Chadema Edgar Malimus Fakili, huku vitisho dhidi yake na wagombea wengine vikiendelea sambamba na vile wanavyopewa Viongozi wa Chama, wakitishiwa usalama na maisha yao kwa sababu ya Chadema kuweka wagombea ubunge na udiwani katika jimbo analogombea Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa. Watu wasiojulikana wamemfuata Mgombea Udiwani Kata ya Nandagala, Said Mnundumi ambaye ni mtu mwenye ulemavu, wakimtisha kuwa hatakuwa salama iwapo atarejesha fomu zake ili ateuliwe kugombea.
4. Morogoro Kusini (Morogoro DC)
Katika Jimbo la Morogoro Kusini, Morogoro DC, Msimamizi wa Uchaguzi naye ameendelea kumnyima fomu ya kugombea Mgombea wa Chadema John Mwenegoha, kinyume kabisa na taratibu zinazosimamia uchaguzi.
Hitimisho
Matendo na matukio hayo si tu yanahatarisha amani na usalama, bali pia yanahatarisha mstakabali wa uchaguzi wenyewe katika maeneo mahalia na Uchaguzi Mkuu kwa ujumla wake. NEC haipaswi kukaa kimya. Katika mazingira hayo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatakiwa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha wagombea wa Chadema wanapata fomu, wanarejesha fomu na wanateuliwa ili wakashindane kwenye sanduku la kura. Ukimya wa NEC utatafsiriwa kuwa ni kubariki na kuwa sehemu ya uvurugaji na uharibifu wa uchaguzi.
Imetolewa leo Agosti 24, 2020 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Chadema
Usiseme subirini muone. Macho yetu ni mazima. Kama kuna giza tuwashe taa.Mmejua kuwa ni waalifu sasaivi kipindi cha uchaguzi eeeh???? Mtajua hamjui mwaka huu!!! Subirini muone
Endeleeni na kejeli zenu. Majibu mtayapata soonUsiseme subirini muone. Macho yetu ni mazima. Kama kuna giza tuwashe taa.
Tabia ya mtoto kumwambia mtu mzima nitakuchapa ACHA. Utapata kipigo cha paka mwizi.
We usiseme "tunaiwasha", sema utaiwasha wewe na ufanye tuone, usiishie kubweka tu hapa jf kwenye fake IDs.Tunaiwasha sasa
Subiri mtaonaWe usiseme "tunaiwasha", sema utaiwasha wewe na ufanye tuone, usiishie kubweka tu hapa jf kwenye fake IDs.