Uchaguzi 2020 Tunduma yazuka vurugu na mabomu ya machozi yapigwa na polisi

Uchaguzi 2020 Tunduma yazuka vurugu na mabomu ya machozi yapigwa na polisi

Together TunawakilishaHome

RPC akanusha kumkamata M/Kiti wa CHADEMA Tunduma
Primary tabs
JUMATATU , 24TH AUG , 2020
NA MWANDISHI WETU
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limekanusha taarifa za kumkamata kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Tunduma Boniface Mwakabanje, kama ilivyoandikwa mitandaoni na kwamba kama kuna mtu ana namba zake basi ampigie ili kujua kama yuko ndani.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital leo Agosti 24, 2020, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe George Kyando, amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote kwa kuwa Mwenyekiti huyo hajakamwatwa na kwamba hata kama Jeshi la Polisi linafanya utaratibu wa kumkamata lakini bado hajakamatwa.

''Mbona hajakamatwa, mimi ninavyofahamu hajakamatwa kama una simu yake mpigie umuulize akwambie yuko ndani, mimi ndiye RPC wa songwe ninavyokwambia sasa hivi Mwenyekiti wa CHADEMA Tunduma hajakamatwa'', amesema RPC kyando.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa Twitter, Mgombea Urais wa CHADEMA Tundu Lissu aliandika kuwa, ''Jeshi la Polisi Tunduma Mkoa wa Songwe limemkamata Mwenyekiti wa CHADEMA Tunduma na mgombea Udiwani Kata ya Majengo Boniface Mwakabanje, na linawatafuta wagombea wengine wanne kwa tuhuma za uongo za uraia, licha ya njama hizi, CCM Songwe haitakwepa kimbunga cha Uchaguzi Mkuu

YALE YALE!!! Ya RPC KILIMANJARO na mawe ya Hai.

Maneno ya Lisdu ni ya kweli maana leo asubuhi nimesema niko Songwe na nimemsikia kiongozi wa UVCCM kwa mdomo wake akisema kwa kura Ccm haita shinda hivyocwana wapunguza kwa kushirikiana na dola na tume..
 
Huyo YEHODAYA, aliwahi kujitangaza humu kuwa anaomba tenda ya kumuua Lissu na haukupita muda Lissu akamiminiwa risasi. Labda anasahau JF kwa utunzaji wa kumbukumbu...ushahidi upo
Nishaanza kumfuatilia , nashukuru kwa kunikumbusha mkuu
 
Kama sio raia..miaka yote ameishi vipi bila ya vibali?Tulia nae Mzambia
Halafu kwenye pingamizi kuna hicho kipengele cha kumpinga mtu kama sio raia. Kwanini wasiache aka pingwe na wagombea wenzake? Hadi polisi wasaidie?? Nini kiko nyuma ya hili jambo? Polisi aata haribu huu uchaguzi.
 
Mabomu yanapigwa mda huu kituo cha polisi Tunduma, wananchi wameandamana wanataka Polisi wamwachie mgombea Udiwani wa Chadema kata ya Majengo Boniface Mwakabanje ambaye anashikiliwa kituoni hapo tangu jana usiku kwa tuhuma za kutengenezwa na Polisi kwamba sio raia wa Tanzania

Hii ni tweet ya Hilda Newton mwanachadema

Tuletee na mrejesho wa namna walivyofurushwa kama mende
 
Mabomu yanapigwa mda huu kituo cha polisi Tunduma, wananchi wameandamana wanataka Polisi wamwachie mgombea Udiwani wa Chadema kata ya Majengo Boniface Mwakabanje ambaye anashikiliwa kituoni hapo tangu jana usiku kwa tuhuma za kutengenezwa na Polisi kwamba sio raia wa Tanzania

Hii ni tweet ya Hilda Newton mwanachadema
Mbona ndugu yake anayegombea kupitia CCM hakamatwi, haiwezekani na haitatokea mpapai ukazaa mapapai na nazi.
 
Ndio kilichobaki na wengi waliopo kwenye vyombo vya ulinzi hasa polisi waliingia kwaajili ya ajila tu. So kikiwaka wote hutawaona watatawanyika mpaka kiranja wao.
kwani wengine wameingia kweny vyombo vya ulinz kwa ajili ya Nini mzee Kama sio ajira.
 
Back
Top Bottom