Mbali na semi nyingi zinazotrend kuhusu kutafuta hela kama vile..
1. Tafuta hela V8 sio gari ya serikali
2. Tafuta hela kitanda hakikai kwenye kona[emoji23]
3. Tafuta hela wanawake hawakai mbali na simu [emoji23]
Na nyingine kibao..
Hu usemi wa tafuta hela ndugu sio wachache nimeamini. Sina kiasi hicho ila namshukuru Mungu angalau kidogo naweza hata kula mara 3 kwa siku. Sasa ndugu zangu sijui wananionaje aisee. Unapigwa mizinga mpaka unatamani kuzima simu. Kwa siku lazima upokee simu 2 mpaka 4 sijui mie mtoto wa fulani, mie fulani, siku ya mwisho anataka hela imsaidie jambo fulani duh... ndugu zangu mie sina hela kihivyo maisha ni magumu kama lilivyo jina langu.
Tafuta hela uache kusumbua ndugu.