Tunduru: Judith Sichalwe (29) sasa kuhamishiwa Mjini, ni baada ya kuzaa Mapacha wanne

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
MTATIRO AAGIZA MWALIMU ALIYEZAA PACHA WANNE KUHAMISHIWA MJINI

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kuanza mchakato wa kumhamishia kwenye shule iliyoko Tunduru mjini Mwalimu Judith Sichalwe mwenye miaka 29 (mwanamke anayeonekana kwenye picha) ambaye amejifungua watoto wanne bila upasuaji katika hospitali ya Wamisionari ya Mbesa iliyoko Tunduru.

DC Mtatiro ametoa maelekezo hayo alipomtembelea Mwalimu huyo katika kijiji cha Mkapunda katika Shule ya Msingi Mkapunda iliyoko kilomita 100 kutoka Tunduru Mjini ambako anafundisha.

Mtatiro ameeleza ni wajibu wa serikali ya wilaya ya Tunduru kumrahisishia maisha mwalimu huyo ambaye anaweza kukabiliwa na hatari ya kushindwa kumudu gharama za maisha kutokana na idadi hiyo ya watoto wachanga kwa wakati mmoja.

Afisa Tarafa wa tarafa ya Nalasi ambako mwalimu Judith anaishi, Salumu Kijumu, ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuratibu misaada mbalimbali, lakini pia amewaomba watanzania wote watakaoguswa na kazi ya malezi ya pacha hawa wanne kumsaidia mwalimu huyo.

DC Mtatiro ameelekeza kuwa mtanzania atakayeguswa na akahitaji kumsaidia Mwalimu Judith Sichwale asisite kuwasiliana na Mwalimu Judith moja kwa moja kupitia namba ya Tigo 0673 103 536 iliyosajiliwa kwa majina Judith Sichwale.

Na Nuru I. Koba,
Tunduru,
26 Juni 2022.
IMG-20220626-WA0008.jpg
IMG-20220626-WA0010.jpg
IMG-20220626-WA0007.jpg
IMG-20220626-WA0009.jpg
 
Baba wa watoto anasemaje? Why ahamishwe je hakuna huduma muhimu?ni changamoto gani zitamkabili akibaki hapo? je mme wake nayeye mwalimu ninamaswali mengi fikirishi niishie hapo wenye chochote namba hiyo juu kama tulivo achiwa neno la upendo na mwl Nyerere tuendelee kupendana watz ni wamoja tumuwezeshe mama mapacha wa nne.
 
Hivi huu upumbavu wa ma DC na ma RC kutembea na majeshi nyuma bado unaendelea?
Nilidhani alikufa nao Jiwe.
Waaafrika tunapenda sana sifa na kutukuzwa
 
MTATIRO AAGIZA MWALIMU ALIYEZAA PACHA WANNE KUHAMISHIWA MJINI

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kuanza mchakato wa kumhamishia kwenye shule iliyoko Tunduru mjini Mwalimu Judith Sichalwe mwenye miaka 29 (mwanamke anayeonekana kwenye picha) ambaye amejifungua watoto wanne bila upasuaji katika hospitali ya Wamisionari ya Mbesa iliyoko Tunduru.

DC Mtatiro ametoa maelekezo hayo alipomtembelea Mwalimu huyo katika kijiji cha Mkapunda katika Shule ya Msingi Mkapunda iliyoko kilomita 100 kutoka Tunduru Mjini ambako anafundisha.

Mtatiro ameeleza ni wajibu wa serikali ya wilaya ya Tunduru kumrahisishia maisha mwalimu huyo ambaye anaweza kukabiliwa na hatari ya kushindwa kumudu gharama za maisha kutokana na idadi hiyo ya watoto wachanga kwa wakati mmoja.

Afisa Tarafa wa tarafa ya Nalasi ambako mwalimu Judith anaishi, Salumu Kijumu, ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuratibu misaada mbalimbali, lakini pia amewaomba watanzania wote watakaoguswa na kazi ya malezi ya pacha hawa wanne kumsaidia mwalimu huyo.

DC Mtatiro ameelekeza kuwa mtanzania atakayeguswa na akahitaji kumsaidia Mwalimu Judith Sichwale asisite kuwasiliana na Mwalimu Judith moja kwa moja kupitia namba ya Tigo 0673 103 536 iliyosajiliwa kwa majina Judith Sichwale.

Na Nuru I. Koba,
Tunduru,
26 Juni 2022.
View attachment 2273233View attachment 2273234View attachment 2273235View attachment 2273236
Hapa kwenye picha yupo wapi
 
Mtatiro ndio kanenepa hivi,, kwel pesa ni sabuni ya roho
Huyu jamaa hata akiwa chuo na baada kuingia siasa alionekana kuwa na mwili so hapo alipo ni sehemu ya mwili wake.

🎶Yote kwa yote tumpe kongore na zawadi mwalimu aliyetuletea wajukuu wanne kwa mpigo duniani.
 
Kwani Kuwasiliana kuna uhusiano gani na usajili wa laini?
 
Mianasiasa bana!

Kulikuwa na ulazima kweli wa kuvihangaisha vimalaika hivi kupiga navyo picha?
Babu nawe[emoji23] historia hiyo[emoji23]

Nilivyoenda huko mbesa nilikuta haka ka habari kanatrend

Wazungu wa hapo hospital waliomba wakabidhiwe watoto wawili walee,wazazi wamegoma.
 
Hivi huu upumbavu wa ma DC na ma RC kutembea na majeshi nyuma bado unaendelea?
Nilidhani alikufa nao Jiwe.
Waaafrika tunapenda sana sifa na kutukuzwa
Watakwambia Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
All in all,amefanya jambo jema kwa kweli kwenda kumuona but na makamera ya vidio si sawa.
Nimeona kwenye habari ITV wazazi wa hao mapacha wakiomba msaada.
 
baba wa watoto anasemaje? why ahamishwe je hakuna huduma muhimu?ni changamoto gani zitamkabili akibaki hapo? je mme wake nayeye mwalimu ninamaswali mengi fikirishi niishie hapo wenye chochote namba hiyo juu kama tulivo achiwa neno la upendo na mwl Nyerere tuendelee kupendana watz ni wamoja tumuwezeshe mama mapacha wa nne.
Wewe baki na ufupi wa akili zako
 
Back
Top Bottom